HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI YATOA MAGARI 31 NA VIFAA TIBA MKOA WA MARA KWA SHUGHULI ZA AFYA

Na Shomari Binda, Musoma

MKOA wa Mara unatarajia kupokea jumla  ya magari 31 na vifaa tiba kwaajili ya kuhudumia wagonjwa na kufanya ufatiliaji  wa shughuli za afya.

Magari hayo ni pamoja na magari 20 kwaajili ya kubeba wagonjwa (Ambulance) na magari 11 kwaajili ya shughuli za usimamizi na ufatiliaji.

              Baadhi ya gari 

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda amesema mnamo Oktoba 28 mwaka huu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alitoa vifaa vya Tsh. 3,718,394,680.48 ambapo mkoa wa Mara umepata vifaa vyenye thamani ya Tsh. 232,405,917.53 ambavyo vimepelekwa kituo cha afya Kisorya.

       Mkuu wa Mara Said Mtanda akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu upokeaji wa magari na vifaa vya afya

Amesema vifaa vilivyopokelewa kwa mkoa wa Mara kwenda vituo vya afya pamoja na Hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni pamoja na vipimo vya mionzi aina ya CT Scan,X Ray,Ultra Sound,Machine za kusafishia damu( Dialysis Machine).

Vifaa vya kutolea huduma ya dharura( Emergency Service) zikiwemo mashine za maabara na vifaa vya huduma kwa wagonjwa mahututi( ICU Services) na mtambo wa kufua hewa tiba ya Oksijeni.

                  Vifaa

Mkuu huyo wa mkoa amesema jumla ya vituo vya afya 25 vimepatiwa vifaa vya kuwezesha kutoa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine pamoja na huduma ya kuongeza damu.

" Kwa magari haya kila halmashauri itapokea magari 2 kwaajili ya huduma za wagonjwa na gari moja kwaajili ya ufatiliaji wa shughuli za afya.

" Nitoe wito kwa wataalam wa afya kuvitunza vifaa hivi vilivyotolewa na serikali ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa",amesema Mtanda.

                      Vifaa

Mkuu huyo wa mkoa amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusaidia kuboresha huduma za afya hadi ngazi ya msingi inayowezesha wananchi kuwa na afya njema.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Zabron Masatu, amesema kupatikana kwa vifaa tiba hivyo pamoja na magari kutasaidia kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo.

No comments