HEADER AD

HEADER AD

MTO MARA WATAPIKA NA KUHARIBU MAZAO NYAMONGO


Na Dinna Maningo, Tarime

BAADHI ya Wakazi Nyamongo, Kata ya Matongo, Wilayani Tarime mkoa wa Mara, wakiwemo wakulima huwenda wakakumbwa na njaa baada ya mto Mara kufurika na maji kusambaa kwenye mashamba na kuharibu mazao.

Zaidi ya ekari 2,000 za zao la mahindi katika kijiji cha Matongo na ekari zaidi ya 200 za mahindi katika kijiji cha Nyabichune zinadaiwa kusombwa na maji na mazao mengine kuharibika baada ya maji kujaa mashambani.

          Mazao yakiwa yameharibiwa na maji yaliyotoka mto Mara

Vijiji hivyo vimepakana na mto Mara na wakulima wengi mashamba yao yamepakana na mto huo huku maeneo mengine wakiyatumia kama makazi na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

DIMA Online imefika katika baadhi ya mashamba ya wakulima na kushuhudia maji yakiwa yamejaa kwenye mashamba na kuharibu mazao.

            Maji yaliyotoka mto Mara yakiwa yamesambaa mashambani na kusomba mazao

Pia mazao mengine yamesombwa na maji baada ya mto Mara kuacha mkondo wake na maji kutapakaa mashambani.

Mkazi wa Kijiji cha Matongo Mwita Ntora amesema ametumia gharama nyingi za fedha katika kilimo " Nililima ekari 13 za mahindi kwa kukodi trekta lakini mto umesomba mazao.

             Mwita Ntora

"Huwenda nisipate kabisa chakula maana maji ni mengi mazao yaliyosalia  shambani nimeshindwa kuyavuna maji yamejaa na mvua bado inaendelea kunyesha " amesema Ntora.

Mkazi wa kijiji hicho Apson Marwa amesema" Mwandishi hapo unapoona maji ya mejaa kuna karavati ambalo limefunikwa na maji.

Apson Marwa

" Watu wanalazimika kuvuka maji yaliyotoka mto Mara kwa kutembea ndani ya maji au kuogelea hata mifugo imeshindwa kwenda malishoni" amesema Marwa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwinyunyi Daniel Isaroche amesema wananchi wake wote ni wakulima ambao mashamba yao yamepakana na mto Mara.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwinyunyi Daniel Isaroche

"Mto huo umeathiri Kijiji cha Matongo na Nyabichune vinavyopakana na mto Mara ambavyo wakazi wengi mashamba yao yamepakana na mto Mara na wanategemea kilimo hivyo anaiomba serikali kusikia kilio chao kwani huwenda wakakubwa na njaa kwakuwa mazao yamesombwa na maji" amesema Isaroche.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabichune  Mgaya Kisire amesema zaidi ya ekari 200 zimesombwa na maji na kwamba kijiji chake kina uhaba wa ardhi kwakuwa maeneo mengine yanatumika kwa shughuli za wachimbaji wadogo wa madini. 

"Mto umekuwa ukileta shida kuna mwananchi wangu ana mashamba kijiji cha Matongo alivuna viroba 70 vya mahindi akarudi nyumbani ili afate punda wakapakie mahindi alipofika shambani akakuta viroba vyote vimepelekwa na maji" amesema Kisire.

Katibu Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Matongo, Sadock Maningo ambaye ni mkulima katika kijiji cha Matongo, amesema kuwa zaidi ya ekari 2,000 za zao la mahindi zimesombwa na maji.

   Katibu Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Matongo, Sadock Maningo

"Mazao mengi yamesombwa na maji na kijiji hiki hakina maeneo mengine kuwezesha wakulima kulima mazao. Maeneo waliyokuwa wakiishi awali walihamishwa na mgodi wa Barrick kwa shughuli za mgodi.

"Walivyohamishwa wakasogea na kuishi maeneo yaliyokuwa yamesalia na hivyo kujikuta  wakiendelea kulima mazao jirani na mto huo" amesema.Ameiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia suluhu kuona namna ya kuwasaidia wakulima walioathiriwa na mafuriko mto Mara vinginevyo jaamii itakuwa na maisha magumu kwakuwa mazao mengi yamesombwa na maji.

Akizungumza na DIMA Online , Afisa Kilimo Kata ya Matongo Godwin Swai, alisema ekari 348 vir mahindi katika kijiji cha Matongo na Ekari 82 za mahindi katika kijiji cha Nyabichune zimesombwa na maji Mto Mara.

Afisa Kilimo Kata ya Matongo Godwin Swai

Ameiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia suluhu kuona namna ya kuwasaidia wakulima walioathiriwa na mafuriko mto Mara vinginevyo jaamii itakuwa na maisha magumu kwakuwa mazao mengi yamesombwa na maji.

Akizungumza na DIMA Online, Afisa Kilimo Kata ya Matongo Godwin Swai, alisema ekari 348 za mahindi katika kijiji cha Matongo na Ekari 82 za mahindi katika kijiji cha Nyabichune zimesombwa na maji Mto Mara.

Ameiomba Serikali kuona namna ya kuwasaidia wakulima kwani wakulima wengi wamelima mazao na mengine yamepelekwa na maji na bado mvua zinaendelea kunyesha na huwenda mazao yaliyosalia shambani nayo yakazidi kuaathirika.

Mbali na Mto Mara kuathiri mazao Nyamongo umesomba mazao katika kata zinazopakana na mto huo wilayani Tarime na mazao ya wakulima wa wilaya ya Serengeti ambao mashamba yao yamepakana na mto Mara.

       Mahindi yaliyovunwa yakiwa yameharibika baada ya maji kutoka mto mara kusambaa mashambani na kuharibu mazao


No comments