TAA BARABARANI ZILIVYO NA UMUHIMU JAPO ZINA HUJUMIWA
>>>Wananchi Tarime wasema taa za barabarani zinasaidia kuimalisha usalama wa watumia barabara
>>>TARURA Tarime yasema wizi wa taa za barabarani umekuwa ukifanyika lakini wananchi hawatoi taarifa dhidi ya wanaohujumu
>>>TANROADS Mara, yawashauri wananchi kutoa ushirikiano kuhakikisha taa zinalindwa kwani gharama Taa moja ni kati ya Milioni 4 - 5
>>>Jeshi la Polisi Tarime/Rorya lawanasa watuhumiwa, laendelea kuwasaka wahalifu taa za Barabarani
Na Dinna Maningo, Tarime
UNAPOTEMBEA Barabarani nyakati za usiku unatamani kupata mwanga ili kukuwezesha kuona kule huendako na wakati mwingine waweza kumbwa na matukio ya kiuhalifu kutokana na giza nene kugubikwa barabarani.
Taa za barabarani za jua (Sola) zimekuwa muhimu sana katika kuimalisha mwanga maeneo ya barabarani lakini pia kuupamba mji na kuongeza usalama nyakati za usiku.
Kwa miaka kadhaa barabara kuu katika mji wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, zilitawaliwa na giza nene jambo ambalo lilisababisha kupungua kwa usalama barabarani nyakati za usiku na kuibuka kwa matukio ya uhalifu yakiwemo ya vibaka kupora simu za watu na mali mbalimbali.
Kuwepo kwa changamoto hizo Halmashauri ya Mji wa Tarime ikanunua taa za jua na kuweka katika baadhi ya barabara mjini Tarime.
Taa hizo zikaumulika mji na kuupamba kwa mwangaza mwanana uliowawezesha wafanyabiashara na wajasiliamali kufanya biashara zao nyakati za usiku bila woga.
Kadri siku zilivyozidi kusonga taa hizo zikaharibika na zingine zikaibwa hususani sola na betri na hivyo giza likarejea tena katika mji huo.
Taa ya Barabarani isiyokuwa na betri baada ya kuibwa
Kuwepo kwa giza lililowapa adha wananchi wa mji wa Tarime, Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mara, ikarejesha mwanga kwa kuweka taa mpya za kisasa maeneo mbalimbali ya mji wa Tarime.
Taa hizo zimesaidia kukuza biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwakuwa hujiongezea kipato kwa kufanya biashara zao nyakati za usiku.
Waeleza umuhimu taa za barabarani

Annastazia Maximillian Kirati ni Mjasiliamali anayeuza nguo za mitumba mjini Tarime, anasema tangu taa zilipowekwa barabarani mji wa Tarime nyakati za usiku ung'aa na kupendeza na kwamba zimesaidia wafanyabiashara na wajasiliamali kukuza vipato vyao.
Annastazia Maximillian Kirati Mjasiliamali
"Taa zina faida kwa wajasiliamali na wafanyabiashara, kabla ya taa kuwekwa barabarani ilipofika saa moja usiku watu waliwahi kufunga biashara zao.
" Kwa sasa watu wanafanya biashara zao hadi saa nne usiku, taa zimeupa hadhi wilaya imependeza. Uwepo wa taa za barabarani umezuia vibaka kufanya uhalifu, taa zimekuwa ni ulinzi katika maeneo ya mjini " anasema Annastazia.

Lukas Chacha ni mwendesha pikipiki (Bodaboda) mkazi wa Rebu sokoni, anasema taa za barabarani zinasaidia waendesha pikipiki wanaopaki kwenye vijiwe vilivyopo pembezoni mwa barabara kufanya kazi zao kwa usalama bila woga wa kuvamiwa na vibaka katika maeneo ya maegesho.
Wakala wa mabasi yaendayo mikoani kampuni ya BATCO katika stendi kuu ya Mabasi mjini Tarime, Weboga Warioba anasema uwepo wa taa za barabarani zinasaidia usalama wa abiria wanapopita barabarani kuingia stendi.

Wakala wa mabasi yaendayo mikoani kampuni ya BATCO katika stendi kuu ya Mabasi mjini Tarime, Weboga Warioba
"Taa zikiwepo barabarani zinapunguza wizi kwa abiria wanaosafiri maana wakati wanatembea barabarani kwenda stendi barabara inakuwa na mwanga hivyo kibaka hawezi mvamia tofauti na miaka ya nyuma vibaka walivamia watu barabarani wakati wakiingia stendi kwakuwa hakukuwa na taa barabarani" anasema Weboga.
Anashauri kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyozunguka mitaani nyakati za usiku kwani vitasaidia kupunguza matukio ya wizi wa taa barabarani.
Wizi, uhalibifu wa taa haufai
Licha ya kwamba taa zilizopo barabarani zinasaidia kuimarisha mwanga na usalama kwa watumiaji wa barabara, baadhi ya madereva wa magari wasio na nia njema wamekuwa wakiziharibu kwa kuzigonga na wengine kuziiba kitendo kinachoisababishia serikali hasara pamoja na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Antony Magoti ni mkazi wa mtaa wa Mawasiliano mjini Tarime anasema taa za barabarani ni mkombozi wa wananchi na wafanyabiashara kwakuwa zinahimarisha usalama.

Antony Magoti ni mkazi wa mtaa wa Mawasiliano mjini Tarime
" Umeme wa TANESCO ukikatika taa za barabarani zinasaidia kutupa mwanga lakini chakushangaza watu hawaoni umuhimu wanaiba betri na sola, haitoshi taa zinagongwa na magari na wagongaji hawajulikani.
"Nilishashuhudia pale karibu na kituo cha mafuta gari ikigonga taa na kuwa nyang'anyang'a, taa nyingine iligongwa pale ujenzi, jamani wananchi wenzangu uharibifu na wizi wa taa haufai mwishowe tutarudi kwenye zama za giza " anasema Magoti.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mawasiliano Chacha Balozi anasema kuwekwa taa barabarani zinatoa mwanga ambao unasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mawasiliano Chacha Balozi
Mwenyekiti huyo anasikitika kuona wizi wa taa umezuka kwa baadhi ya mitaa iliyopitiwa na taa za barabarani huku akiwaomba wenyeviti wa mitaa ambao Taa za barabarani zimepita kwenye mitaa yao washirikiane kwa pamoja kudhibiti wizi wa taa.
"Wenyeviti wenzangu nawaomba tufanye doria za mara kwa mara mitaani kwetu. Mwanzoni kulikuwa na taa zalizowekwa na halmashauri baadhi ya taa zikaibwa na zingine zilikufa kwakuwa zilikuwa na uwezo mdogo wa mwanga" anasema.
Mwenyekiti huyo anaongeza kusema
"Serikali kupitia TANROADS ikatuletea taa zenye mwanga wa kutosha zimeweka baadhi ya barabara hapa mjini na mtaa wangu umepitiwa na hizo taa.
" Nashangaa kusikia kwamba kumezuka wizi wa taa za barabarani. Kule Buhemba wezi wameiba taa eneo ambalo lilikuwa hatarishi kwa vibaka kuvamia watu njiani, taa zilivyowekwa uhalifu ulipungua sasa utarejea tena" anasema Chacha.
Mwenyekiti huyo anasema kuna haja ya kufanya upekuzi kwenye gereji na maeneo yanayonunua vyuma chakavu na kwamba baadhi ya taa zinazoibwa huuzwa nchini Kenya.
" Inasemekana kuwa taa zikiibwa zinaenda kuuzwa Kenya, kwenye magereji na wanakonunua vyuma chakavu. Naomba ukaguzi ufanywe kwenye maeneo hayo, haiwezekani turudishwe kwenye giza tunajua madhara ya giza.
Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) , Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mhandisi Charles Marwa anawaomba wananchi kuwafichua wezi wa Taa za barabarani kutokana na kuzuka kwa wizi wa taa.
Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) , Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mhandisi Charles Marwa
"Kuna sehemu mbalimbali kumeibuka wizi wa taa barabarani mtu anakatia chini kabisa anaiba betri na taa na maeneo zilipo taa hizo ni barabarani ni karibu na makazi ya watu wanapita lakini uhalifu unafanyika watu wanakaa kimya wanawaficha wahalifu hawawasemi.
"Niwaombe wananchi wa Tarime pale ambapo mmoja wetu ataonekana anahujumu basi najua eneo hilo wapo wananchi tusiwafiche tutoe taarifa na ikiwezekana tuwakeme tujitahidi kuitunza na kuipenda miundombinu ya barabara inamanufaa kwetu sote " anasema Mhandisi Marwa.
Anaongeza kuwa kutokana na kuzuka wizi wa taa za barabarani tayari mikakati imewekwa kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wahalifu wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
TANROADS yaeleza manufaa
Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mara, Mhandisi Vedastus Maribe anawashauri wananchi kutoa ushirikiano kuhakikisha taa zinalindwa kwasababu zimewekwa kwa manufaa yao na zinasaidia usalama wakati wa usiku.
"Zinasaidia pia wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa muda mrefu nyakati za usiku, unakuta watu wanapanga vitu vyao vinaonekana.
" Zinapoibwa au kuharibiwa zinaleta changamoto kubwa na hasara kwa serikali, kwasababu inatumia fedha nyingi kuweka hizo taa.
" Zinapoibwa au kuharibiwa zinaleta changamoto kubwa na hasara kwa serikali, kwasababu inatumia fedha nyingi kuweka hizo taa.
"Zinapoharibika serikali inabidi iweke taa zingine ambapo zingewekwa sehemu nyingine isiyo na taa tunajikuta tunarudia pale pale." anasema Mhandisi Mariba.
Anawaomba wananchi kuzilinda taa kwakuwa zina manufaa na ni gharama ambapo taa moja inauzwa kati ya sh. Milioni 4 hadi Milioni 5 na kwamba watakaobainika kuharibu au kuiba taa za barabarani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Polisi wakamata watuhumiwa
Kuibuka kwa wizi wa taa za barabarani Jeshi la Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya limefanya msako na kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za wizi na uharibifu wa taa za barabarani.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Mark Njera anasema kwamba, mpaka sasa kuna matukio mawili yameripotiwa ya uharibifu na wizi wa taa za barabarani mjini Tarime.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Mark Njera
Anasema kwamba tukio la kwanza liliripotiwa Desemba, 8, 2023 ambapo betri mbili ziliibwa na Sola ya taa moja iliharibika baada ya nguzo yake kuangushwa.
Kamanda Njera anasema tukio lingine liliripotiwa Desemba, 27, 2023 ambao betri na sola ya taa moja ziliibwa na kwamba matukio yote yalitokea eneo la Darajani lililopo karibu na chuo cha ualimu Tarime.
"Uchunguzi umefanyika na watuhumiwa wawili wamekamata na wamekili kuhusika na matukio hayo.
Juhudi za kuwakamata watuhumiwa wengine watatu waliotajwa kuhusika na matukio haya zinaendelea " anasema Kamanda Njera.

Rejea
>>>Awali akizungumza na Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa Novemba, 8, 2023 waliokuwa wakitembelea miradi mbalimbali ya kimkakati iliyotekelezwa kwa fedha za Serikali, Meneja huyo wa TANROAD mkoa wa Mara, alisema wametenga Tsh. Bilioni 1.6 kwa lengo la kuweka taa za barabarani 308 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mariba anasema katika mkoa wa Mara tayari taa 900 zimekwisha wekwa ambazo zimechochea uchumi wa wafanyabiashara na wajasiliamali kwa kufanya biashara mpaka nyakati za usiku.
Mariba anasema katika mkoa wa Mara tayari taa 900 zimekwisha wekwa ambazo zimechochea uchumi wa wafanyabiashara na wajasiliamali kwa kufanya biashara mpaka nyakati za usiku.
Post a Comment