HEADER AD

HEADER AD

MAKONDA AWAPIGIA SIMU MAWAZIRI WANNE MKUTANONI, AWAAGIZA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

 


Na Alodia Babara, Bukoba

KATIBU wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Paul Makonda ametoa maagizo mbalimbali kwa Mawaziri wa wizara nne hapa nchini ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuwapigia simu mawaziri hao na kutoa majibu ya changamoto kutatua changamoto hizo.

Mawaziri waliopigiwa simu ni pamoja na waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, Waziri wa mambo ya ndani Hamad Massaun, Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa na Waziri wa ujenzi,  Innocent Bashungwa.

Makonda ametoa maagizo hayo Novemba 9,2023 wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara akiongea  na  wananchi mkoani Kagera uliofanyika uwanja wa mashujaa Mayunga.

Moja ya changamoyo zilizotajwa ni pamoja na ujenzi wa soko kuu, kingo za mto Kanoni, ujenzi wa stend kuu, uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Bukoba, tatizo la vitambulisho vya Taifa (NIDA) maeneo ya mipakani na ujenzi wa barabara za rami.

Waziri ofisi ya Makamu wa Rais serikali za mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akijibu kuhusu changamoto za ujenzi wa soko kuu, stend kuu na kingo za mto Kanoni amesema kuwa maagizo ya katibu itikadi na uenezi CCM taifa Makonda ameyapokea na akufanyia utekelezaji haraka mwezi Desemba 2023 atafika mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua maeneo itakapotekelezwa miradi hiyo.

Akijibu changamoto ya NIDA kwa upande wa wananchi waishio mipakani Waziri wa mambo ya ndani Hamad Massaun amesema kuwa,  swala la NIDA katika maeneo hayo Wizara inalifanyia kazi ili kuharakisha zoezi na wale wenye haki ya kupata kadi za nida waweze kuzipata. 

Amesema wameanza mkakati wa kutembelea mikoa iliyopo maeneo ya mpakani  kwa kuanza na mkoa wa Mara baadaye watakwenda Kagera.

Makonda amewataka matrafiki wote nchini kutowaonea waendesha pikipiki maalufu kama bodaboda badala yake watumie sheria wanapowakamata na kuwakuta na makosa.

No comments