MNEMBWE ASHINDA UENYEKITI SOKO LA MNARANI KIBAHA
Na Gustafu Haule, Pwani
WAFANYABIASHARA wa Soko la Mnarani lililopo Loliondo Kata ya Tangini katika Halmashauri ya Mji Kibaha wamefanikiwa kupata viongozi wapya watakaoongoza soko hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Viongozi hao wamepatikana kufuatia uchaguzi uliofanyika Desemba mwaka huu sokoni hapo ambapo hata hivyo nafasi ya mwenyekiti imekwenda kwa Mohamed Omari (Mnembwe).
Mnembwe,ambaye alikuwa anatetea nafasi yake ameshinda kwa kishindo baada ya kumbwaga mpinzani wake Anthony Maganga ambaye alijikuta anapata kura 130 dhidi ya Mnembwe aliyepata kura 423.
Mwenyekiti wa Soko la Mnarani lililopo Loliondo katika Halmashauri ya Mji Kibaha Mohamed Omari aliyeshinda katika uchaguzi uliofanyika juzi sokoni hapo.Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi kutoka ofisi ya Mtendaji Kata ya Tangini Idd Hassan, amesema kuwa Mnembwe ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura nyingi zaidi ya mwenzake .
"Nafasi ya mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili akiwemo Levis Anthony Maganga na Mohamed Said Omari (Mnembwe) lakini katika uchaguzi Maganga amepata kura 130 na Mnembwe amepata kura 423 hivyo Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Mnembwe kuwa mwenyekiti wa Soko hili,"anasema Hassan.
Aidha kwa mujibu wa Hassan nafasi nyingine zilizowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Katibu wa Soko iliyochukuliwa na Sheiza Steven aliyepata kura 302 na kumshinda Abdul Kombo(211) pamoja na Emmanuel Mwasha(106) huku nafasi ya Katibu msaidizi imekwenda kwa Leonard Msimbe(548).
Pia nafasi ya mwekahazina ilikuwa na wagombea wawili akiwemo Josephu John na Lazaro Josephu ambapo hatahivyo Josephu John ameibuka kuwa mshindi baada ya kupata kura 434 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 263.
Wafanyabiashara wa Soko la Mnarani wakiwa katika zoezi la kuchagua viongozi wao.Aidha nafasi nyingine zilizowaniwa katika uchaguzi huo ni uongozi wa kitengo cha Mabucha ambapo mwenyekiti ni Saimon Chirwa(29) na katibu ni Tunda Tajiri(25),wakati kitengo cha Ndizi Mbivu ni Venance Mkumbo(26) na katibu ni Lazaro Stephano(17) huku Mjumbe ni Gasper Msimbe.
Kitengo cha Malimbichi walioshinda ni Salim Mdimu aliyechukua nafasi ya uenyekiti (17) wakati Katibu ni Hssan Konda(36) huku kitengo cha Mamalishe mwenyekiti ni Mwanahamis Mohamed (09) na katibu ni Grace Shilla huku Mjumbe ni Abdallah Hamisi(62).
Upande wa Matunda mwenyekiti ni Khatibu Omari(50) na katibu ni Amina Mwinyimvua (45) huku Mjumbe ni Amos Selemani wakati upande wa Fremu viongozi wake ni Paul Mashimba(37) na katibu wake Swedi Mkumba (38).
Wafanyabiashara wa Soko la Mnarani wakiwa katika zoezi la kuchagua viongozi waoKitengo cha nafaka aliyeshinda nafasi ya mwenyekiti ni Ally Mfinanga (46) na Katibu wake ni Juma Soke(47) huku Mjumbe ni Josephu Mushi (47) na upande wa Bodaboda aliyeshinda kuwa mwenyekiti ni Zuberi Bakari(14).
Katika upande wa Kuku mwenyekiti ni Bakari Msuya na kitengo cha Nyanya mwenyekiti ni Greyson Richard(37) na Katibu ni Sheba Kalage(40) huku Mjumbe ni Idd Nassoro (40) wakati upande wa stendi mwenyekiti ni Lazaro Benjamin (106) na Katibu wake ni Yusuf Mmari(123) na Mjumbe ni Zawadi Mbonde(123).
Hatahivyo,upande wa bidhaa mchanganyiko Mwiru Ngombale ameibuka kuwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 120 wakati Thadeo Paskali ameshinda nafasi ya Katibu Kwa kupata kura 57 na kuwabwaga wapinzani wake Eliana Massawe(39) huku Zuberi Mazwazwa akiambulia kura 25.
Mfanyabiashara akipiga kura kuchagua viongozi wa Soko la Mnarani Loliondo Kibaha Mjini.Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi Mnembwe amesema kuwa amefurahi kutangazwa kuwa mshindi lakini ushindi wake umetokana na kazi nzuri iliyofanyika kipindi cha nyuma cha uongozi wake.
Mnembwe amesema kuwa baada ya ushindi wake wafanyabiashara wategemee mazuri zaidi hasa katika kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kujenga paa eneo la Matunda,kufanya marekebisho eneo la bidhaa mchanganyiko na mchele pamoja na maeneo mengine.
Post a Comment