HEADER AD

HEADER AD

RC ATAKA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA KLINIKI YA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI


>>Atumia masaa 7 kuwasikiliza wananchi 

Na Shomari Binda, Musoma

MKUU wa mkoa  wa Mara Said Muhamed Mtanda amezindua kliniki ya kusikiliza migogoro ya ardhi na kuagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wake.

Kauli hiyo ameitoa kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo ulipofanyika uzinduzi huo ambapo ametumia saa 7 kuwasikiliza wananchi wenye kero na migogoro mbalimbali ya ardhi.

Amesema mkoa wa Mara hauna eneo la kutosha la ardhi kwani ni asilimia 27.8 wanalolitumia wananchi na mifugo na hivyo kusisitiza matumizi bora ya ardhi.

       Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda akizungumza na wananchi kwenye uzinduzi wa kliniki ya utatuzi wa migogoro ya ardhi mjini Musoma

Amesema lengo la kuanzisha kliniki ya migogoro ya ardhi iliyozinduliwa ni kuwasikiliza wananchi na kupata utatuzi wake.

Mtanda amesema mara baada ya kliniki hiyo kupita anahitaji kupata taarifa ili kujua migogoro iliyopokelewa na kupatiwa ufumbuzi.

Watumishi wa ardhi wamewafuata wananchi kwenye maeneo yao kusikiliza kero zao.

" Leo tumefanya uzinduzi wa kliniki hii na lengo lake ni kusikiliza kero na malalamiko ya migogoro ardhi ambayo ipo kwa wananchi.

" naomba wananchi wasikilizwe mkoa mzima  na kisha nipate taarifa za utatuzi wa migogoro iliyosikilizwa na baadae tukomeshe migogoro yote",amesema Mtanda.

Amesema wananchi wametangaziwa kliniki hiyo lakini walojitokeza ni wachache na matokeo yake wakiona ziara ya viongozi wa kitaifa husimama na kutoa malalamiko.

Amesema wananchi wanapaswa kuitumia fursa hiyo kupeleka kero zao na kuahidi kuzimaliza kwa namna zilivyopokelewa.

        Mmoja wa wananchi akikabidhiwa hati

Kamishina Msaidizi wa ardhi mkoa wa Mara Joseph Batinamani amesema imeandaliwa 'data' kwaajili ya kusikiliza na kupokea migogoro yote itakayotolewa ili kuepuka migogoro kutojirudia 

Amesema wakiwa manispaa ya Musoma watasikiliza kero kwa siku 5 na baadae kuhamia katika maeneo mengine ya mkoa wa Mara  mkuu wa mkoa 

Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wameishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia ofisi ya Kamishina Msaidizi wa ardhi kwa namna alivyoamua kumaliza migogoro ya ardhi.

No comments