DC TARIME : WANANCHI JITOKEZENI UWANJA WA TARAFA, SERENGETI MUMSIKILIZE WAZIRI MKUU
Na Dinna Maningo, Tarime
MKUU wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anayetarajia kuwasili wilayani Tarime kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, DC Mntenjele amesema kuwa Waziri mkuu atawasili wilayani Tarime kwa ziara ya siku mbili Februari, 27-28, 2024 akitokea wilaya ya Serengeti.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele
" Waziri Mkuu atakuwa Tarime tarehe 27, ataweka jiwe la msingi katika halmashauri ya wilaya ya Tarime Kata ya Nyamwaga na kusalimia wananchi" amesema Dc Mntenjele.
Amesema tarehe 28 Waziri Mkuu atakuwa na ziara wilayani Rorya kisha atakwenda Sirari na kufanya mkutano wa hadhara uwanja wa Tarafa kuzungumza na wananchi.
Pia atafika Tarime mjini na kuweka jiwe la msingi soko kuu la kimkakati kisha ataelekea katika uwanja wa Serengeti mjini Tarime kufanya mkutano wa hadhara.
"Nawaomba wananchi wa Tarime wajitokeze kwa wingi uwanja wa Tarafa na Serengeti ili waweze kumsikiliza Waziri mkuu, ikitokea nafasi ya maswali wawe huru kusema ili waweze kusikilizwa" amesema Dc Mntenjele.
Post a Comment