HEADER AD

HEADER AD

KIKUNDI CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE MARA, MAHAKAMA WATEMBELEA WAFUNGWA GEREZANI

Na Jovina Massano, Musoma 

KATIKA kusherekea wiki ya sheria, Watendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Kikundi cha Waandishi wa Habari Wanawake mkoa wa Mara, (Visionary Women Journalists) na wadau mbalimbali wa sheria wametembelea Gereza la wilaya ya Musoma na kutoa msaada.

Wadau hao wa sheria wametembelea gereza hilo Januari, 29,2024 ambapo Naibu Msajili Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Eugnea Rujwahuka akizungumza kwa niaba ya Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Salome Mushasha, amesema kuwa mahakama haijajikita tu kutoa elimu bali pia kufanya matendo mema kwa wahitaji.

Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Salome Mushasha (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Gereza la wilaya ya Musoma SSP Jackson Murya

"Kwa kuwa sisi pia ni sehemu ya jamii tumewiwa na kuona tushirikiane na wadau mbalimbali wa kisheria, wa mawasiliano ambao ni Tigo, TTCL sambamba na waandishi wa habari kwa kuwaletea ndugu zetu mahitaji hapa gerezani.

" Mahakama haikujikita kwenye utoaji elimu pekee bali imeweza kufanya tendo jema kwa wahitaji kwa kutoa msaada wa Luninga sambamba na king'amuzi chake likiwemo bando, kandambili, miswaki, taulo za kike, mashine za kunyolea, sukari, sabuni, mafuta ya kupaka na ya kupikia" amesema Rujwahuka.

Mlezi wa Kikundi cha Wanawake wenye maono mkoa wa Mara (Visionary Women Journalists) ambaye pia ni Mweka Hazina Shirika la Jicho la Tanzania, Joyce Sokombi amewashauri wananchi kujenga utamaduni wa kuwakumbuka wahitaji ili kuwaondolea upweke, wawapatie faraja ili wasihisi wametengwa na jamii

      Joyce Sokombi akiongea na waandishi wa habari

"Niiombe jamii tuwe na utamaduni wa kuwatembelea wenzetu na kuwafariji kama Mahakama ilivyofanya kwa kutushirikisha wadau mbalimbali.

"Waliomo gerezani si wote wakosaji na hata wakosaji wakitoka tunaimani watakuwa raia wema kwa jamii hatutaishia hapa Magereza tutafika pia kituo cha watoto nao tuwashike mkono kwa tulichobarikiwa,"amesema Sokombi.

Nae Mkuu wa Gereza Wilaya ya MusomaSSP Jackson Murya amewashukuru wadau wote waliowiwa kufika kuwafariji.

 Mkuu wa Gereza la Musoma SSP Jackson Murya (kulia) akizungumza, kushoto ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Salome Mushasha

"Nashukuru kwa kuja kuwatia moyo ndugu zetu waliomo gerezani kwani watu hawa wanahitaji faraja, matunzo na kusaidiwa kwa namna moja au nyingine tendo hili nao wanajiona ni sehemu ya jamii, amesema Murya.

Mtunza hazina wa kikundi cha waandishi wa habari wenye maono mkoa wa Mara, Veronica Modest kwa niaba ya Mwenyekiti wa Visionary Women Journalists amesema kutembelea wafungwa ni moja ya uwajibikaji na uhabarishaji kwa utume  wa kuwajali na kuwafariji watu.

     Mtunza hazina wa kikundi cha waandishi wa habari Wanawake wenye maono mkoa wa Mara, Veronica Modest

    Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Musoma Salome Mushasha akikabidhi msaada kwa mkuu wa Gereza SSP Jackson Murya

   Naibu Msajili Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Eugnea Rujwahuka (aliyevaa kofia), wa kwanza kulua ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Musoma Salome Mushasha.

      Joyce Sokombi akisalimiana na mtendaji wa Mahakama kuu Kanda ya Musoma Festo Chonya


No comments