HEADER AD

HEADER AD

JET YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KURIPOTI MIGONGANO BAINA YA BINADAMU, WANYAMA

Na Andrew Chale, Bagamoyo 

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) , kimetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari za Mazingira juu ya kuripoti kwa usahihi taarifa za Mradi wa Kupunguza Migongano baina ya binadamu , wanyamapori Tanzania, Ukanda wa Ruvuma yaliyoaandaliwa na GIZ huku ukitekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT). 

Awali akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku mbili, 22-23 Februari, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Maliasili na Utalii,  John Mapepele aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema kwa sasa wizara ina falsafa mbili kubwa.

     Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Maliasili na Utalii,  John Mapepele

Amesema falsafa hiyo ni pamoja na Uhifadhi na Utangazaji utalii  na hivyo mafunzo hayo lengo lake kuu ni kusaidia katika kuimarisha uhifadhi ili usaidie katika utangazaji Utalii suala mabalo ni muhimu kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

"Uhifadhi ukiimarika mazao ya uhifadhi pia yataimarika kama vile utalii na hivyo kulifanya taifa kupata fedha za kigeni na kuimarisha uchumi wake kupitia hifadhi zetu." amesema Mapepele.

Ameongeza kuwa, Wizara imewekeza nguvu kubwa katika njia bora na za kisasa kutangaza Utalii na kuhifadhi huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha uhifadhi ambapo amehakikisha uhifadhi unaendelezwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vizazi vya baadae

Aidha, Mapepele amewataka wanahabari kutumia siku hizo mbili za mafunzo ambazo zitawasaidia kujengewa uwezo kwa ajili ya kutoa habari za rasilimali kwa faida ya Taifa kwa ujumla.

“Katika kipindi hiki mbapo tutakuwa hapa kwa siku mbili tutumie fursa hii adhimu vizuri kwani itatusaidia sana kutujengea uwezo katika nchi nyingi ambazo zimeendelea hufanya haya tunayofanya leo’’ amesema Mapepele.

Aidha amebainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo imepiga hatua kubwa katika eneo la uhifadhi ambapo asilimia 32 ya nchi imehifadhia jambo ambalo ni la kupongezwa.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), John Chikomo ameishukuru GIZ na Serikali ambapo amebainisha kuwa mafunzo yatawasaidia waandishi kutoa Habari za migongano baina ya binadamu na wanyamapori kwa ufasaha na weledi mkubwa.

Nae Mshauri wa mradi huo kutoka GIZ, Anna Kimambo amesema kuwa mradi kwa unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kutoka maeneo ya mradi ikiwemo Liwale mkoa wa Lindi, Namtumbo na Tunduru kutoka mkoa wa Ruvuma ambapo Vijiji 30, vitafikiwa katika mradi huo.

       Nae Mshauri wa mradi huo kutoka GIZ, Anna Kimambo

Katika mafunzo hayo, wawezeshaji wataalamu wa masuala ya migongano baina ya binadamu na wanyama; Dk. Maria Montero kutoka GIZ, na John Noronha wamesema kumekuwa na changamoto ya mwingiliano kati ya binadamu na wanyama na kuchangia migogoro.

Naye mwanahabari mkongwe nchini Pili Mtambalike akiwasilisha mada juu ya uandishi wa makala zenye vionjo tofauti katika ubunifu wa taarifa (Story Telling ).

Mafunzo hayo pia yamehudhuriwa na maafisa habari kutoka Halmashauri za Liwale, Namtumbo na Tunduru pamoja na waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini.




No comments