HALIMA MDEE MGENI RASMI FAINALI YA MASHINDANO YA ESTER BULAYA CUP 2023
Na Shomari Binda, Bunda
MBUNGE wa viti maalum Halima Mdee anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya Ester Bulaya Cup 2023.
TIMU ya Bunda Sports Kids na Sazira fc zinakutana kwenye mchezo wa fainali wa mashinsano ya Ester Bulaya Cup 2023 utakaofanyika leo Novemba, 12, 2023.
Fainali hiyo itafanyika kwenye uwanja wa sabasaba itatanguliwa na michezo mbalimbali ikiwemo ya bao,karata pamoja na draft.
Mchezo wa fainali ya timu za soka za wanawake kati ya timu ya Bunda Queen na Bunda Kids zitacheza mchezo wa fainali utakaochezwa kuanzia majira ya saa 5 asubuhi.
Tayari mashabiki wa timu zote 2 wametoa tambo huku kila upande ukitamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
Upande wa mashabiki wa timu ya Sazira umesema haujafika hapo kwa bahati mbaya na watadhihilisha hilo kwa kuchukua ubingwa.
Wamesema wanayo timu nzuri iliyoonyesha ushindani tangu kuanza kwa mashindano hayo mwezi uliopita.
Kwa upande wao mashabiki wa timu ya Bunda Sports Kids wamesema wanao vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka hivyo hawana shaka na kuchukua ubingwa.
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakifatilia mashindano hayo wamesema jambo ambalo amelifanya mbunge Ester Bulaya linastahili pongezi.
Wamesema kipindi chote cha mashindano wamekuwa wakipata burudani ya kutosha na kuomba mashindano hayo yawe yanafanyika mara kwa mara.
Post a Comment