Home
/
HABARI KITAIFA
/
WADAU WAIPONGEZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI UTOAJI ELIMU UBOREJASHI DAFTRI LA WAPIGA KURA
WADAU WAIPONGEZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI UTOAJI ELIMU UBOREJASHI DAFTRI LA WAPIGA KURA
Na Dinna Maningo Rorya
WADAU wa uchaguzi wameipongeza Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania kwa kuvishirikisha Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, Wazee wa Mila, Makundi Maalum na Waandishi wa habari katika utoaji elimu ya uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Wadau wa uchaguzi wametoa pongezi hizi Novemba, 20, 2023 katika ukumbi wa Mapsap Wilayani Rorya mkoani Mara,wakati Tume ya Taifa ya uchaguzi ilipokutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kwa lengo la uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Idd Mtani amesema kuwa elimu waliyoipata itawajenga na kwamba nao wataenda kuelimisha wengine ili wajitokeza kujiandikisha na kurekebisha taarifa zao.
Helena Paul mwenye ulemavu wa ngozi mkazi wa mtaa wa maziwa kata ya Nyakati Manispaa ya Musoma ulemavu wa ngozi ameipongeza Tume ya uchaguzi kuwashirikisha watu wenye ulemavu.
"Watu wenye ulemavu tumeshirikishwa, tumeshiriki watu sita na vyama vya walemavu vipo sita na tumepewa nafasi ya kutoa maoni yetu, kila chama kimetoa maoni yao na yamesikilizwa na maswali yaliyoulizwa yamepata majibu.
Baadhi ya Waandishi wa habari mkoani Mara wameipongeza Tume kwa kuwashirikisha Waandishi wa habari katika mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi na kusema kuwa watasaidia kufikisha elimu hiyo ya uboreshaji wa majaribio kwa jamii kupitia vyombo vya habari wanavyoripotia.
Karol Jacob Mwandishi wa habari wa Chombo cha habari cha Clouds TV amesema Vyombo vya Habari vikishirikishwa vyema ni mabalozi wazuri wa kufikisha taarifa kwa jamii na kusambaa kwa haraka .
" Tunaipongeza Tume kwa kushirikisha waandishi wa habari katika mkutano wa kujadili zoezi la uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura, kwani kupitia vyombo vya habari taarifa zinafika kwa haraka na kwa watu wengi.
" Kuwatumia waandishi wa habari itaisaidia Tume zoezi la uandikishaji wa watu kufanikiwa kwakuwa watu watakuwa wamepata taarifa kupitia vyombo vya habari, ambapo bila waandishi wa habari huwenda Tume isingeweza kuwafikia wananchi wengi katika utoaji elimu ya zoezi la majaribio.
Karoli ametoa wito kwa Taasisi zingine za serikali na binafsi kuvitumia vyombo vya habari katika utoaji elimu kwa jamii ili wananchi waliopo vijijini nao wapate elimu kupitia vyombo vya habari ikizingatiwa kwamba wananchi huviamini vyombo vya habari na ni rahisi kumfikia mwananchi katika upashaji habari kupitia magazeti, Redio , mitandao ya kijamii na runinga
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima pamoja na maafisa wengine wa Tume waliwasili Wilayani humo na kuwaeleza wadau kwamba, lengo la kuwakutanisha wadau wa uchaguzi ni kuwapa fursa wadau kuchangia hoja, kuuliza maswali juu ya uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura zoezi litakalofanyika katika vituo sita kata ya Ikoma kuanzia Tarehe 24 hadi 30, Novemba, 2023.
Ramadhani amesema kuwa wamefanya majaribio katika Kata ya Ikoma kwa ajili ya uboreshaji wa majaribio kwa kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo wa uboreshaji wa Daftari ili kuweza kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza na kuzipatia ufumbuzi mapema kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi la uboreshaji nchi nzima.
Mkurugenzi huyo wa uchaguzi wa Tume ya Taifa amewaomba wananchi wa Ikoma kujitokeza katika uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura zoezi litakalofanyika katika vituo sita katika Kata hiyo.
Post a Comment