WAANDISHI WA HABARI WAVUTIWA MAONESHO SHUGHULI ZA KITAALUMA
Na Alodia Babara, Dodoma
WAANDISHI wa Habari katika Klabu mbalimbali nchini wameonyesha kufurahia uwepo wa maonyesho ya shughuli za kitaaluma, kijamii na kiuchumi zinazofanywa na klabu hizo ambapo maonyesho hayo yamewapa mbinu za kuongeza kipato katika Klabu na kwa mwandishi mmoja mmoja.
Maonyesho hayo yamefanyika Desemba 09, 2023 katika ukumbi wa ofisi za Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania( UTPC) zilizopo katika jiji la Dodoma.
Wajumbe wa bodi na secretarieti ya UTPC wakiongozwa na rais wa UTPC Deogratias Nsokolo anayesaini kitabu cha wageni katika banda la Kagera Press Club wakikagua vibanda vya maonyesho ya klabu mbalimbali nchini. Picha na Alodia Babara
Maonyesho hayo yaliyoshirikisha klabu zote 28 nchini kila klabu imeweza kuonyesha miradi mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kitaaluma inayoiendesha
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Mbeya MBPC Elizaberth Nyivambe amesema maonyesho hayo ni kiashiria tosha cha kuendana na kauli mbiu ya UTPC from Good to Great kuelea mabadiliko kwenye klabu zetu.
Naye mwenyekiti wa Kagera Press Klabu KPC Mbeki Mbeki amesema miradi iliyoonyeshwa na baadhi ya klabu imeweza kuzichochea klabu ambazo hazina miradi mikubwa kuanzisha miradi kwa masirahi ya klabu zao.
"Viongozi wamejengeana uzoefu na uthubutu wa kujiedesha wenyewe endapo mfadhiri atakuwa amejiondoa hivyo klabu kwa kutumia ubunifu na uzoefu waliopata watakuwa tayari kujiendesha." Amesema Mbeki"
Kwa upande wake rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Deogratias Nsokolo amesema kuwa, bodi ya UTPC katika mkutano wa mwaka huu waliamua yawepo maonyesho na waliwataka viongozi wa klabu kuja kwenye maonyesho na hawakuwambia waonyeshe nini lakini waanfishi wa habari wameweza kuonyesha vitu vizuri vya kujenga klabu.
"Kama ambavyo sote tumeshuhudia hapa tumeona mambo mengi sana ya kitaaluma, kiuchumi na kijamii ambayo yameonyeshwa na waandishi wetu, kwa hiyo tunaweza kuona ni kwa namna gani maonyesho yanaweza kujibu maswali mbalimbali ambayo yanawakabili waandishi wa habari wa Tanzania" amesema Nsokolo
Aidha mkurugenzi wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Kenneth Simbaya ameeleza kwamba, maonyesho yamekuwa na mafanikio makubwa anatarajia mwaka ujao yatakuwa makubwa sana.
"UTPC tuna kauli moja kwamba kila jambo tunalolifanya tukiangalia nyuma tunaona tunaweza kuliboreshaji hili tunalolifanya, kwa hiyo tunawaza tunawezaje kuliendeleza likawa bora zaidi, haya maonyesho mliyoyaona leo mwaka ujao hayatakuwa kama yalivyokuwa leo yatakuwa bora zaidi" amesema Simbaya
Vilevile ameeleza kuwa, katika kauli mbiu ya UTPC ya from good to great jambo la msingi ni kuchukua mrejesho namna ya kuboresha, wamepata mrejesho na wanaendelea kuikusanya na wamefarijika kwa sababu wameona ubunifu uliopo kwenye club, kama secretarieti wanajipanga kupita katika club moja moja kuibua mijadara ili club zitumie fulsa zilizopo katika maeneo yao kujenga club imara.
Post a Comment