TMDA YANG'ARA MASHINDANO YA SHIMMUTA, YAICHAPA LGTI MABAO 4 KWA 2
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU ya soka ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) maalufu kama TMDA FC imeicharaza timu ya
Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo ya LGTI FC kwa jumla ya mabao 4 dhidi ya 2 katika mashindano ya SHIMMUTA yanayoendelea Jijini Dodoma.
Mchezo huo umechezwa leo saa 2:00 asubuhi katika uwanja wa Humanity-1 uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa TMDA Bw. Brian Kyando ameeleza kuwa timu yake ilijiandaa vyema kupata matokeo katika mchezo huo.
"Tunamshukuru Mungu kwa kupata matokeo mechi ya leo.
Tulijipanga kushambulia kuanzia dakika ya kwanza ili tuweze kupata magoli mengi lakini wapinzani wetu nao walijitahidi kutuzuia tukaishia magoli hayo manne. Mchezo huo umeshapita na sasa tunaangalia michezo iliyo mbele yetu ili nayo tufanye vizuri.
Mashindano ya SHIMMUTA yameanza kuanzia tarehe 12 Novemba, 2023 na yanatarajiwa kuendelea hadi tarehe 25 Novemba, 2023.
Post a Comment