HEADER AD

HEADER AD

KAMPUNI YA KYEM YATOA VIFAA VYA UJENZI CCM KATA YA TANGINI


Na Gustafu Haule, Pwani

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tangini iliyopo Kibaha Mjini imepokea msaada wa vifaa vya ujenzi  kutoka kampuni ya uuzaji wa chuma chakavu na usambazaji wa vifaa vya ujenzi Kyem General Supplies vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 3.5.

Kyem ,imetoa vifaa hivyo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya CCM ya Kata hiyo katika  hatua ya kukamilisha msingi ambapo vifaa walivyotoa ni nondo 40,kokoto,mchanga ,mbao na misumari.

Msaada huo umekabidhiwa leo na  mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Kyem General Supplies Martha Jackson kwa Katibu wa CCM Kata ya Tangini Sophia Mtase hafla ambayo imefanyika katika eneo la ujenzi wa ofisi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Martha amesema kuwa kampuni yake ilipata maombi ya kusaidia ujenzi huo kupitia mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tangini Shauri Yombayomba.

Martha,amesema baada ya kupokea ombi hilo kampuni ilikaa na kujadili jambo hilo na hivyo kufikia maamuzi ya kusaidia kulingana na maombi yaliyoainiashwa katika barua yao.

"Leo kampuni yetu ya Kyem imekuja hapa kukamilika maombi ya CCM Kata ya Tangini kwa ajili ya kujenga ofisi yao na tumeleta vifaa vya ujenzi ikiwemo Nondo,Mchanga,Kokoto,Mbao na misumari," amesema Martha

Aidha,Martha amesema kampuni ya Kyem kutoa msaada huo sio mara ya kwanza kwani mara nyingi wamekuwa wakiigusa jamii hasa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu,Wajane na Wazee.

" Mbali na kutoa msaada huu leo lakini kampuni yetu imekuwa ikisaidia jamii inayotuzunguka kwa mahitaji mbalimbali lakini hatahivyo tumetoa ajira ya vijana 200 waliopo katika Kata yetu na tutaendelea kuajiri kulingana na mahitaji yanavyoongezeka,"amesema Martha.

Katibu wa CCM Kata ya Tangini Sophia Mtase, akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo kwani utafanyakazi kubwa ya kukamilisha ujenzi wa msingi wa ofisi hiyo.

Mtase,amesema kuwa ujenzi wa ofisi hiyo ulianza mapema mwaka huu ambapo wadau mbalimbali walichangia akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka pamoja na Mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani Musa Mansoor.

"Naishukuru kampuni ya Kyem kwa kuungana nasi katika ujenzi wa ofisi yetu ya chama,leo nafuraha kuona wamekuja kutuletea vifaa ambavyo vitakwenda kukamilika hatua ya awali ya msingi,"amesema Mtase.

Mtase ,ameongeza kwasasa bado kuna mahitaji makubwa ya ujenzi huo kwani wanahitaji matofali ,7000 na fedha kwakuwa mpaka kukamilika Kwa ujenzi huo itafikia gharama ya milioni 60.


Ameiomba kampuni hiyo pamoja na wadauwengine  kuendelea kushirikiana katika kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo ili kusudi Chama kipate sehemu ya kufanyiakazi zake kwani kwasasa wanafanyia kazi katika kumbi za starehe

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Tangini Shauri Yombayomba, amesema kuwa kampuni ya Kyem ambayo ipo Mtaani kwake inafanyakazi nzuri ya kushirikiana na jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.

Yombayomba, amesema kuwa awali viongozi  wa CCM Kata ya Tangini walimpa maombi juu ya mahitaji hayo lakini akaona atafute mdau wa kusaidia jambo hilo na hatimaye kuipata kampuni ya Kyem iliyopo Mtaani kwake.

"Nilipata barua kutoka kwa uongozi wa CCM Kata wakiniomba msaada katika ujenzi huo lakini mimi ikabidi nihangaike kutafuta wadau wa kunisaidia na hatimaye nikapata Kyem ambao leo wametimiza ndoto yangu na vifaa vimekuja,"amesema Yombayomba.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Jeremiah Komba,amesema hatua ya Kyem kutoa msaada huo imetoa njia kwa wadau wengine kuendelea kuchangia ujenzi wa ofisi hiyo.

Hatahivyo ,Komba amesema ujenzi wa ofisi hiyo utarahisisha utendaji kazi wa viongozi huku akiwapongeza wanaoendelea kutoa michango ya fedha na vifaa na kuwaomba wengine wajitokeze zaidi.



No comments