HEADER AD

HEADER AD

RC MARA : HALMASHAURI TARIME ITENGE FEDHA ZA CSR KUWEZESHA WACHIMBAJI WANAOZUNGUKA MGODI


Na Dinna Maningo, Tarime

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda amesema kuwa wachimbaji wadogo wa madini wanaozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Nyamongo, Wilaya ya Tarime unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick wanatakiwa kunufaika na fedha za uwajibikaji wa makampuni kwa jamii ( CSR).

Amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime inapaswa kutenga fedha za CSR kuwezesha wachimbaji wadogo ili zisaidie kutatua changamoto zao.

Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda ( wa pili kushoto) akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kitare Daud Wangwe.

Ameyasema hayo Novemba,23, 2023 wakati akizindua mpango wa mafunzo ya kukuza biashara ya siku mbili ya uendeshaji biashara kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara yaliyoandaliwa na mgodi wa Barrick North Mara ambapo wawezeshaji wa mafunzo ni kutoka Kampuni ya Impacten Afrika limited na kutoka Taasisi mbalimbali.

Amesema kuwa baada ya kuvitembelea vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wataweka utaratibu wa fedha za uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR) kusaidia wachimbaji wadogowadogo wa madini.

        Wafanyabiashara mkoani Mara wakiwa Kwenye mafunzo ya kujengewa uelewa wa kukuza biashara

"Nitafanya ziara vijiji vyote 11 vinavyozunguka mgodi, tunataka tuone fedha za CSR zinasaidia maisha ya wachimbaji wadogowadogo kwenye vijiji ambavyo vinazunguka mgodi ili na wenyewe wawe na uhakika wa kuchimba, ili Vijana watoke mtaani wasiende kuvamia mgodi na kujikuta wakipigwa risasi.

"Kwa sababu wanaovamia wanaenda na mapanga na hivyo kujeruhiana. sasa nataka wachimbaji wadogowadogo wanaozunguka mgodi tuwe na utaratibu CSR kupitia Halmashauri itenge fedha kuwezesha wachimbaji nao wana mahitaji yao, mara maduara yamejaa maji, kwahiyo vipo vitu ambavyo nao wanahitaji wanufaike" amesema Mtanda.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kusema " Kama kuna mitambo ya kuosha Dhahabu tuweke makubaliano waoshe, kama mgodi mnaweza kununua Dhahabu zao mnunue. Kwahiyo baada ya ziara yangu tutakaa tutathmini tuone CSR namna gani fedha hizo ziweze kusaidia ili kukuza ajira kwenye migodi midogomidogo.

 Mkuu wa mkoa wa Mara ( wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi w mgodi wa Barrick North Mara pamoja na Wafanyabiashara wa mkoa wa Mara 

" Lakini pia hata mgodi wawezeshe wafugaji, Vijana waunde kikundi cha ufugaji wapewe ng'ombe wa kisasa na mgodi ukaelekezwa kununua maziwa wawe na uhakika wa soko ili wasihangaike na maisha " amesema Mtanda.

RC Mtanda amesema kuwa kumekuwa na mvutano kuhusu mgawanyo wa fedha za CSR kwamba baadhi ya watu wanasema Vijiji vinavyozunguka mgodi vinapaswa kupata asilimia 100 za CSR na siyo asilimia 40.

             Mfanyabiashara akichangia mada Kwenye mafunzo ya wafanyabiashara

"Asilimia 40 ya fedha za CSR zitaenda kwenye Vijiji vinavyozunguka mgodi na asilimia 60 zinatakiwa kunufaisha vijiji vingine vya Halmashauri ya wilaya. Kumekuwa na mvutano wengine wanataka asilimia 100 zote zibakie pale kwenye vijiji 11.

" Hii Sera siyo ya mkuu wa mkoa siyo sera ya halmashauri ni kanuni zilizotungwa na Serikali kupitia Wizara. Serikali yetu imeendelea kunufaika na uwepo wa mgodi wa North Mara "amesema 

Ameongeza " Unasikia watu wanasema mgodi haunufaishi watanzania utasikia wanaoishi na mgodi hawanufaiki mpaka nikawauliza je wananchi wa Kilimanjaro na wao waseme mlima Kilimanjaro upo Kwetu kwahiyo pesa zote za mlima Kilimanjaro zibakie Kilimanjaro?.


"Mimi natoka Lindi hivi karibuni mmesikia Rais wetu anataka kusaini mikataba ili kusambaza gesi nchini kwahiyo na sisi watu wa Lindi tuseme gesi na pesa zote za gesi ibakie mkoa wa Lindi?.

"Asilimia 36 ya mkoa wa Mara ni hifadhi ya Taifa ya Serengeti na inaingiza pesa nyingi kwenye mfuko wa taifa je na wao waseme wananchi wote waajiriwe hifadhini au huduma zote zinazofanyika ndani ya Hifadhi zichukuliwe na Vijana wa Serengeti?" amehoji.

Ameupongeza mgodi wa North Mara kwa kutoa pesa za CSR Bilioni 7.3 fedha ambazo ni nyingi ikilinganishwa na mapato yanayokusanywa na halmashauri ya mji Tarime takribani Tsh. Bilioni nne.

Kaimu Meneja wa Mgodi wa Barrick North Mara, Hermence Christopher  Lulah amesema Kampuni ya Barrick ni Kampuni yenye ubora na Serikali ya Tanzania na kwamba mgodi wa North Mara ni wadau wakubwa katika uwekezaji katika ukanda wa Tarime.

     Kaimu Meneja wa mgodi wa Barrick North Mara Hermence Christopher Lulah

" Sisi kama kampuni iliyosajiliwa Tanzania kuna sheria na taratibu zinazotutaka sisi kama wawekezaji wakubwa kuweza kuwajengea uwezo watanzania katika shughuli mbalimbali kama sehemu ya kuhakikisha watanzania wanashiriki vizuri kwenye mnyororo wa thamani wa wachimbaji wa madini hasa wazawa wanaotokea katika mgodi" amesema Hermence.

                Heri Emmanuel Mkufunzi akiendesha mafunzo ya biashara

          Charles Mkufunzi akiendesha mafunzo ya Biashara

Maafisa wa Kampuni ya Impacten inayoendesha mafunzo ya wafanyabiashara, wa kwanza kulia ni  Meneja Mradi wa mafunzo ya kukuzia biashara Joseph Alex



      Wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Rin. co.ltd ya Nyamongo, (katikati) ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Isaack Range.

Picha za wajumbe wakiwa Kwenye mafunzo

No comments