HEADER AD

HEADER AD

HOSPITALI YA BUGANDO YABAINI WATU 215 NYAMONGO WANA UZITO KUPITA KIASI


>>> Ni baada ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupiga kambi Nyamongo kutoa huduma za magonjwa yasiyo yakuambukiza

>>>Watu 102 wana shinikizo la Damu, 20 wana ugonjwa wa Kisukari na 20 wana ugonjwa wa Masikio, wengine wana matatizo ya mgongo na mifupa

>>>Tafiti za Shirika la afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa nusu ya watu wazima Duniani watakuwa na unene kupita kiasi ifikapo mwaka 2030, huku Tanzania idadi ikiongezeka kupita kiasi

Na Dinna Maningo, Nyamongo

MADAKTARI Bingwa kutoka Kliniki ya Madaktari Bingwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando mkoani Mwanza, wamepiga kambi Nyamongo Wilaya ya Tarime mkoa wa Mara kutoa huduma za uchunguzi wa afya kwa magonjwa yasiyoyakuambukiza.

Watu wapatao 506 wamepata huduma wakati wa maonesho ya ' TWENDE MARA'  yaliyoandaliwa na Kampuni binafsi ya Powerlife Organic Wellness (T) LTD yenye makao makuu Jijini Dar es Salaam ambapo kati yao watu 215 sawa na asilimia 70  wamegundulika kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi, watu 102 sawa na asilimia 21 wanashinikizo la damu (Pressure).

Pia zaidi ya watu 20 sawa na asilimia 04 wamegundulika kuwa na kisukari huku watu zaidi ya 20 wakionekana kuwa na matatizo ya usikivu na kutoboka kwa ngoma za masikio, wengine wana matatizo ya mgongo na mifupa.

Dkt Bingwa wa magonjwa ya Tiba toka Bugando Kliniki ya Madaktari Bingwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Raymond Wilson amewashauri wananchi kijenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara.

            Dkt. Raymond Wilson 

"Tuko hapa Nyamongo kwenye maonesho ya 'TWENDE MARA' tupo hapa tangu tarehe 4, Novemba, 2023, na huduma hii itatolewa hadi Novemba, 12 mwaka huu, kwa siku sita watu zaidi ya 507 wamepata huduma, kati yao zaidi ya watu 2015 wamegundulika kuwa na uzito uliopita kiasi,102 wanashinikizo la damu, zaidi ya 20 wana kisukari na 20 wana matatizo ya usikivu .

" Tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali bure, tulifika hapa kwa ajili ya kufanya matibabu, upimaji wa magonjwa hasa yasiyoyakuambukiza. Tumekuwa tukipima magonjwa ya usikivu, magonjwa ya masikio, shingo, Kisukari, Presha, uzito pamoja na ushauri kwa wateja wetu ambao wametufikia.

Dkt.Raymond amesema kuwa lengo hasa ni kutambua magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza ambayo ni tatizo kwa Dunia kwa sasa yanasababisha athari nyingi na athari ya uchumi wa inchi.
Dkt. Raymond Wilson akimsikiliza mwananchi aliyefika kupata huduma.

"Watu wengi wanakuwa na shida ya presha lakini hawajitambui kama wana magonjwa, hao tuliowapima wengi wao walikuwa hawajui kama wana matatizo ya magonjwa hayo, wengine wamepatiwa matibabu na kushauriwa, wapi ambao tumewashauri kwenda hospitali ya Kanda  Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi .

"Kuna ambao wana tatizo ya usikivu ngoma za masikio zimetoboka na sababu zingine mbalimbali zinazopelekea kupoteza usikivu, wamepata ushauri nawengine kupewa Rufaa kwa matibabu zaidi" amesema .

        Mwananchi akifanyiwa uchunguzi na Daktari Bingwa wa masikio

Dkt. huyo ameongeza "  Tunahitaji kuwafikia watu wengi tuwape elimu kwa namna gani waweze kuchukua hatua kujizuia wasiweze kupata magonjwa hayo na wengine wana matatizo ya mgongo na mifupa pengine kwa shughuli mbalimbali zinazoleta shida ya mgongo kutumia pamoja na mifupa.amesema.

Amesema asilimia kubwa ya wateja waliofika kupata huduma wanawake wanaongoza kuliko wanaume " Imegundulika hata Kwenye Kliniki zetu naomba watu wote wapende kufika kufanyiwa uchunguzi.


Anasema huduma hiyo hutolewa kwa vipindi maalum " Kama hapa tulikuja kwenye maonesho ya TWENDE MARA, pia huduma hizo tunaziendesha mara kwa  mara kwenye maadhimisho, makongamano, Warsha mbalimbali na tunazitoa kwenye maeneo yetu ya hospitali na mikoa mbalimbali ila kwa hapa Nyamongo ni mara yetu ya kwanza kufika" amesema Dkt Raymond.

Wananchi waliofika kupata huduma wamekipongeza Serikali na Hospitali ya Bugando kwa kufika kutoa huduma mbalimbali za magonjwa yasiyoyakuambukiza kwani hawakufahamu kama wanaishi na magonjwa hayo katika mihili yao.

Mkazi wa Kitongoji cha Masinki Kijiji cha Nyabichune, Suzan Magesa amesema" Tunaishukuru Serikali kutuletea karibu huduma hii kupitia Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Bugando, imetusaidia sana imetuepushia gharama za usafiri na tumejitambua Afya zetu, tumepewa maelekezo wanaelekeza vizuri.

        Mkazi wa Kitongoji cha Masinki Kijiji cha Nyabichune, Suzan Magesa

" Tunaomba waende na maeneo mengine, tunashukuru kwa kufika Nyamongo wametupunguzia gharama ambazo tungeenda kupata vipimo hospitali au kwenye maabara kucheki afya na vipimo" amesema Suzan.

Sinda Mwita Kichere mkazi wa Kitongoji cha majengo amesema " nimepata huduma nawashauri na watu wengine waje wapime kujua afya zao na hali zao zipoje washauriwe kama kuna tatizo waelekezwe au watibiwe.

     Mkazi wa Kitongoji cha majengo Sinda Mwita Kichere

Mkazi wa Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Nyangoto Laurence Muhiri amesema " nina ugonjwa wa Kisukari niliposikia kuna huduma zinatolewa na Madaktari Bingwa kutoka Bugando nimefika nikapata huduma.

"Wamenishauri vyakula ambayo natakiwa kula, niliambiwa nisitumie wanga nyingi, maziwa na vitu ambayo vina sukari nyingi. 
       Mkazi wa Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Nyangoto Laurence Muhiri

"Tunaomba wawe wanakuja mara kwa mara maana sisi tupo kwenye maeneo ya uchimbaji huduma hizi tukizipata mara kwa mara zitatusaidia"amesema.

Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Ingwe Kuyeba Onesmo amesema? Mimi nimefika nikapata huduma ya kupima presha nikaambiwa nijitahidi kunywa maji mengi.

     Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Ingwe Kuyeba Onesmo

Mwita Steven Waigama aliyepata matibabu yeye na watu watano ambao ni familia yake amesema amefurahi kwa huduma nzuri na anatamani Serikali isogeze karibu huduma ya kibingwa Nyamongo.

Zisemavyo Tafiti

Tafiti za Shirika la afya Duniani (WHO) za 2018 zinaonesha kuwa nusu ya watu wazima Duniani watakuwa na unene kupita kiasi ifikapo mwaka 2030, huku Tanzania idadi ikiongezeka kupita kiasi hali ambayo imechangia kuwepo kwa magonjwa yasiyoyakuambukiza, na kusababisha Serikali kutumia fedha nyingi katika matibabu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya utafiti kupitia kijarida sera cha kusambaza matokeo ya utafiti kilichoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa uchumi na Kijamii (ESRF), Shule ya uchumi, Chuo kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Imeelezwa;

Utafiti unaonesha kuwa Tanzania, vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoyakuambukiza vimeongezeka kutoka asilimia 19.5 hadi asilimia 32.9 kati ya mwaka 200 na 2016.

Pia mwaka 2014  watu Bilioni 2.1duniani walikuwa na uzito kupita kiasi hali ambayo imesababisha watu kupata magonjwa yasiyoyakuambukiza kama Kisukari, Moyo, na Saratani ambayo huleta athari.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti inaelezwa kuwa nchi ya Tanzania, kiwango cha kuenea kwa unene kupita kiasi umeongezeka kwa wanaume na wanawake kutoka asilimia 5.9 mwaka 2014 hadi asilimia 8.4 mwaka 2016.

Tafiti zimebaini kuwa sababu inayochangia unene kupita kiasi ni matumizi ya vinywaji vyenye kiwango cha juu cha sukari huongezeka kalori nyingi mwilini ambazo huhusishwa na kuongezeka kwa uzito uliopitiliza.

Pia kwa mujibu wa Wataalam wa afya inaelezwa kuwa uwiano wa urefu na uzito (BMI) inayotakiwa ni 18 mpaka 29.5.














Picha chini, Waandishi wa Habari wakipata huduma ya vipimo shinikizo la Damu








No comments