HEADER AD

HEADER AD

TAARIFA YA UTENDAJI KAZI WA DIMA ONLINE KWA KIPINDI CHA SEPTEMBA, 21, 2022 HADI SEPTEMBA, 20,2023



>> Jumla ya habari 566 zimeripotiwa.

>>Mkoa wa Mara unaongoza kwa habari nyingi ukifuatiwa na mkoa wa Dar es Salaam.

Na DIMA ONLINE

IFUATAYO ni Taarifa ya utendaji kazi wa DIMA ONLINE BLOGU kwa kipindi cha Mwezi Septemba 21, 2022 hadi Septemba, 20, 2023.

Awali ya yote Uongozi wa DIMA ONLINE  unamshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema kwa kuwawezesha afya njema viongozi na waandishi wa habari kuendelea kuitumikia DIMA Online katika kuhakikisha habari zinaripotiwa ili kuwezesha wananchi kupata habari mbalimbali.

Pia kuwawezesha wasomaji kuendelea kufuatilia na kusoma habari mbalimbali kupitia DIMA ONLINE.

DIMA ONLINE ni Chombo cha Habari cha Mtandaoni yaan 'BLOGU' kupitia Tovuti ya www.dimaonline.co.tz, mtandao wa Instagram kupitia akaunti ya dima_onlinenews na Twitter : dimaonline255, kinachomilikiwa na mtu Binafsi Mwandishi wa Habari Dinna Stephano Maningo mkazi wa wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.

Chombo hiki cha habari kina Mkurugenzi Mtendaji aitwaye Rose Joseph Kimaro na wafanyakazi wengine wapatao 12 waliopo katika mikoa mbalimbali.

Makao makuu ya Ofisi ya DIMA ONLINE yapo mtaa wa Rebu Senta Mjini Tarime.

Ndugu wasomaji wa DIMA ONLINE, awali habari zilianza kupostiwa kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram  na Twitter tarehe 21mwezi wa tano, mwaka 2022.

Hata hivyo, tarehe 21, Mwezi Septemba, mwaka 2022, BLOGU ya DIMA ONLINE ilisajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mmiliki kukabidhiwa leseni ya uendeshaji wa Maudhui ya kimtandao na habari kupostiwa  kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania na nje ya Nchi.


Chombo cha Habari cha DIMA ONLINE kipo kwa lengo la kuihabarisha jamii habari mbalimbali zikiwemo habari za Kijamii,Habari za Uchunguzi,Michezo/ Burudani,Uchumi/ Biashara, Kilimo,Utawala Bora,Jinsia,Makundi Maalumu, Elimu, Afya,Sayansi,Teknolojia na Ubunifu.

MALENGO YA DIMA ONLINE 

Malengo ya kuanzishwa DIMA ONLINE ni ;

1.Kuhakikisha habari zinapostiwa punde tu zinaporipotiwa na Waandishi wa Habari.

2.Kuhakikisha DIMA ONLINE inawajibika vilivyo katika kukusanya habari kupitia Vyanzo vyake mbalimbali vya Habari.

3. Kuchakata habari, Kuziandika kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari, miiko ya uandishi wa habari na maadili ya uandishi wa habari kama vile kuhakikisha habari haziegemei upande mmoja (Balance) na kutoandika uongo.

4.Kuelimisha Jamii, Kuburudisha na kukosoa.

5.Kuibua habari zilizofichika kama njia ya kuisaidia Serikali kujua yaliyojificha ili yafanyiwe kazi lakini pia kuchochea uwajibikaji kwa mamlaka husika na jamii kwa ujumla.

6.Kuhakikisha habari nyingi ni za kutoka kwa wananchi ili kupaza sauti za wananchi hususani wa vijijini.

7.Kuandika habari ambazo zitapelekea kuibuka kwa hoja na mijadala katika jamii na mamlaka mbalimbali ili kuleta utatuzi.

8.Kuandika habari za maendeleo yaliyofanywa na Serikali, Taasisi, Kampuni, Mashirika katika nyanja mbalimbali mf. miradi ya maendeleo n.k.

9.Kuhakikisha habari zinazoripotiwa zinakuwa chachu, zitakazowavutia wasomaji katika kujipambanua kifikra, zitakazosaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

SABABU YA KUANZISHWA BLOGU YA DIMA ONLINE

Blogu hii ilikuwa ni ndoto na matarajio ya mmliki wa chombo hiki aliyoifikiria kuianzisha kwa miaka kadhaa iliyopita.

Hata hivyo kulingana na changamoto za kifedha ilichelewa kuanzishwa ambapo mmiliki aliamua kuanzisha chombo hicho cha Habari kupitia mitandao ya kijamii Twitter na Instagram.

Kutokana na Habari kusomwa na watu mbalimbali kupitia mitandayo hiyo ya kijamii, DIMA ONLINE katika kukusanya maoni ya wasomaji, baadhi ya wasomaji walitoa maoni yao wakiomba ianzishwe Blogu .

Kwakutambua umuhimu wa wasomaji, mmiliki wa chombo hiki cha Habari akasajiri Blogu ambayo hadi sasa inaendelea kufanya kazi ya kuhabarisha wananchi ndani ya nchi na nje ya nchi.

MAFANIKIO 

Blogu ya DIMA ONLINE imesaidia habari hasa makala kupostiwa ikiwa imekamilika yote tofauti na hapo awali makala zilipostiwa Instagram taarifa nusu nusu kitendo ambacho wasomaji walishauri ianzishwe Blogu ili kuwawezesha kusoma makala kwa urefu na kwa urahisi bila usumbufu.

Katika Kipindi cha mwaka mmoja tangu DIMA ONLINE isajiliwe rasmi Tarehe, 21, Septemba, 2022 hadi Septemba, 20, 2023. imefanikiwa kuposti habari na Makala mbalimbali jumla ya Posts  zote ni 566.

Habari zimeripotiwa katika makundi mbalimbali kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa DIMA ONLINE Septemba 21,2022.

Habari za Kitaifa ni 221, Afya habari 39,Barabara habari 20, Biashara/uchumi 18, Dini 9, Elimu 27, Habari Kimataifa 15, Habari Mchanganyiko 16, Kijijini kwetu habari 20, Kilimo 6, Majanga 1, Maji, 9,Makala, 13, Makundi maalum habari 5, Maliasili/ Utalii ni 15, Mazingira 6, Michezo /Utamaduni 18, Mifugo/ Uvuvi12, Mila/ Utamaduni 11, Ndoa/Mahusiano 2.Polisi 15, Siasa 30, Teknolojia/Ubunifu 5 na Watoto 7.

Habari zimeripotiwa katika baadhi ya mikoa ambapo mkoa wa Mara unaongoza kwa habari nyingi zipatazo 176 zilizopostiwa kwenye Blogu, Dodoma habari 20, Mwanza 15, Mbeya 5, Manyara habari 07,  Arusha 07, Shinyanga 9, Dar es Salaam 75, Simiyu 57, Kagera 40, Tanga 22, Pwani 22, Lukwa 09, Lindi 02, Kigoma 03, Geita 12, Morogoro 4 Mtwara 7, Ruvuma habari 5, , Mbeya 3,  Njombe 2, Kilimanjaro 4, Iringa 9, Tabora 9, Songwe  habari 1 na Zanzibar habari 16 .  Kati ya mikoa hiyo Jumla Habari za kimkoa ni 551 na habari za Kimataifa ni habari 15.

Kupitia DIMA ONLINE baadhi ya waandishi wa habari wamefanikiwa kupata mafunzo / Semina ya uandishi wa habari zikiwemo habari za uchunguzi na kazi mbalimbali za kihabari kutoka kwa wadau wa habari
 .


CHANGAMOTO

Kati ya siku 365 za mwaka, DIMA ONLINE imeposti habari siku 299 ambapo siku 66 katika mwaka hazikupotiwa habari mtandaoni.

Sababu ya Habari kutopostiwa ni kutokana na mazingira ambayo wakati mwingine kutokuwepo kwa mtandao, miingiliano ya shughuli zingine nje habari inayochangia habari kutokusanywa kwa wakati ili zipostiwe.

Wakati mwingine kukosekana kwa kifurushi cha bando yaani MB. ,pia pale mfanyakazi anapougua hupumzika kutofanya kazi kwa muda.

DIMA ONLINE ni chombo cha habari kipya bado hakijaanza kupokea matangazo ya biashara.

Mkakati uliopo ni kuzidi kutatafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kiweze kujiendesha.

Ofisi ya DIMA Online ina uhaba wa vitendea kazi kama vile Camera, Kompyuta, vifaa vya kurekodi, samani za Ofisi na vifaa vinginevyo.

Hakuna vitendea kazi kama komputa, Camera,kifaa cha kurekodi sauti wakati wa kukusanya habari kutoka kwenye vyanzo vya habari kama njia ya kutunza kumbukumbu,kwani mwandishi anaishia tu kuandika kwenye notbook ambapo taarifa zingine anazikosa pale asipokuwa makini kusikiliza au kuandika.

Kutofanikiwa kuripoti habari kutoka Mikoa yote nchini kutokana na ukosefu wa fedha za kuwalipa waandishi wa habari jambo ambalo limesababisha. Baadhi ya mikoa kutokuwa na maripota wa DIMA Online.

Waandishi wa Habari kutoripoti habari za vijijini kadri inavyohitajika  kila siku kwakuwa DIMA Online ni chombo kichanga hivyo hakijapata fedha za usafiri kuwawezesha waandishi wa habari kufuatilia habari vijijini.

Baadhi ya viongozi kutotoa ushirikiano wa habari na hivyo kusababisha habari kutoripotiwa kwa wakati licha ya Katiba ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 kusisitiza haki ya uhuru wa mawazo, haki ya kila mtu kutoa mawazo na haki ya kupewa taarifa. 

Hata hivyo Katika Uzinduzi WA DIMA ONLINE uliofanyika Oktoba, 8, 2023 Nyamongo- Tarime wananchi na wadau wa habari walichanga fedha kiasi cha Tsh.Milioni 10 na ahadi zaidi ya Tsh. Milioni 30 zikiwemo ahadi za Dolla elfu kumi kutoka kwa wadau wa DIMA ONLINE waishio nchini Marekani.

Fedha hizo ni kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi za DIMA ONLINE Tarime mjini na Nyamongo ambapo baadhi ya vifaa vitanunuliwa na kadri pesa zitakapotimia kwa mujibu wa ahadi zilizotolewa zitatekeleza mahitaji yote ya vitendea kazi.

MAONI YA WASOMAJI WA DIMA ONLINE

Wasomaji wa DIMA Online pamoja na kuvutiwa na habari kupitia chombo hiki cha habari wamekuwa wakitoa maoni yao ili kuongeza ufanisi na uboreshaji.

Wasomaji wameshauri kuongezwa Waandishi wa habari kuripoti habari toka Mikoa mbalimbali nchini ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa taarifa kama njia ya kuiwezesha DIMA ONLINE kujulikana zaidi na kuwafikia watanzania wengi.

Kuongeza juhudi katika kazi ili habari zipostiwe kila wakati.

DIMA ONLINE iendelee kuibua habari kwakuwa habari za DIMA zimekuwa na mrejesho chanya kwa jamii.

Ubunifu na uandishi wa habari za uchunguzi ili kuibua yaliyofichika ndani ya jamii yaweze kutafutiwa ufumbuzi na kupaza sauti za wananchi.

DIMA ONLINE ianzishe TV Online ili hiendelea kuhabarisha wananchi kupitia YouTube channel.

MIKAKATI NA MATARAJIO YA DIMA ONLINE
 
Ndugu wasomaji DIMA ONLINE imepokea maoni ya wananchi katika kuongeza uboreshaji na imeahidi kuiboresha ili izidi kukua na kuaminiwa.

DIMA ONLINE inatarajia kuendelea kuongeza Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa kazi na upatikanaji wa habari hususani habari za kijamii.

Kuibua habari zilizofichika zikiwemo za makundi maalumu ya Watu wenye Ulemavu,Wazee,Yatima,Wajane na Waghane, pamoja naChangamoto mbalimbali za kijami.

Kujifunza ujuzi mbalimbali kupitia TEHAMA ili Online hizidi kuhimarika.

Kutafuta vyanzo vya mapato ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa chombo hiki.

Kuwa na ubunifu katika uandishi wa habari.

Kuanzisha TV online kupitia YouTube channel baada ya uzinduzi ili Habari na Makala zipostiwe.

Kufungua ofisi nyingine Nyamongo ya DIMA ONLINE ili kuwasogezea wananchi huduma karibu ya maswala ya kihabari.

Pia Malengo ya ofisi ya DIMA ONLINE kwa miaka ya mbeleni tunatarajia kuja kuanzisha Kituo cha Redio na Runinga. yaani (Television).

Wasomaji wa DIMA ONLINE waendelee kufuatilia na kusoma habari zitakazo waelimisha na kuwafurahisha.

Tunawashukuru nyote mlioungana nasi katika kutembelea blogu , Twitter na Instagram ya DIMA Online. Mwenyezi Mungu awabariki.

Taarifa hii imetolewa na uongozi wa DIMA ONLINE.

MUNGU IBARIKI DIMA ONLINE,MUNGU WABARIKI WASOMAJI WA DIMA ONLINE MUNGU IBARIKI TANZANIA.







No comments