ROPE TANZANIA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI MAPINGA
Na Andrew Chale, Bagamoyo
SHIRIKA la ROPE Tanzania lenye makao yake makuu Bagamoyo Mkoani Pwani, limetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Mapinga.
Shirika hilo linalojihusisha na masuala ya kijamii ikiwemo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita mila potofu katika jamii, ndoa na mimba za utotoni, ndoa za kulazimishwa na ukosefu wa usawa wa kijinsia.
ROPE Tanzania imetoa vifaa hivyo vya shule vya kujifunzia vikiwemo vitabu, madaftari, kalamu, penseli, rula, vichongeo, vifutio na vingine vingi katika shule hiyo ya msingi Mapinga ambapo pia wamepata wasaha wa kuzungumza na Walimu pamoja na Wanafunzi kuhusiana na Elimu na kuwahimiza waongeze juhudi ili kuweza kufika malengo yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Mshauri wa maswala ya Elimu wa ROPE Tanzania. Bi. Theresia Urassa amesema kuwa, lengo la kugawa vifaa hivyo ni baada ya kuona changamoto inayowakabili baadhi ya wanafunzi maeneo mengi hapa nchini hivyo ikiwemo kukosa vifaa muhimu vya shule ambapo waliamua kuanza na shule hiyo ya Msingi Mapinga iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani.
ROPE Tanzania tumekuwa wa faraja kuhakikisha tunaifikia jamii ikiwemo wanafunzi angalau kwa uchache katika kusaidia pale tunapoweza.
Hakika wanafunzi wamefurailifurahi sana kwa kupatiwa vifaa vya shule kwasababu walikuwa wakipitia changamoto katika masomo yao kwa uwepo wa vifaa vichache vya kujifunzia ila kwa kupata vifaa hivi kutawasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.” Amesema Mshauri wa maswala ya Elimu wa ROPE Tanzania Bi. Theresia Urassa.
Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walishukuru msaada huo kwani unaongeza hali ya wanafunzi hao katika kujifunza na kupata maarifa Zaidi kwenye masomo yao huku wanafunzi nao wakishukuru kwa pamoja ujio wa shirika hilo la ROPE Tanzania katika kusaidia vifaa hivyo muhimu.
Post a Comment