WAZEE TARIME WAOMBWA KUTOA ELIMU YA MAADILI KWA VIJANA
Na Timothy Itembe, Tarime
WAZEE wilayani Tarime mkoani Mara, wametakiwa kutoa elimu kwa vijana juu ya maadili mema na Tamaduni za Kitanzania badala ya kuiga tamaduni za kigeni.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini, Michael Kembaki mjini Tarime wakati akiongea na wazee katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi na kuwataka wazee hao kuwafundisha vijana wao maadili mema ya Tamaduni za kitanzania badala ya kubobea tamaduni za kigeni ambazo baadhi zinavunja maadili ya kitanzania na kiafrika.
Aidha Kembaki alisema kuwa umefika wakati mwafaka Bunge kutunga sheria ya wazee kupata asilimia ya fedha ya makusanyo ya ndani ya halmashauri kama vile makundi ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu wanavyopokea ili kuanzisha miradi midogo midogo ya kujikwamua nakuondokana na wimbi la umasikini.
Pia Kembaki aliongeza kuwa atawasiliana na mamlaka husika juu ya wazee wa Tarime kupatiwa chumba kwa ajili ya kuanzisha makumbusho ya zana za makabila ya. Watu wa mkoa Mara ili watalii wa ndani na nje kuja kutembelea makunbusho hayo.
Katibu wa Shirika lisilo la kiserikali SAPITA, Simon Munyoro alimwomba mbunge wa huyo kuwasemea wazee Bungeni ili sheria itungwe ya wao kuwa na mwakilishi Bungeni wa kuwasemea kama ilivyo kwa makundi mengine ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
"Mheshimiwa Mbunge wazee karibia wote wamepatiwa vitambulisho vya matibabu kwa wazee bila malipo, vitambulisho hivyo vimekuwa changamoto hawapatiwi dawa badala yake wazee wanaambiwa wakanunue dawa kwenye maduka ya watu binafsi huku wakijua kuwa wazee hawana fedha na kama tungelikuwa na mwakilishi Bungeni angelitusemea" alisema Munyoro.
Khadija Omari aliomba serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kuwajali wazee kwa kuwa wazee ni tunu ya Taifa
Post a Comment