TRA MARA YAVUKA LENGO KWA KUKUSANYA KODI BILIONI 35
>> Yavuka lengo, ilipangiwa kukusanya Kodi Julai -Sepetemba Bilioni 27
Na Shomari Binda, Musoma
MAMLAKA ya Mapato Tanzania ( TRA) mkoa wa Mara imevuka malengo ya ukusanyaji wa kodi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na robo mwaka wa 2023.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Mara Nassoro Ndemo katika kilele cha wiki ya shukrani kwa walipa kodi na kutambua mchango wa walipa kodi.
Amesema kwa mkoa wa Mara kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ulipangiwa kukusanya kiasi cha Tsh.Bilioni 113 na kukusanya Bilioni 126 sawa na asilimia 111.
Ndemo amesema katika robo ya kwanza kuanzia julai hadi septemba 2023 walipangiwa kukusanya Tsh Bilioni 27 ambapo Tsh Bilioni 35 zimekusanywa sawa na asilimia 130 na kuvuka lengo husika.
Amesema hayo ni mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kupongezwa na hasa walipa kodi wa mkoa wa Mara ambao wamefanya
kazi hiyo.
Kaimu meneja huyo amesema kodi inapolipwa huiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo.
" Tuko hapa kwaajili ya kutoa shukrani kwa walipa kodi ambao wametuwezesha kuvuka malengo ya ukusanyaji wa kodi.
" Kabla ya kilele cha leo kwa kutoa vyeti vya pongezi kwa walipa kodi kwa wiki nzima tumekuwa na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa misaada kwenye vituo vyenye uhitaji",amesema Ndemo.
Akisoma hutuba ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda mkuu wa wilaya ya Musoma Dk.Khalfan Haule amewapongeza walipa kodi kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Amesema ulipaji wa kodi unaisaidia serikali kuwahudumia wananchi kwenye elimu, afya,maji,miundombonu na huduma mbalimbali.
Kwa upande wao wafanyabiashara ambao wamekabidhiwa vyeti vya pomgezi wameishukuru serikali kwa kutambua mchango wao na kuwatia moyo wa kuendelea kulipa kodi.
Post a Comment