WASEMAVYO WANANCHI, WANASIASA TARIME MAANDAMANO YA CHADEMA
>>> Wananchi Tarime waipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kuhurusu maandamano
>>Wanaccm wasema wakati CHADEMA wao wanaandamana, CCM wanajipanga uchaguzi Serikali za mitaa
>>Wanachadema wasema Serikali ndio inasababisha fujo
>>>ACT Wazalendo yasema Rais Samia amethubutu kutengua marufuku waliyoiweka ya kuzuia maandamano
Na Dinna Maningo, Tarime
BAADHI ya Wananchi na Wanasiasa wilayani Tarime mkoa wa Mara, ambao wamezungumza na chombo hiki cha Habari cha DIMA Online, wameeleza hisia zao baada ya Serikali kuruhusu Chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Taifa kufanya maandamano ya amani.
Mwandishi wa DIMA Online amefanya mazungumzo nao kufahamu nini mitazamo yao na wasemavyo baada ya Serikali kuruhusu maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Januari, 24, 2024 yakiongozwa na viongozi wa Kitaifa wa Chama hicho.
Kwa mujibu wa CHADEMA maandamano hayo yalilenga kufikisha jumbe mbalimbali ikiwemo kuhimiza serikali mchakato wa katiba mpya, changamoto ya ugumu wa maisha.
Pia marekebisho kwa baadhi ya Miswada ya sheria na utitiri wa tozo, na kodi ambazo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara na wananchi.
Viongozi wa vyama vya upinzani wamesema kwamba maandamano ni haki ya kikatiba lakini yalizuiliwa na kudidimizwa na serikali iliyopita ya awamu ya tano iliyoongozwa na Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wake ambaye kwa sasa ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi waipongeza Serikali
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa hatua ya kuruhusu CHADEMA kufanya maandamano ya amani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa hatua ya kuruhusu CHADEMA kufanya maandamano ya amani.
Wamesema wameshangaa kuona maandamano hayo yamefanyika kwa amani bila vurugu jambo ambalo hawakulitegemea huku wakiiomba Serikali kutozuia maandamano kwa vyama vya siasa na makundi mengineyo.
Mweka hazina Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime, Abia Orindo mkazi wa Nyamongo, ameipongeza Serikali " Naipongeza Serikali kuruhusu maandamano, tumeshangaa kusikia maandamano yanafanyika kwa amani.
"Huwa tunashuhudia upinzani wakitaka kufanya maandamano au kundi lingine wanazuiliwa na polisi watu wanapigwa na kujeruhiwa.
" Nakumbuka kule Murwambe wananchi walifanya maandamano kudai fidia walipigwa na polisi hata mama yangu akapigwa, watu wakaogopa kudai haki zao. Tunajiuliza kwanini serikali ilizuia maandamano mbona ilivyoruhusu hakuna fujo iliyotokea ? alihoji Abia.
Deo Ching'wa Chacha mfanyabiashara wa viatu vya mtumba mjini Tarime amesema " Suala la maandamano kufanyika ni haki ya kikatiba ilimradi taratibu zimefanyika. Kilichokuwa kinasumbua nchi hii ni hofu ya kupandikizana.
" lengo la maandamano ni kufikisha ujumbe husika, maandamano ya jana nadhani serikali imeona, Taifa limeona na ulimwengu umeona kwamba Tanzania ina amani isipokuwa serikali ndiyo ilikuwa na hofu" amesema Deo.
Lucus Mwita mkazi wa Rebu shuleni ambaye ni mwendesha pikipiki (Bodaboda) amesema" Rais Samia katoa haki ya uhuru wa mawazo kupitia maandamano.
"Ni haki ya watu kutoa dukuduku lao ukizingatia wao wenyewe CHADEMA walisema ni maandamano ya amani na kweli yamekuwa ya amani hakuna fujo iliyotokea " amesema Lucus.
Daniel Chacha Magige mkazi wa Kata ya Ganyange amesema maandamano ni mazuri kama yakifanyika kwa amani na ameipongeza serikali kuruhusu maandamano na kusema kuwa yalipozuiliwa yalijenga chuki baina ya watu na serikali.
Wanachadema wasema Serikali ndio tatizo
Baadhi ya wanachadema wamesema kuwa serikali ndio husababisha fujo pindi hizuiapo maandamano ya CHADEMA.
Katibu wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu Kanda ya Serengeti CHADEMA, Mrimi Zablon Mwita, mkazi wa Kata ya Gwitiryo amesema " Maandamano ni haki ya Kikatiba, waliokuwa wanafanya maandamano ya CHADEMA yawe ya fujo ni Serikali iliyokuwa inayazuia likiwemo Jeshi la Polisi.
"Serikali ndio chanzo cha fujo maana iliporuhusu maandamano hakuna fujo iliyotokea. Nawashukuru wana Dar es Salaam kufanya maandamano ya amani, hiyo kwetu ni ishara njema na ujumbe mahususi umefika, ujumbe ni kushinikiza Serikali ichukie hatua juu ya hali ngumu ya maisha, Katiba mpya, Tozo.
" Kuna miswada inayohitaji marekebisho mswada wa sheria ya vyama vya siasa, sheria ya uchaguzi, mswada wa rais, wabunge na madiwani. Tunahitaji miswada itakayoleta mageuzi makubwa ya kidemokrasia kwenye nchi yetu" amesema Mrimi.
Afisa Idara ya Mawasiliano na Interejensia CHADEMA Kata ya Matongo na Kata ya Kemambo -Nyamongo ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Tawi la Nyabichune, Jonas Chacha Magwe amesema Serikali imefanya jambo jema kuruhusu maandamano.
"Naipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeweka usawa katika vyama vya upinzani maana tumekuwa tukishuhudia CCM ikifanya maandamano lakini CHADEMA ikitaka kufanya maandamano inazuiliwa.
"Hii itabadili akili za wananchi kwamba kumbe anaweza kuingia kiongozi mwingine katika urais na akabadili mfumo uliokuwa umekaririwa kwenye serikali, kwakweli rais Samia katuonesha Demokrasia kwa vyama vya upinzani.
Jonas amesisitiza kuwa maandamano hayo yalete tija kwa taifa yasiwe na manufaa kwa mtu binafsi au kiongozi huku akiiomba Serikali kutekeleza kwa ustawi wa Taifa la Tanzania kile ambacho CHADEMA imekuwa ikishauri na kukosoa kupitia maandamano na mikutano.
"Naipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeweka usawa katika vyama vya upinzani maana tumekuwa tukishuhudia CCM ikifanya maandamano lakini CHADEMA ikitaka kufanya maandamano inazuiliwa.
"Hii itabadili akili za wananchi kwamba kumbe anaweza kuingia kiongozi mwingine katika urais na akabadili mfumo uliokuwa umekaririwa kwenye serikali, kwakweli rais Samia katuonesha Demokrasia kwa vyama vya upinzani.
Jonas amesisitiza kuwa maandamano hayo yalete tija kwa taifa yasiwe na manufaa kwa mtu binafsi au kiongozi huku akiiomba Serikali kutekeleza kwa ustawi wa Taifa la Tanzania kile ambacho CHADEMA imekuwa ikishauri na kukosoa kupitia maandamano na mikutano.
ACT yasema Rais Samia analinda Katiba
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Mara, Charles Mwera aliyewahi kuwa Mbunge jimbo la Tarime amesema " Mambo ya maandamano Katiba inaruhusu, utawala wa rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli ndio ulikuwa unakandamiza maandamano na mikutano ya hadhara ambayo ni halali kwa vyama na makundi mbalimbali.
" Nampongeza rais Samia maana angekataa maandamano yasingefanyika, alikuwa msaizidi wa Magufuli wakafuta maandamano na mikutano lakini ameona arejeshe waliyofuta kwakuwa ni rais na alikula kiapo cha kuilinda na kuiheshimu Katiba" amesema Charles.
" Serikali inapozuia maandamano ndio inaleta fujo kwasababu wanadanganya watu na kuleta fujo, sasa mbona jana CHADEMA imefanya maandamano na hakuna fujo iliyotokea ?" anahoji Mwenyekiti huyo.
Kiongozi huyo amemwomba Rais Samia na Serikali kusimamia yale yaliyoshauriwa na vyama vya upinzani na kwamba vyama vya upinzani haviichukii serikali bali vinakosoa ili serikali ijisahihishe.
" Kikosi kazi kilifanya kazi kikapendekeza mambo lakini miswada iliyokwenda Bungeni imeonekana baadhi ya mambo yaliyopendekezwa hayamo, kwahiyo Rais asimamie.
" Hata Mahakama ilishatoa maamuzi hata ile kesi ya Bob Chacha Wangwe ilikataa wakurugenzi wasisimamie uchaguzi" amesema.
CCM yasema maandamano hayawapi presha
Mwenyekiti Mstaafu Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (Namba Tatu) amesema kitendo cha Serikali kuruhusu maandamano ni demokrasia na haiathiri kisiasa Chama cha Mapinduzi.
"Rais ni mtu wa Demokrasia tunaamini kwa niaba ya serikali aliridhia maandamano hayo. Niwaombe wana CCM wenzangu tusiogope kuona CHADEMA wanaandamana, wao wakati wanaandamana sisi tujipange kuhakikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa tunapata ushindi mkubwa.
" Wakati huo wao wanaandamana sisi tukae karibu na wananchi tuwaeleze mambo yaliyofanywa na serikali ya CCM katika kuhakikisha inatekeleza ilani ya CCM " amesema Kiboye.
" Wakati huo wao wanaandamana sisi tukae karibu na wananchi tuwaeleze mambo yaliyofanywa na serikali ya CCM katika kuhakikisha inatekeleza ilani ya CCM " amesema Kiboye.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Manga Samwel Itinde Mseti amesema " Maandamano ya CHADEMA hayatutetemeshi kwasababu kama ni maendeleo Serikali ya rais wetu mama Samia imefanya na CCM itashinda kwasababu Ilani yetu ya chama serikali inatekeleza " amesema Samwel.
Katibu Mwenezi mstaafu Kata ya Turwa, Thobias Joseph Marwa amesema CHADEMA kufanya maandamano rais ametimiza demokrasia kwani walipozuiliwa waliiona serikali inawaonea.
"Sisi hayo maandamano hayatupi hofu kwasasabu hata walipoandamana hakuna hatari iliyotokea, wanapoandamana yapo mazuri wanayoyasema yanafanyiwa kazi na yapo mabaya wanayoyasema hayafanyiwi kazi hivyo tusiwapuuze.
Ameongeza kuwa, upinzani ni sehemu mojawapo ya kuikosoa serikali pale inapokosea ili iendelee kujisahihisha na kujirekebisha na kwamba kuruhusiwa kufanyika maandamano ni jambo la msingi na wananchi wataona uongozi wa rais Samia ni wa kidemokrasia.
Post a Comment