MILIONI 767.5 KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATA YA KABITA
Na Samwel Mwanga, Busega
WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu itatumia Tsh. 767,507,222.50 kutekeleza mradi wa maji wa Kabita ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Kata ya Kabita iliyoko wilayani humo.
Hayo yameelezwa Desemba 12 mwaka huu na Meneja wa RUWASA wilaya ya Busega, Mhandisi Daniel Gagala wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huoi wa maji kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo katika wilaya hiyo kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Mwenyekiti CCM mkoa wa Simiyu,Shemsa Mohamed(mwenye miwani)akimsikiliza Meneja wa Ruwasa wilaya ya Busega,Mhandisi Daniel Gagala(mwenye Sweta rangi nyekundu) juu ya Utekelezaji wa mradi wa Maji KabitaAmesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 RUWASA wilayani humo ilipangiwa kiasi hicho cha fedha kupitia Mfuko wa Maji(NWF)kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza.
Amesema kuwa kwa mujibu wa mkataba mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi M/S MHAPA BUILDERSA&ROAD WORKS LTDu.
Mradi huo umeanza kutekelezwa Desemba 12,2022 na ulipaswa kukamilika Novemba 30 mwaka huu lakini kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha mkandarasi huyo ameomba kuongezewa muda wa miezi miwili hadi Januari 30,2024.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Busega,Mhandisi Daniel Gagala akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani)Utekelezaji wa mradi wa Maji wa Kabita wilaya ya BusegaMhandisi Gagala amesema kuwa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 80 ya utekelezaji na Mkandarasi tayari amelipwa kiasi cha Sh 430,679,470/-na mradi huo utakapokamilika utaweza kuwahudumia watu 33,389 waishio katika Kata hiyo yenye vijiji vya Nyakaboja, Kabita, Nyamikoma A,Nyamikoma B na Shimanilwe.
“Mradi huu utakapokamilika utawahudumia wakazi 33,389 wa Kata ya Kabita katika vijiji vyotevya Kata hiyo ambavyo ni Nyakaboja, Kabita, Nyamikoma A, Nyamikoma B na Shimanilwe ambao watapata maji safi na salama ya bomba,”amesema.
Amesema kuwa kazi ambazo zilipangwa kutekelezwa ni pamoja na Ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa M 450 ambao ujenzi wake umefikia asilimia 84,Ujenzi wa chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha lita 1,229,760 ambao umefikia asilimia 52,Uchimbaji wa mtaro kwa ajili ya kulaza bomba kuu na la kusambazia maji mita 2550 na Ununuzi na Ulazaji na uungaji wa bomba Mita 2550.
Muonekano wa Tanki la kuhifadhi Maji katika Mradi wa Maji wa Kijiji Cha Kabita wilaya ya Busega.Pia Mhandisi Gagala amesema kuwa hadi sasa katika kutekeleza mradi huo kazi ambazo bado kufanyika ni pamoja na ununuzi na uwekaji wa pampu,upelekaji wa umeme kwenye chanzo cha maji na ujenzi wa vituo viwili vya kuchotea maji.
Aidha amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo utaongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 7.94 na kufanya jumla ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini katika wilaya hiyo kufikia asilimia 76.96 kutoka asilimia 69.02 ya hivi sasa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Shemsha Mohamed amewata RUWASA kuhakikisha mradi huo unakamilika kulingana na muda ambao wamemuongezea mkandarasi ili wananchi wa maeneo hayo aweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Mwenyekiti CCM mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed(mwenye miwani)akimsikiliza Meneja wa Ruwasa wilaya ya Busega,Mhandisi Daniel Gagala(mwenye Sweta rangi nyekundu) juu ya Utekelezaji wa mradi wa Maji KabitaAmesema kuwa ni vizuri mkandarasi akaongeza kasi ili ifikapo Januari 30,2024 mradi huo uwe umekamilika na dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha anamtua ndoo mama kichwani na ndiyo maana amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta ya maji.
Amesema kuwa katika ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 imeeleza kuwa ifikapo mwaka 2025 kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inapatikana maeneo ya vijijini kwa asilimia 85 na maeneo ya mijini asilimia 95.
“Nitumie fursa hii kumpongeza Rais Dkt. Samia Sulluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za maendeleo hususan katika sekta ya maji na ninyi ni mashahidi mmeona katika mradi huu wa maji wa Kabita ametoa kiasi cha fedha zaidi ya Tsh. Milioni 700 hii inadhihirisha kabisa lengo lake la kumtua mama ndoo kichwani ifikapo mwaka 2025 linatimia,”amesema.
Naye Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt Yahaya Nawanda amesema kuwa atahakikisha mradi huo unakamilika kwa ubora unaotakiwa ili uweze kuwahudumia wananchi sambamba na kuwaomba wananchi kutunza na kuilinda miundo mbinu ya maji itakayojengwa kwenye mradi huo ili iweze kutumika na kwa vizazi vijavyo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu,Shemsa Mohamed (mwenye kitambaa cheusi)kichwani akisaidiwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dkt Yahaya Nawanda(mwenye shati la kijani) kupanda juu ya tenki la maji katika Mradi wa maji wa Kabita wilaya ya Busega
Post a Comment