HEADER AD

HEADER AD

HALMASHAURI YA MUSOMA VIJIJINI YAZINDUA MPANGO WA MALEZI YA MTOTO" MMMAM"

Na Shomari Binda, Musoma

BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini limepokea  na kuzindua mpango jumuishi wa taifa wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto( PJT-MMMAM) 2021/2023 na 2025/2026.

Akizindua mpango huo mbele ya baraza hilo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Charles Magoma amesema mpango huo ni mzuri na wapo tayari kuutekeleza.

         Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Musoma Charles Magoma

Amesema mtoto anapaswa kuwa na makuzi bora pamoja na malezi na kupelekea serikali kuja na mpango huo jumuishi.

Mwenyekiti huyo amesema madiwani kwenye Kata zao kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali watahakikisha wanautekeleza kama ilivyo kusudiwa.

" Mpango huu ni mzuri na tumeupokea na kuuzindua kwaajili ya utekelezaji wake kwenye halmashauri yetu ili kufikia malengo kusudiwa.

" Serikali inayo nia njema na watoto wetu na kuja na mpango huu na sisi kama tulivyouzindua tupo tayari kutekeleza kwenye maeneo yetu",amesema Magoma.

Mkuu wa kitengo cha mipango, uchumi na maendeleo kutoka Kanisa la AICT-Tanzania Charles Mashauri wanaosimamia mpango huo ameipongeza halmashauri ya Musoma kwa kuwa ya kwanza kuzindua mpango huo.

    Mkuu wa idara ya mipango,uchumi na maendeleo wa Kanisa la AICT,Charles Mashauri

Amesema kwa maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda baada ya kuzindua kimkoa maelekezo yalitolewa kwa halmashauri zote kukamilisha uzinduzi kabla ya mwezi Novemba kumalizika.

Amesema dhamira ya serikali kuwekeza katika mpango wa malezi,malezi na maendeleo ya awali ya mtoto ni kulenga kwenye lishe pamoja na afya bora.

Mashauri amesema mpango huo wa MMMAM unaangalia pia ulinzi na usalama wa mtoto ikiwa ni pamoja na kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia,ajali,unyanyasaji wa kihisia,kimwili na ngono.

Mkuu wa kitengo cha idara ya maendeleo ya jamii Tana Nyabange, amesema kwa upande wao tayari walishaanza kuzuia vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kunzisha kamati za kuzuia vitendo hivyo kwenye vijiji 68 vilivyopo kwenye halmashauri hiyo.

      Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa halmashauri ya Musoma,Tana Nyabange

No comments