UTPC YATAJA TAKWIMU ZA MADHIRA YALIYOWAKUMBA WAANDISHI WA HABARI WAKITEKELEZA MAJUKUMU YAO
Na Helena Magabe Tarime
TAKWIMU za matukio mbali mbali mabaya dhidi ya Waandishi wa Habari nchini zimetajwa kufikia idadi ya Waandishi wa habari 272 katika kipindi cha miaka 10.
Katika matukio hayo wanaume ni 219 na Wanawake ni 53 na vyombo vya habari 94 vilikumbwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na 24 kufungiwa na faini 14.
Jeshi la Polisi Tarime Rorya limetajwa kuongoza kwa matukio 51,TCRA 21 Wizara mbali mbali 14 Wasiojulikana 10, Wakuu wa Wilaya 9 ,Wakuu wa Mikoa 7,Shabiki wa mpira 5, habari maelezo 4 pamoja na Wakulima na wafugaji 2.
Akiwaslisha taarifa ya hiyo ya umoja wa vilabu vya Waandishi wa Habari hapa nchini (UTPC), Ofisa programu Msaidizi Edmund Kipungu, amesema lengo la kufanya midahalo baina ya waandishi wa habari na jeshi la Polisi ni kuwajengea mahusiano Waandishi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuwaondolea hofu.
Kipungu amesema hali hiyo inawasababishia hofu waandishi wa habari na kushindwa kuandika habari za uchaguzi .
Ameeleza kuwa UTPC inafanya midahalo hiyo Kwa ajili ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari Kwa kutambua kwamba wanasukuma shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii na kupata uelewa juu ya masuala mbalimbali ya Nchi .
Kwa upande wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Tarime/Rorya Mark Njera amesema ushirikiano wa vyombo vya habari Dunia nzima ni wa kusua sua lakini watu wote wanategemeana na kuwataka waandishi wa habari kutokuwa wanyonge katika kutekeleza majukumu yao .
Amesema zipo changamoto chache za utoaji taarifa, kwani zipo zinazotakiwa kutolewa katika vyombo vya habari na ambazo hazitakiwi kutolewa.
Aidha amesema Kila mmoja anapotekeleza majukumu yake azingatie kanuni na sheria na kwamba Jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa chache kutokana utunzaji wa ushahidi nakwamba kutoa taarifa ambayo iko kwenye uchunguzi kunaweza kuathiri uchunguzi.
Katika hatua nyingine amesisitiza Waandishi wa sheria ya habari ibala30 kuwa na sare maalumu wakati wakutekeleza majukumu yao na pale wanapokwenda kufanya habari za uchunguzi watoe taarifa Polisi kwa usalama zaidi
Amesisitiza waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari kupata mafunzo ya ulinzi na Usalama .
Post a Comment