HEADER AD

HEADER AD

AFISA HUDUMA ZA UANGALIZI, MAGEREZA WATOA ELIMU YA KIFUNGO CHA NJE

 Na Jovina Massano, Musoma

JAMII yatakiwa kuielewa adhabu mbadala ya kifungo gerezani itolewayo na Idara ya huduma za uangalizi  kwa  mhalifu alietenda kosa la jinai.

Hayo yamesemwa na Afisa huduma za uangalizi mkoa wa Mara Joyce Rwegalula alipokuwa akiongea na DIMA Online katika maonyesho yaliyoandaliwa na Mahakama kuu.

        Afisa huduma za uangalizi mkoa wa Mara Joyce Rwegalula (kushoto) akizungumza.

Maonesho hayo yanaendelea kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo Manispaa ya Musoma katika banda la Wizara ya Mambo ya ndani.

Ameleeza kuwa jamii imekuwa ikitafsiri kifungo cha nje kuwa mtumikia adhabu yupo huru na kuanza kutuhumu vyombo vya sheria kuwa vimefanya upendeleo.

"Adhabu mbadala kimsingi inasadia kupunguza msongamano gerezani kutokana na wahalifu kuongezeka lakini pia hupunguza  mzigo wa jamii kuhudumia idadi kubwa ya wafungwa hivyo serikali ilitafuta ufumbuzi na kubuni Idara ya huduma kwa jamii ambayo ilipitishwa bungeni kama sheria namba 6 ya mwaka 2002 ", amesema Joyce.

Anasema Aladhabu hiyo hutolewa kwa mshtakiwa mwenye makosa madogo yenye kifungo chini ya miaka mitatu kwa kufanya kazi za kijamii kama ilivyoamriwa.

Afisa huyo anasema hii husaidia waliohukumiwa kupata nafasi ya kuhudumia familia zao huku akiwa chini ya uangalizi wa Afisa majaribio na si kwamba ameachiwa huru.

Mwandishi wa habari gazeti la uhuru Ghati Msamba, akizungumza na afisa huduma za uangalizi Joyce Rwegalula

Joyce ameainisha aina ya kazi za kijamii zinazotolewa kuwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira, ukarabati wa majengo ya serikali na nyingine maalum kwa faida ya jamii na hufanya kazi kwa masaa aliyopangiwa na mamlaka husika.

Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa Magereza  Erick Mjarifu, amesema kuwa mbali na idara hiyo kutoa adhabu hiyo kwa mhalifu lakini pia Jeshi la Magereza kupitia kanuni  yake ya sheria kifungu cha 105 cha sheria ya Magereza sura ya 58, kinampa mamlaka mkuu wa gereza kumtoa mfungwa kwenda kufanya kazi za kijamii aliefungwa Mwaka mmoja kurudi chini.

      Mkaguzi msaidizi wa Magereza Erick Mjarifu (kulia) na SGT Msafiri Phinias kushoto wakizungumza

"Hii mkuu wa Gereza huangalia aina ya kosa kwa mhalifu na tabia yake ndipo huamua kumpa kifungo cha nje kwa kufanya shughuli za kijamii",amesema Erick.

Ameongeza kuwa Magereza pia ina utaratibu wa kutoa  wafungwa wenye vifungo virefu kurudi katika jamii chini ya masharti kuendelea kutumikia adhabu zao ambao unatambulika kuwa ni kauli rasmi( Parole) kuwa atazingatia sheria zote na kanuni chini ya utaratibu wa urekebishaji.

SGT Msafiri Phinias wa Kitengo cha sheria na Parole ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara amesema kuwa wafungwa wanufaika ni wenye vifungo virefu ambao tayari wametumikia robo tatu ya vifungo na hawana msamaha wa vifungo vyao.

Amesema hurudi kuitumikia adhabu yao kwa jamii kwa kufuata utaratibu alizopewa na adhabu hii hutolewa mara baada ya mchakato kukamilika na kusainiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Ameongeza kuwa waliofungwa kwa ubakaji, kifungo cha maisha na kifungo cha uvamizi kwa kutumia silaha hawapewi adhabu hiyo bali huendelea kutumikia gerezani kwa mujibu wa utaratibu.

Nae Salama Salehe mkazi wa Nyamazugo wilayani Sengerema mkoani Mwanza akiwa katika shughuli zake mjini Musoma , amesema kuwa yeye alikuwa anafahamu kuwa wengi wanaotoka mapema kabla ya muda wao wa kifungo kuwa ameachiwa huru.

                Salama Salehe

"Kuna kaka wa hapo kijijini kwetu alifungwa hakukaa muda mrefu tulishangaa kumwona amerudi tukajua ameachiwa huru mara akawa anafanya usafi kwenye zahanati ya Kijiji nikajua ameajiriwa na serikali,

" Nilipomuuliza akasema kuwa yupo kifungo cha nje anatumikia adhabu yake  nilishangaa sikujua kuwa kuna kifungo cha aina hiyo", amesema Salama.

Adhabu hii mfungwa hueleweshwa endapo hataridhia ataitumikia akiwa gerezani na kwa wale wanaokuwa wahalifu sugu au usalama wao utakuwa hatarini hawapewi adhabu ya kifungo cha nje.


             

No comments