WANAUME WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI WA WATOTO
Na Alodia Babara, Bukoba
JESHI la polisi mkoani Kagera linatarajia kuwafikisha mahakamani wanaume wawili ambao wanatuhumiwa kwa matukio ya ubakaji wa watoto.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari Januari 15, mwaka huu amesema kuwa watuhumiwa hao wa ubakaji wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Chatanda amesema kuwa, jeshi hilo linaendelea na taratibu za kisheria dhidi ya watuhumiwa hao ambao ni Gaudiozi Rutayuga Yepa (42) mfanyabiashara wa simu katika mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe na Philemon Reveliani (39) mkazi wa kisiwa cha Msira manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za ubakaji.
“Mtuhumiwa Rutayuga Yepa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 02, mwaka huu majira ya saa 20:00 usiku katika mtaa wa Bomani, kata ya Kayanga, wilaya ya Karagwe ambapo alimrubuni mtoto mwenye umri wa miaka 10 mwanafunzi wa darasa la nne.
"Mruhumiwa huyo alimwambia apande kwenye gari lake lenye namba za usajiri T 639 BKP aina ya pijoti ili ampeleke nyumbani kwao na baada ya mtoto huyo kupanda ndipo alimbaka kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali mwilini”amesema Chatanda"amesema Kamanda
Amesema mtoto huyo baada ya kurudi nyumbani na mama yake mzazi kuona alivyokuwa ameumizwa alimkimbiza hospitali ya Nyakahanga wilaya ya Karagwe kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
Ameeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa na kudhaminiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kuanzia sasa.
Wakati huo huo, mtuhumiwa Philemon Revelian ambaye ni baba wa kambo wa mtoto aliyembaka mwenye umri wa miaka mitano anadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 26, mwaka jana majira ya 09:00 asubuhi.
Mtuhumiwa huyo akiwa amebaki nyumbani na mtoto huyo katika kisiwa cha Msira kata ya Miembeni manispaa ya Bukoba baada ya mama mzazi wa mtoto huyo Gaudensia Charles (30) mkazi wa kisiwa hicho kuwa ameenda hospitali kujifungua.
Chatanda ameema kuwa, mama huyo akiwa ameenda katika kituo cha afya Zamzam kilichopo manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kujifungua na baada ya kurudi nyumbani ndipo aligundua kuwa mtoto wake amebakwa.
" Baada ya kugundua kuwa mtoto wake amebakwa na kufuatilia kwa kina zaidi ndipo aligundua kuwa, kitendo hicho kilifanywa na baba yake wa kambo ambaye ndiye mtuhumiwa"amesema.
Amesema mtoto anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera,Bukoba na hali yake inaendelea vizuri na mtuhumiwa atafifikishwa mahakamni mara tu upelelezi na taratibu za kisheria zitakapokamilika.
Jeshi la polisi mkoa wa Kagera limetoa onyo kwa watu wote wenye tabia hizo zilizo kinyume na maadili ya Kitanzania kuacha mara moja na halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote wenye tabia hizo.
Amewaomba wananchi wote kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha mkoa wa Kagera unaendelea kuwa salama.
Post a Comment