MKUTANO MKUU WAMACU WABARIKI UZINDUZI WA KIWANDA
Timothy Itembe , Tarime
MKUTANO mkuu wa(14) wa Chama cha wakulima mkoa Mara WAMACU umebariki kuzinduliwa kiwanda cha kuchakata kahawa kilichojengwa pamoja na gharama za ununuzi wa mashine kwa Tsh. 1,303,376,250.
Mkutano uliandaliwa kwa lengo la kujadili na kupitisha bajeti ya WAMACU ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa miaka mitano.
Mkutano huo ambao umefanyika Januari 31, 2024 ukiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Devd Hechei ambapo mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda amezindua kiwanda hicho.
Katika uzindunzi huo Rc Mtanda amewataka wafanyakazi pamoja na wananchi ambao wanazungukwa na kiwanda hicho kulinda na kutunza miundombinu ya kiwanda ili kidumu.
Wakati huohuo amezitaka taasisi mbalimbali ikiwemo Magereza, JKT na wengine waungane kuungana pamoja na WAMACU kushirikiana ili kuhakikisha wanaongeza uzalishaji.
RC Mtanda amewataka wajumbe waliochaguliwa na kuaminiwa na wakulima kuwa mabalozi wazuri na wasimamizi wa bajeti iliyoandaliwa na wataalamu ili bajeti hiyo iguse hitaji la kila mkulima na kumwinua mkulima ili kuondokana na umasikini wa kipato.
Meneja Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Mara Cooperative Union WAMACU, Samweli Gisiboye amesema katika msimu wa 2023/2024 Chama kimeuza kahawa katika soko la moja kwa moja kiasi cha kilo 249540.
Aidha amesema mauzo yote mpaka sasa yamefikia jumla ya Tsh. 1,346,359,300 kabla ya makato ya Bodi ya kahawa(Export fee asilimia moja na Coffee development fund 200 kg).
Meneja huyo ameongeza kuwa mkopo wa mashine ya kuchakata kahawa kavu na mbivu wa Tsh. 603,376,250 uliochukuliwa kutoka benki ya kilimo TADB, Tsh. 523,376,250 ilikuwa ni mashine na Tsh 80,000,000 ilikuwa ya ujenzi wa miundombinu.
Hata hivyo amesema gharama ya miundombinu imeongezeka na kufikia Tsh. Milioni 700,000,000 ambayo imeombwa kupelekwa kwenye mkopo wa muda mrefu kati ya fedha ya mkopo Tsh. Milioni 184,026,316.
Mkuu wa wilaya Tarime Michael Mntenjele amesema matarajio ya chama hicho ni kuhakikisha ushirika unaimarika.
"Baadhi ya wakulima wasio waaminifu wanachukua mbolea na kwenda kuuza kimagendo, tunaomba biashara ya mbolea iende kwa wakulima ambao ndio walengwa kwa kuwa serikali inatoa fedha kuingiza kwenye Ruzuku ya mbolea.
"Tuwahamasishe vijana kupenda kilimo hususani kilimo cha kahawa kwa sababu kilimo cha sasa ni kilimo biashara" amesema Dc Mntenjele
Samsoni Shiengo kutoka Banki TADB amekitaka chama hicho kuhakikisha kahawa inakuwa na uzalishaji mkubwa katika kwa mkoa Mara.
Mrajisi mkoa Mara Lucas Kiondere amewapongeza WAMACU kwa ukamilishaji wa kiwanda ambacho kitakuwa chachu na kutoa ajira na kukuza uchumi wa mkulima wa kahawa.
Post a Comment