HEADER AD

HEADER AD

WAPEWA ELIMU UMUHIMU WA KUWA NA VITAMBULISHO VYA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

 Na Dinna Maningo, Musoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Madini na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa madini Tanzania (FEMATA) wametoa elimu ya umuhimu wa wachimbaji wadogo wa madini, wachenjuaji na wafanyabiashara ya madini kuwa na vitambulisho.

Akizungumza kwenye semina ya wachimbaji wadogo wa madini mkoani Mara iliyofanyika November, 7, 2023 katika ukumbi wa uwekezaji ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara, Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Mara Hamad Kallaye amesema wamepokea kamati ya vitambulisho iliyoundwa na FEMATA kwa kushirikiana na Wizara ya Madini.

      Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Mara Hamad Kallaye

Amesema lengo na madhumuni ni kuhakikisha takwimu za wachimbaji wadogo wa madini, wachenjuaji na wafanyabiashara wa madini zinapatikana.

"Kamati hii imekuja na suala zima la vitambulisho, awali hatukuwa na takwimu za wachimbaji wadogowadogo, takwimu ambazo ofisi inakuwa nazo ni kwa mujibu wa sheria ambao ni wamiliki wa lessni za uchimbaji, lessni za uchimbaji, lessni za wafanyabiashara wakubwa na wadogo.

"FEMATA imekuja na utaratibu wa kuhakikisha kila mdau wa mnyororo wa madini anatambulika kwa mujibu wa vitambulisho ambavyo atakuwa navyo kuanzia suala la uchimbaji, uchenjuaji, wafanyabiashara wa Dhahabu" amesema Hamad.

Amesema Wizara ya Madini na FEMATA wamefika Mara kutoka elimu "Sisi kama mkoa wa Mara tumelipokea na wadau wa uchimbaji wa madini wamelipokea vizuri na umuhimu wake ni mkubwa kwa sababu zao katika sekta ya madini.

            Wachimbaji wadogo wa madini wakiwa kwenye semina

Ametoa wito kwa wadau wote wa madini kuchukua fursa hiyo kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho ambavyo vitakuwa na faida kwao ikiwemo utunzaji wa kumbukumbu, taarifa mbalimbali za shughuli za uzalishaji na mikopo kwenye Taasisi za kibenki.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara ya madini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mradi wa vitambulisho, Stephen Masumbuko amesema kuwa kuna haja ya wachimbaji kutambulika na kueleweka, kufahamu idadi yao Kitaifa, Kimkoa na kiwilaya.

     Mwenyekiti wa wafanyabiashara ya madini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mradi wa vitambulisho, Stephen Masumbuko

" Wachimbaji wa madini tuna mchango mkubwa katika michango ya ulipaji kodi na mirabaha ya serikali, kwa maana hiyo serikali inataka kutuondoa kwenye uchimbaji wa kubahatisha, inahitaji kutusapoti itupe ruzuku katika uchimbaji wetu.

" Serikali kupitia Wizara yetu imekuja na mbinu nzuri ya uchimbaji kuchimba kisayansi na siyo uchimbaji wa kubahatisha. FEMATA imepewa heshima na serikali kupitia Wizara ya madini ili kumhakiki mchimbaji " amesema Stephen.

Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wa madini (MAREMA) mkoa wa Mara, David Bitta amesema kuwa katika mkoa huo uchimbaji umepiga hatua na kwamba wachimbaji wamekuwa na mwitikio mkubwa kujiandikisha ili kupatiwa vitambulisho vya wachimbaji wadogo.

     Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wa madini (MAREMA) mkoa wa Mara

"Tayari watu wameanza kijiandikisha kupokea vitambulisho, tumekubaliana tuendelee kutoa elimu mgodini, tumetoa elimu mgodi wa Kibaga, Jumatatu tutakuwa nyamongo, jumanne tutakuwa mgodi wa Buhemba na migodi mingine katika mkoa huo.

" Lengo ni kutoa elimu ya manufaa ya vitambulisho na wamepata elimu na watu wanajiandikisha kupata vitambulisho" amesema David.

Wachimbaji wa madini wameipongeza Serikali na FEMATA kwa utoaji wa vitambulisho kwa wachimbaji vitakavyosaidia wao kutambulika.

Magaka Madaha mchimbaji mdogo wa madini wilayani Bunda amesema " Serikali na FEMATA wameona ni namna gani wachimbaji wadogo waweze kufahamika kwa idadi.

      Magaka Madaha mchimbaji mdogo wa madini wilayani Bunda

"Hata Serikali inapoenda kuwahudumia ijue inawahudumia watu wangapi hata ikileta vifaa ujue ni idadi gani itakayoweza kukidhi mahitaji"amesema.

Mchimbaji wa madini wilayani Butiama Jackline Aringo amesema amefurahi wachimbaji kupewa vitambulisho.

        Mchimbaji wa madini wilayani Butiama Jackline Aringo

 kwani vitasaidia kupunguza migogoro kati ya wachimbaji na wamiliki wa leseni na vitabeba taarifa zote na vitawafanya watambulike kitaifa na kuweza kukopesheka.

















No comments