HEADER AD

HEADER AD

BENKI YA TADB YATOA MKOPO WA NG'OMBE WA MAZIWA KWA WANAWAKE 600 KAGERA

 

Na Alodia Babara, Karagwe

WANAWAKE na vijana wapatao 600 mkoani Kagera wamewezeshwa na benki ya maendeleo ya wakulima TADB kupata mkopo wa n'gombe wa maziwa kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.

Wanawake na vijana wamewezeshwa kipitia Mpango wa kopa n'gombe lipa maziwa ambao utawezesha wananchi kujiongezea kipato kwa kuuza maziwa,lishe bora na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maziwa nchini na kwa kuanzia watagawa ng'ombe 300 na baadaye tena n'gombe 300.

Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi n'gombe hao wa kisasa Januari 23, mwaka huu amesema, ilani ya chama cha mapinduzi imeagiza serikali kuanzisha program mbalimbali.

 Kuanzisha vyama vya ushirika vya wafugaji ni moja katika program hizo ambapo ccm iliagiza serikali kuwa na miradi ya namna hiyo ya kopa n'gombe lipa maziwa.

Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi mitamba ya n'gombe wa kisasa kwa vikundi vya wanawake na vijana wilaya ya Karagwe

"Kwa maono, maelekezo na dira ya Rais Samia Suluhu Hassan kwetu katika kuisimamia na kuitekeleza ilani ya chama cha mapinduzi leo tumeanza kuona mwanga tunamshukuru na kumtakia afya njema Rais wetu Dkt. Samia" amesema Ulega.

Amesema maono ya Rais yanaleta tija na mafanikio makubwa miongoni mwa watanzania wachakalikaji wakiwemo wa mkoa wa Kagera.

Ulega amesema n'gombe hao walitolewa na benki ya maendeleo ya wakulima TADB kupitia kwa mwekezaji Josam Ntangeki ambaye amejenga kiwanda cha maziwa cha Kahama Fresh ambapo wakulima hao watakuwa wanalipa maziwa na maziwa hayo kuchakatwa kiwandani.

Aidha ameeleza kwamba waliopokea n'gombe ni wilaya ya Karagwe na kwa wale waliopata n'gombe atakayefanya vizuri akarejesha maziwa kama inavyotakiwa.

Pia atapewa mkopo mwingine wa n'gombe, na akawaagiza benki ya wakulima kutafuta wawekezaji wengine kama Josam ili mpango wa lipa n'gombe kopa maziwa uweze kuwafikia wanakagera wote na wengine wafuge n'gombe wa maziwa na wengine wa nyama.

"Tunataka baada ya siku zijazo sisi tuwe na uwezo wa kuzalisha maziwa si tu kuingiza nchini bali na sisi tuwauzie wengine uwezekano huo tunao kwa sababu tunayo ardhi kubwa, tunao vijana na akina mama wachapa kazi wenye uwezo wa kufanya kazi" amesema Ulega.

Ameongeza kuwa, katika vitalu ambavyo wamewagawia watanzania wakafanye kazi, kwa yeyote ambaye atakuwa na vitalu hiyvo halipi kodi, hafanyi uwekezaji wa maana, anafuga mapori na vichaka na hajulikani ana n'gombe wangapi, hana faida yoyote na kwamba watamtoa na kumuweka muwekezaji mwingine mwenye uwezo wa kufanya vizuri kwani lengo ni kujenga uchumi wa taifa.

Waziri Ulega amesema wanataka Tanzania iuze nyama na maziwa nchi za nje ili wapate fedha za kigeni, anataka aone mkoa wa Kagera wenye rachi za Taifa zisizozidi tano liwe enek la mfano lenye uwezo wa kuzalisha na kuilisha Tanzania, Afrika na dunia nzima.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha Kahama Fresh kilichopo wilaya ya Karagwe Josam Ntangeki amesema kuwa, n'gombe wa kisasa waliotolewa kwa wanawake na vijana tayali wote wana mimba na wamenunua n'gombe hao kutoka Sudan, Uganda na Kenya kwa Tsh. Bilioni 3.2 na kuingizwa nchini bila kodi. 

"N'gombe mmoja ana uwezo wa kukamuliwa lita 40 za maziwa kwa siku, kila aliyekopa n'gombe kwa siku atakuwa analeta kiwandani au kwenye vituo vyetu vya maziwa lita tano za maziwa kwa kipindi cha miaka 2" amesema Josam.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Walles Mashanda amewataka wananchi kutumia fulsa ya uwepo wa kiwanda cha kuzalisha maziwa ili wafuge kisasa na waachane na ufugaji wa kuzululisha mifugo.

Baadhi waliopokea n'gombe hao wameshukuru serikali kwa kuendelea kuwapigania wananchi wake katika swala la kuwainua kiuchumi.

No comments