HEADER AD

HEADER AD

RC MTANDA, RPC NJERA WASEMA JAMBO SHEREHE YA FAMILIA YA POLISI

Na TImothy Itembe, Tarime

MKUU wa mkoa wa Mara, Said Mtanda amewataka wananchi kuwa na imani na jeshi la Polisi Tarime, Rorya huku akilipongeza kwa ubunifu kwa kuwakutanisha maofisa wa polisi  kutoka nchi jirani ya Kenya katika sherehe ya siku ya familia ya Polisi (Police Day).

Mtanda aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo Januari, 27,2024,  amelipongeza Jeshi la Polisi Tarime, Rorya kwa kuwaunganisha wadau mbalimbali kwenye sherehe hiyo ili kupata ujumbe wa salamu za serikali ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya jamii kujua haki za kimsingi kutoka Jeshi hilo.

      Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda aliyevaa suti nyeusi akiwa na maafisa wa polisi Tarime/Rorya , waliochuchumaa na maafisa wa polisi 

Mtanda ametumia nafasi hiyo kusema kupitia sherehe hiyo, polisi imewajali wananchi na kupata frusa mbalimbali za kielimu za kujua haki zao.

"Kupitia hadhara hii naomba wananchi waitumie fursa ya wiki ya sheria kwenda kupata msaada wa kisheria unaoendelea kutolewa kupitia wadau mbalimbali wakiwemo wa mahakama.

Pia ameitaka jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo katika kupinga vitendo vya kihalifu ili wananchi  waendelee kuishi na kufurahia matunda ya uhuru wa nchi yao.

RC Mtanda amelisisitiza jeshi hilo kwamba, ili liendelee kuaminiwa na wananchi linatakiwa kuzingatia nidhumu na iwe kipaumbele na  kwamba ili kutekeleza vyema majukumu yake linatakiwa kufanya kazi kwa weledi.

       Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda

'Wale wachache ambao wana sifa ya kuchafua Jeshi la polisi hatutawavumilia wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria hatua ambayo itachangia kuimarisha ushirikiano" amesema Mtanda.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Mark Njera amewasisitiza wananchi kuachana na vitendo vya uhalifu vikiwemo vya ukatili wa kijinsia, kujinyonga kwa wivu wa mapenzi na mauji. 
              RPC Tarime Rorya Mark Njera

Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo akiwemo mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Tarime na Mwanza  Peter Zacharia ameiomba jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi.

" Tunapongeza jeshi la polisi kutoa vyeti na zawadi kwa jamii kwa lengo la kujali michango wanayotoa kwa jeshi hilo, wananchi tuendelee kutoa ushirikiano kwa polisi, kwa kufanya hivyo kutakuwa na mafanikio zaidi" amesema Zakaria.



No comments