HEADER AD

HEADER AD

TRA MARA YATOA MSAADA VITUO VINAVYOLEA WATU WENYE UHITAJI MAALUM


Na Shomari Binda, Musoma

VITUO 4 vinavolea watu wenye uhitaji maalum manispaa ya Musoma vimepokea msaada kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA ) mkoa wa Mara.

Msaada huo umetolewa ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya shukrani kwa mlipa kodi ambapo mahitaji mbalimbali kama mchele, sukari, mafuta, sabuni, maharage juice pamoja na mahitaji mengine imetolewa.

Akikabidhi misaada hiyo kwenye vituo 2 vya mji wa huruma vinavyo tunza  na kulea watu masikini na wale wenye changamoto ya afya ya akili, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mara Nassoro Ndemo amesema katika kuwashukuru walipa kodi wameamua kurudisha kwenye makundi hayo.

Kaimu meneja wa TRA mkoa wa Mara Nassoro Ndemo akikabidhi msaada kituo cha ST.Justin Center kilichopo manispaa ya Musoma

Amesema kwenye jamii yapo makundi yenye uhitaji ambayo yana stahili kufikiwa na kusaidiwa ili nao waonekane wenye furaha.

Ndemo amesema kodi zinazolipwa na wafanyabiashara ndizo zinazowezesha kufanya shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa, huduma za afya pamoja na mahitaji mengine kwenye jamii.

Amesema wafanyabiashara wanapaswa kutunza kumbukumbu za biashara zao na kulipa kodi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutoa risiti na wananchi kudai risiti.


" Leo ni uzinduzi wa wiki ya kutoa shukrani kwa mlipa kodi na TRA mkoa wa Mara tumeyafikia makundi yenye uhitaji na kuweza kutoa kile ambacho tumejaliwa.

" Kwa wiki hii tutafanya matukio mbalimbali na licha ya misaada hii tutatoa vyeti na kuwatambua walipa kodi ambao wamefanya vizuri  kwa mwaka wa fedha 2022 na 2023", amesema Ndemo.

Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada uliotolewa na mamlaka hiyo, kiongozi wa vituo vya mji wa huruma Padri Godfrey Pendo ameshukuru kwa msaada huo na kudai umekuja kwa muda muafaka.


Amesema kwa miaka 15 amekuwa akitegemea misaada kutoka kwa watu mbalimbali baada ya shughuli za kiuchumi alizokuwa akizitegemea kushindwa kuendelea na kutegemea misaada.

Vituo vingine vilivyofikiwa na TRA mkoa wa Mara ni pamoja  na Musoma Children Home kinacholea watoto kuanzia mwaka 0 hadi miaka 2 na kituo cha ST.Justin Center kinacholea wenye ulemavu na afya ya akili ambao wote wametoa shukrani kwa TRA kwa msaada walioutoa.



No comments