HEADER AD

HEADER AD

RATIBA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI RORYA, TARIME


Na DIMA Online, Mara

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa yupo mkoani Mara kwa ziara ya kikazi Februari, 25-29, 2024 ambapo atatembelea na kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi pamoja na kuongea na watendaji wa serikali pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Februari, 28, 2024 Waziri mkuu atafanya ziara wilaya ya Rorya na Tarime .

Asubuhi saa 2:00-3:00 msafara utaelekea eneo la mradi wa maji Komuge, 3:00-3:30 Waziri mkuu atatembelea na kukagua mradi wa maji Komuge, 3:30-4:20 msafara utaelekea hospitali ya wilaya ya Rorya, 4:20-5:00 atatembelea na kukagua hospitali ya wilaya ya Rorya.

Msafara utaelekea eneo la mkutano wa hadhara Utegi saa 5:00-5:20, saa 5:20-6:20 Waziri mkuu atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Utegi, 6:20-6:50 msafara utaelekea Sirari- Tarime, 6:50-8:00 mkutano wa hadhara Sirari.

Saa 8:00-8:30 msafara utaelekea Tarime mjini, 8:30-9:00 Waziri mkuu atakagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa soko la kimkakati Tarime mjini, 9:00-9:10 msafara utaelekea uwanja wa Serengeti-Tarime mjini  kwa ajili ya mkutano.

Mkutano wa hadhara uwanja wa Serengeti utafanyika saa 9:20-11:20 na hivyo kuhitimisha ziara yake katika wilaya hizo ambapo ataendelea na ziara nyingine wilaya ya Musoma Februari, 29,2024.

No comments