WATUMISHI OFISI YA RC MARA WAFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA
Na Shomari Binda, Musoma
MADAKTARI na wauguzi kutoka hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inaendelea na zoezi la kuzunguka maeneo mbalimbali na kutoa huduma ya uchunguzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Wataalam hao wameweka kambi kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara na kuwafanyia uchunguzi watumishi na wananchi walio jirani na ofisi hizo.
Baadhi ya watumishi waliofanyiwa uchunguzi wa afya wameshukuru kufikiwa na huduma hiyo kwenye maeneo yao ya kazi.
Mmoja wa wstumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara akifanyiwa uchunguzi wa macho kutoka kwa wataalam wa hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.Wamesema mara nyingi wanaamkia kwenye majukumu ya kazi ofisini na kukosa nafasi ya kufanya uchunguzi wa afya na huduma hiyo imewasaidia.
Wameongeza kuwa wamekuwa wakifika hospitalini pale wanapokuwa wameugua ili kutibiwa na sio kwenda kufanya uchunguzi wa afya.
" Tunaishukuru hospital ya kumbukimbu ya Mwalimu Nyerere kwa huduma hii ambayo wametuletea kwenye maeneo yetu ya kazi.
" Wametueleza umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya kila baada ya muda na tutakwenda kuzingatia ushauri tuliopewa",amesema Abdulratif Rajabu.
Mganga Mfawidhi wa hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk.Osmund Dyagura amesema zoezi hilo ni endelevu katika kufanya uchunguzi wa afya.
Amesema kabla ya wataalam hao kufika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa tayari wameyafikia maeneo mbalimbali yakiwemmo makanisa na misikiti ili kuendesha zoezi la magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Zoezi la upimaji magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa limeambatana na upimaji macho pamoja na upimaji wa virusi vya ukimwi kutoka kwa watoa huduma na madaktari wa hospitali ya rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu J.K Nyerere.
Huduma hiyo ilihusisha watumishi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa,taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali pamoja na wananchi mbalimbali waliyokuwa eneo hilo.
Dyagura amesema huduma zilizokuwa zikitolewa zilikuwa ni upimaji wa kisukari, shinikizo la damu,urefu na uzito,upimaji mach,upimaji wa virusi vya ukimwi pamoja na ushauri.
Post a Comment