WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI TAA ZA BARABARANI TARIME
JESHI la Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya limewakamata watu wawili kwa tuhuma za wizi na uharibifu wa taa za barabarani.
Akizungumza na DIMA Online Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Mark Njera amesema kwamba mpaka sasa kuna matukio mawili yameripotiwa ya uharibifu na wizi wa taa za barabarani mjini Tarime.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Polisi Tarime/Rorya Mark Njera
Kamanda Njera amesema kwamba tukio la kwanza liliripotiwa Desemba, 8, 2023 ambapo betri mbili ziliibwa na Sola ya taa moja iliharibika baada ya nguzo yake kuangushwa.
Amesema kwamba tukio lingine liliripotiwa Desemba, 27, 2023 ambao betri na sola ya taa moja ziliibwa na kwamba matukio yote yalitokea eneo la Darajani lililopo karibu na chuo cha ualimu Tarime.
"Uchunguzi umefanyika na watuhumiwa wawili wamekamata na wamekili kuhusika na matukio hayo, Juhudi za kuwakamata watuhumiwa wengine watatu waliotajwa kuhusika na matukio haya zinaendelea " amesema Kamanda Njera.
Akizungumza na Gazeti hili, Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) , Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mhandisi Charles Marwa amesema kumezuka wizi wa taa za barabarani lakini wananchi hawatoi taarifa dhidi ya wanaohujumu miundombinu ya barabara jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.
" Tayari mikakati imewekwa kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wahalifu wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
Taa iliyoibwa betri
"Niwaombe wananchi wa Tarime pale ambapo mmoja wetu ataonekana anahujumu basi najua eneo hilo wapo wananchi tusiwafiche tutoe taarifa na ikiwezekana tuwakemee, tujitahidi kuitunza na kuipenda miundombinu ya barabara inamanufaa kwetu sote " amesema Mhandisi Marwa.
Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mara, Mhandisi Vedastus Maribe amewashauri wananchi kutoa ushirikiano kuhakikisha taa zinalindwa kwasababu zimewekwa kwa manufaa yao na zinasaidia usalama wakati wa usiku.
"Zinasaidia pia wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa muda mrefu nyakati za usiku, kwahiyo niwaombe wananchi tuzilinde zina manufaa kwetu" amesema Mhandisi Maribe.

Post a Comment