HEADER AD

HEADER AD

MHASHAM MWIJAGE ASIMIKWA KUWA ASKOFU MKUU KANISA KATOLIKI JIMBO LA BUKOBA



Na Alodia Dominick, Bukoba 

KANISA Katoliki limemsimika rasmi askofu mteule wa jimbo katoliki la Bukoba Mhasham Jovitus Mwijage na kuwa askofu mkuu wa jimbo la Bukoba baada ya kuteuliwa na baba Mtakatifu Papa Francis mnamo Oktoba 19 mwaka huu. 

Askofu huyo ametakiwa kuwa daraja la kuonyesha njia za kutatua changamoto zinazowakabili watu wote bila kujali dini zao.

Askofu Mwijage aliteuliwa baada ya kustaafu askofu mkuu wa jimbo hilo Desdelius Rwoma, mwezi Oktoba 22 mwaka 2022, hali iliyosababisha baba mtakatifu Papa Francis kumtangaza askofu msaidizi wa jimbo katoriki la Bukoba Methodious Kilaini kuwa askofu msimamizi wa kitume wa jimbo hilo mpaka Januari 27 mwaka huu ambapo amestaafu rasmi.

      Katikati ni askofu wa jimbo katoliki  Bukoba Jovitus Mwijage akitoa baraka kwa waumini na viongozi mbalimbali wa serikali waliohudhuria   misa takatifu ya kuwekewa wakfu na kusimikwa kwake rasmi.

Tukio hilo lilifanyika Januari 27' mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Kaitaba manispaa ya Bukoba ambapo liliendeshwa na askofu kiongozi kardinali Protase Rugambwa ambaye pia ni askofu mkuu wa jimbo katoriki la Tabora.

Kardinali Rugambwa alimtaka askofu Mwijage kuongozwa na nguzo kuu ambayo ni upendo kwa watu walioko chini yake,wa dini zote,wanaoamini na wasioamini na kusikiliza changamoto zao zinazosababisha magumu wanayoyapitia hasa kwa nyakati hizi na kuwashauri ni jinsi gani wanaweza kuyatafutia ufumbuzi yatakayo waongoza kujiletea maendeleo.

"Kwa msaada wa roho Mtakatifu na kwa hari ya jitihada zako katika kutafakari neno la Mungu na kuzisoma alama za nyakati utaweza kutambua na kung'amua mapenzi ya Mungu na ujumbe wa kinabii unaotukuka uwafikishie watu wako"amesema Rugambwa.

Amemshauri pia kutoa mwanga na mwongozo wa machungu na fadhaha za wanadamu wa nyakati hizi ambayo watu wa nyakati hizi  yaani magumu na matatizo ambayo watu yanawakabili watu wa nyakati hizi wanakabiliwa na kufadhaishwa nayo.

"Hasa wanavyoweza kukabiliana nayo na kutatua masuala ya kijamii yenye uzito wa kipekee na yahusuyo haki, amani, upatanisho na maridhiano, ustawi na maendeleo ya watu "aliongeza Kardinali Rugambwa.

Naye Naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni waziri Nishati Doto Biteko ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alimuomba askofu Mwijage kueneza farsafa  R4 ya kuwaunganisha watu kuwa wamoja katika kujenga Taifa huru.

    Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Doto Biteko aliyekuwa mgeni rasmi katika misa ya kuwekewa wakfu  askofu Jovitus Mwijage akimpa pongezi kwa kuwa askofu wa jimbo hilo.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassani alikuwa na ndoto ya kuwaunganisha watu ambayo ni pamoja na  maridhiano, ambapo amekuwa kinara wa maridhiano na ametafsiri kwa vitendo hasa wakati mtu mmoja anapojaribi kutofautiana yeye hawi mwepesi wa kukasirika na kuhamaki na badala yake humpa nafasi kila mmoja kutoa maoni yake ili kupata suluhisho zuri.

"Changamoto hizi tutaziondoa endapo hatutaruhusu mgawanyiko miongoni mwetu, tunaweza kutofautiana kwa mawazo na mitazamo lakini tukumbuke kinachoshinda ni nguvu ya hoja na wote tuwe wamoja kujenga Taifa huru lenye usawa na haki kwasababu haki huunganisha Taifa "amesema Biteko.

Balozi wa baba mtakatifu nchini Tanzania askofu Angelo Accattino akisoma hati ya kitume kwa niaba ya baba mtakatifu amesema askofu Jovitus Mwijage aliteuliwa rasmi Oktoba 19, mwaka jana kuwa askofu wa jimbo katoriki la Bukoba.


No comments