HEADER AD

HEADER AD

WADAU WA HABARI AKIWEMO PKM, LAKAIRO, MARA ONLINE WAFUNGUKA KUHUSU DIMA ONLINE

Na Mwandishi Wetu, Mara

WANANCHI katika mkoa wa Mara wamekipongeza Chombo cha Habari cha Mtandaoni 'DIMA ONLINE BLOG' kupitia Tovuti ya www.dimaonline.co.tz kwa kile walichoeleza kwamba habari zinazoripotiwa zinagusa Jamii na zinachochea uwajibikaji.

Wakizungumza na DIMA ONLINE kwa nyakati tofauti wamesema kuwa habari za DIMA ONLINE zimekuwa zikileta matokeo chanya zikiwemo habari za uchunguzi kwakuwa zinaporipotiwa mamlaka husika huchukua hatua na zinakuwa na uwajibikaji.

Wadau wa habari wameupongeza uongozi wa DIMA ONLINE na kutoa michango yao ya fedha ili zisaidie kununua vifaa vya ofisi kwa kile walichosema kuwa ni kuunga jitihada nzuri zinazofanywa kutokana na usimamizi mzuri katika kuhakikisha Jamii inapata taarifa za kweli na za uhakika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PKM ambaye ni mkazi wa Nyamongo wilayani Tarime ,Kibiba Machage amesema kuwa anatambua umuhimu wa vyombo vya habari kwakuwa vinawawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali.

       Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PKM ambaye ni mkazi wa Nyamongo wilayani Tarime ,Kibiba Machage.

Amewahimiza wananchi kuendelea kusoma habari mbalimbali kwakuwa kupitia Taarifa hizo watajifunza mengi na wataelimika.

Kibiba kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kuhabarisha umma amekichangia fedha chombo hicho cha habari kiasi cha Tsh. Milioni moja( 1,000,000).

"Kupitia vyombo vya habari tunapata Taarifa mbalimbali zikiwemo zinazofanywa na Serikali, jamiii, hivyo ni jukumu letu wananchi au wadau wa habari kuvisapoti vyombo vya habari ili viweze kujiendesha.

" DIMA ONLINE ni chombo cha habari ambacho mmiliki wake ni Mwanamke mtoto wa nyumbani amekuwa akijitahidi sana kutuhabarisha bila woga na habari zake ukizifuatilia ni za kweli. Hivyo nimewiwa kumchangia Tsh. Milioni moja angalau zimsaidie kununua vitendea kazi vya ofisi" amesema Kibiba.

Mmiliki wa Hoteli ya Lakairo iliyopo mkoani Mwanza ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara, Lameck Airo amempongeza mmiliki wa chombo hicho cha habari Dinna Stephano Maningo kwa kufanya Uzinduzi wa chombo chake cha habari ili wananchi wakitambu.

     Aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara, Lameck Airo

Airo amesema kuwa uzinduzi huo utasaidia wananchi kukifahamu chombo cha habari cha DIMA ONLINE kutokana na matangazo mbalimbali ya Uzinduzi yaliyotangazwa kupitia mitandao ya kijamii, Uzinduzi ulioshirikisha wananchi ana kwa ana waliotoka katika maeneo mbalimbali.

Airo ameichangia DIMA Online kiasi cha Tsh. Laki tano (500,000) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi huku akimwomba mmiliki Kusimamia vyema chombo hicho ili kiwasaidie wananchi katika kupata taarifa mbalimbali zikiwemo zinazowagusa wananchi wanaokabiliwa nachangamoto mbalimbali zikiwemo huduma za afya.

" Nampongoza Dinna kwa kuamua kuwa na chombo chake cha habari, hii ni hatua kubwa sana, namwombea azidi kufanikiwa katika kazi yake ya upashaji habari, hivyo katika kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika taifa letu namchangia Tsh. 500,000." Amesema Airo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri mkuu wa Gazeti la Sauti ya Mara,  Blogu ya Mara Online, pamoja na Gazeti la Kingereza la Lake Zone watch, Jacob Mugini amempongeza mmiliki kwa kufanya uzinduzi ambapo amemchangia Tsh. Laki moja ( 100,000).

      Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri mkuu wa Gazeti la Sauti ya Mara, Blogu ya Mara Online, pamoja na Gazeti la Kingereza la Lake Zone watch, Jacob Mugini.

Jacob amesema kuwa amefurahishwa kwa Mwandishi wa Habari Mwanamke kuweza kufungua chombo chake cha habari ambacho kitampa nafasi akiwa kama Mwandishi wa Habari kuandika mambo mengi zaidi na kufikia ndoto zake ambazo yeye anazitaka.

" Kumekuwa na baadhi ya vyombo vya habari vya Online) (Kimtandao) ambavyo havitoi habari zinazofuata maadili au taaluma, kwahiyo ushauri wangu chombo chake kiweze kujitenganisha na vyombo vingine vya Online kifanye stori za kitaaluma" amesema Jacob 

Jacob amesema kuwa amefurahishwa kwa hatua ya DIMA ONLINE "  Nipongeze kwa kuchangia Tsh. 100,000 kwani nimefurahi nami niwe sehemu ya kuwezesha ili isonge mbele.

"Tukiwa na Waandishi ambao wamepiga hatua basi sekta ya habari itaendelea kukua. Dinna nakutia moyo usonge mbele" amesema Jacob.

Mweka hazina wa Chama cha Wasioona Wilaya ya Tarime, Abia Orindo amesema " Dinna ni rafiki yangu ni mwanamke anayejituma kwenye kazi yake, mchapa kazi na asiye kata tamaa, chombo chake kinajitahidi kutupatia taarifa kutoka mikoa mbalimbali namchangia Tsh. 100,000" amesema Abia.

Stephano Maningo baba mzazi wa mmiliki wa DIMA ONLINE amesema mwanae kwa miaka mingi amekuwa akijitahidi kufanya kazi yake ya uandishi wa habari kwa bidii bila kukata tamaa.

" Dinna anaipenda kazi yake licha ya magumu anayopitia katika kazi yake ya uandishi wa habari, nampongeza sana kwa kujituma. Namuunga mkono kwa kumchangia Tsh. 500,000 na ng'ombe mmoja jike ili awe anakamua anywe maziwa" amesema Stephano. 

Oktoba, 8, 2023 Chombo cha Habari cha DIMA ONLINE kilizinduliwa Rasmi, Uzinduzi ulifanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ingwe- Nyamongo ambapo wananchi na wadau wa habari walishiriki na kuchanga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi ya DIMA ONLINE Nyamongo na Tarime Mjini.



Katika uzinduzi huo jumla ya Tsh. Taslimu Milioni 10 zilichangwa na ahadi zaidi ya Tsh. Milioni 30 zikiwemo Dolla elfu kumi zilizoahidiwa na wadau wa DIMA ONLINE waishio nchini Marekani.

Baadhi yao waliochanga fedha ni pamoja na aliyekuwa mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa DIMA ONLINE, Bhoke Bwiso mkazi wa Nyamongo aliyechangia Tsh. 1,000,000, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PKM mkazi wa Nyamongo alichangia Tsh. 1,000,000. 

    Aliyesimama kulia ni Mjasiliamani Bhoke 
Bwiso aliyekuwa mgeni Rasmi Uzinduzi wa DIMA ONLINE 

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni mlezi wa Kikundi cha Waandishi wa habari Wanawake wenye maono Mkoa wa Mara na Mweka hazina Shirika la Jicho la Tanzania Joyce Sokombi alichangia Tsh. 1,000,000.

    Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara,(aliyesimama) ambaye pia ni mlezi wa Kikundi cha Waandishi wa habari Wanawake wenye maono Mkoa wa Mara na Mweka hazina Shirika la Jicho la Tanzania, Joyce Sokombi.

Wengine ni John Onaka, Malima Mafuru na Samwel Ojolo ambao ni wakazi wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara walichanga Tsh. 900,000, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya RIN. Co. LTD. Isaack Chale Range alichangia Tsh. 500,000, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya Tarime Tsh. 100,000.

Diwani wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi ( CCM) Felister Julius Range mkazi wa Nyamongo amechangia Tsh. 200, 000. Diwani Viti Maalum Eliza Marembela mkazi wa Nyamongo ametoa Tsh. 50,000.

Wengine ni Steven Wambura Tsh. 200,000, Chacha Sultani 100,000, Henry Kiula 50,000, Happens Bonifas Tsh 50,000, Anna Shadrack Tsh. 30,000, Yohana Wambura 50,000, Neema Enock 20,000, Ghati Enock 10,000, Ester Mseti. Tsh. 10,000, Mwl Mekaus Maingu Tsh. 20,000, Mariam Tura Tsh. 20,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WARACHA LTD David Ryoba Tindo Mkazi wa Nyamongo - Tarime, amechangia 300,000, Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Mark Njera amechangia Tsh. 100,000 na Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Kemanyaki LTD Nicolaus Mgaya amechangia Tsh. 100,000.

        Diwani wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi ( CCM) Felister Julius Range 

Baadhi ya Waandishi wa Habari walishiriki katika uzinduzi huo na kuchanga Tsh. 200,000.

Familia ya Julius Orindo imechangia Tsh. 400,000, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Turwa Marwa Timoro Tsh. 50,000, Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki amechangia Tsh. 100,000.

Baadhi ya ndugu wa mmiliki wa DIMA ONLINE waliichaga fedha ni pamoja na baba zake wadogo, Lazack Maningo katoa Ng' ombe mmoja jike na Tsh.50,000, Sadoki Maningo katoa ng'ombe mmoja dume na Tsh. 50,000, Shangazi zake, Sefloza Maningo Tsh. 200,000 na Msabhati Maningo Tsh. 50,000.

Ndugu wengine ni pamoja na Maria Stephano Maningo ameichangia DIMA ONLINE Tsh. 200,000, Rhobi Stephano Maningo, Tsh. 100,000, Waziri Stephano Maningo 50,000, Oliver Stephano Maningo Tsh. 50,000, Staroni Lazack Maningo, Tsh. 40,000, Yusuph Lazack Maningo Tsh. 30,000, Mrimi Juma Maningo Tsh. 30,000, Maningo Sadok Tsh. 30,000.

Suzy Marwa Maningo Tsh.20,000, Aloyce Rhobi Marwa Maningo Tsh. 50,000, Ngoko Marwa Maningo Tsh. 20,000, Ester Marwa Maningo Tsh 30,000, na Mkami Wambura Nyamoha Tsh. 20,000.

Uongozi wa DIMA ONLINE akiwemo mmiliki Dinna Stephano Maningo, Mkurugenzi Mtendaji wa DIMA ONLINE, Rose Joseph Kimaro wamewashukuru wananchi walioshiriki kwenye uzinduzi na kuchanga fedha ununuzi wa Vifaa vya ofisi huku wakiahidi kufanya kazi kwa bidii za kuhabarisha umma.

Mmiliki wa DIMA ONLINE Dinna Stephano Maningo aliyebeba kikapu akiwa na Waandishi wa habari.

       Mkurugenzi Mtendaji wa DIMA ONLINE,Rose Joseph Kimaro 
              Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Mark Njera.


        Diwani wa Viti Maalum Eliza Marembela mkazi wa Nyamongo 
           Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Turwa Marwa Timoro.

        Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki 
        Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Kemanyaki LTD Nicolaus Mgaya amechangia Tsh. 100,000.





No comments