WAFANYABIASHARA SOKO LA DHAHABU NYAMONGO WATAKA WAJENGEWE SOKO LA KISASA
>>>Wasema Soko la Dhahabu Nyamongo lipo vizuri katika mapato lakini jengo wanalotumia ni dogo ukilinganisha na mavuno serikali inayoyapata
>>>Wachangia tundu moja la choo
>>>Wasema ufinyu wa jengo unawakosesha vijana ajira
Na Dinna Maningo, Nyamongo
WAFANYABIASHARA ya Madini ya Dhahabu Nyamongo Wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wameitaka Serikali kuwajengea soko la kisasa pamoja na choo.
Wamesema haiwezekani waendelee kutumia jengo finyu lisilo na upana linalowapa kero na kubanana hilihali serikali inakusanya fedha nyingi zitokanazo na madini ya dhahabu Nyamongo.
Soko la Dhahabi Nyamongo
Wameyasema hayo hivi karibuni Desemba, 11,2023 wakati walipotembelewa ofisini na Mwenyekiti wa wafanyabiashara ya madini Tanzania, Mwanasheria wa Shirikisho la Vyama vya wachimbaji wa madini Tanzania (FEMATA).
Wengine ni Maafisa kutoka Tume ya Madini Dodoma, Katibu Msaidizi wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Mara pamoja na Maafisa wa madini mkoa wa Mara.
Walifika kutoka elimu ya umuhimu wa wachimbaji wa madini, wachenjuaji na wafanyabiashara ya madini kuwa na vitambulisho vya wachimbaji.
Mwenyekiti Soko la Dhahabu Nyamongo Mwita Samson amesema soko la dhahabu Nyamongo halikidhi mahitaji ya wafanyabiashara ya madini jambo ambalo linalowapa kero pamoja na wateja wao.
"Mchango wa madini ni mkubwa lakini soko la dhahabu Nyamongo haliendani na uhalisia halikidhi mahitaji ya wafanyabiashara ya madini namaanisha Mabloka (Wafanyabiashara wadogo wa madini).
"Kama unavyoona soko letu siyo zuri, vyumba vimebanana na ni vidogovidogo sana, nashukuru uzuri watu wa vitambulisho mmetembelea soko mmejionea wenyewe joto lililo ndani kwakweli halifai hukilinganisha na mavuno ambayo serikali inayapata kupitia soko hilo ni makubwa.
Ameongeza kusema " Tunachangia kodi nyingi serikalini makato ni mengi, soko la Nyamongo lipo vizuri katika mapato kwahiyo tunaomba serikali wakati inahangaika na vitambulisho lakini pia watujengee soko la kisasa lenye kutosha mahitaji makubwa na kulipanua ili vijana wapate ajira.
" Hatuwezi kuongeza vyumba vingine jengo ni dogo, watu wanakujua wafanye biashara lakini hakuna nafasi kwahiyo tunaomba serikali itukumbuke" amesema Mwita.
Amesema soko lina tundu moja la choo hivyo wafanyakazi katika soko hilo maarufu Mabroka wanalazimika kuchangia tundu moja na wateja wanaume kwa wanawake wanaofika kupata huduma.
" Tunaiomba Serikali itujengee choo cha kisasa maana inakusanya kodi na inapata pesa" amesema Mwita.
Mfanyabiashara wa Dhahabu soko hilo la Dhahabu Rama Chibota ameongeza kusema "Muangalie uhalisia jinsi soko lilivyo ukilinganisha kwamba Nyamongo ni mji wa madini, tunao mgodi mkubwa lakini pia sisi wenyewe wafanyabiashara ya dhahabu tuna mchango mkubwa kwenye sekta hii ya madini hata ukiingia kwenye takwimu.
" Soko letu haliendani na uhalisia, uzuri mwenyekiti wetu wa wafanyabiashara naye kasema joto, ameshuhudia mwenyewe kuna joto na hatuna chumba cha kufanyia mikutano.Tunaomba tupate soko la madini la kisasa kulingana na uzalishaji uliopo " amesema Rama.
Mwanasheria wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) ambaye pia ni Meneja Mradi wa vitambulisho nchini, Maina Owino amesema wachimbaji wa madini ni wateja muhimu na wanachangia uchumi wa Taifa hivyo wanastahili kujengewa soko la kisasa.
Mwanasheria wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) ambaye pia ni Meneja Mradi wa vitambulisho nchini, Maina Owino
"Wachimbaji wa madini ni wateja muhimu kabla ya kuondoka Musoma tutakutana na ofisi ya madini na RMO lakini pia suala hili tunalichukua kama sehemu ya kazi yetu kama FEMATA kuja kulishughulikia hawa watu wa Nyamongo wapate soko la kisasa, kiukweli hata mimi mwenyewe linanitia aibu poleni sana" amesema Mwanasheria.
Wakati huohuo, Wafanyabiashara soko la Dhahabu wamelalamika kwa kitendo cha kukamatwa bila sababu za msingi.
Rama Chibota amesema " Wanakuja watu humu wanakamata mabloka, wamekamatwa wengi kwa mambo ya kusingiziwa, vyesi vya kueleweka wanakuja wanakamata watu wanakaa vituoni, gerezani wanaachiwa.
" Hii inashusha Bloka kiuchumi, tunao watu ambao walikamatwa na Task force na wakija hawajitambulishi jambo ambalo ni hatari anaweza kuja jambazi akatuvamia kwa kisingizio kuwa ni Task force maana hawaoneshi utambulisho wao" amesema Rama.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara ya Madini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa mradi wa vitambulisho kwa wachimbaji wadogo nchini, Stephen Masumbuko akizungumzia malalamiko ya wafanyabiashara kukamatwa amesema ;
Mwenyekiti wa wafanyabiashara ya Madini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa mradi wa vitambulisho kwa wachimbaji wadogo nchini, Stephen Masumbuko.
" Tunafanyiwa hivyo ni kwa sababu hatuna kumbukumbu zetu vizuri za ununuaji wa madini yetu, madini yako yanapochukuliwa kwenye mwalo, wanavyokuletea kwenye mlolongo unavyotakiwa.
"Hata Task force wakija ukawaonesha mlolongo wako wa madini, jinsi unavyopeleka sokoni na unavyolipa hapo utakuwa umemzidi na huwenda atakuwa amedanganywa kwasababu wakati Mwingine tunacholeana sisi wafanyabiashara wenyewe" amesema Mwenyekiti.
Post a Comment