JUMUIYA YA WAZAZI MARA NA UTOAJI ELIMU YA MAADILI BUTIAMA
UMOJA wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliundwa mwaka 1955 ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuundwa kwa chama cha TANU mwaka 1954.
Umoja huu uliundwa ukiwa na misingi mikuu miwili, Elimu pamoja na Malezi, na mtu mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa jumuiya ya wazazi.
Majukumu ya jumuiya ya wazazi ni kuhamasisha wazazi na watanzania wa rika zote juu ya umuhimu wa elimu pamoja na kuanzisha na kusimamia shule za jumuiya .
Jukumu lingine ni kusimamia maadili na malezi bora kwa vijana na jamii kwa ujumla ili kujenga taifa lenye maadili na linalosimamia misingi ya utamaduni wa Tanzania.
Pia kusimamia rasilimali pamoja na shughuli za kiuchumi zilizopo na kubuni miradi mipya, kwa manufaa ya Jumuiya na Taifa kwa ujumla.
Malengo ya jumuiya ya wazazi ni kuhakikisha kuwa, wazazi kama nguzo ya jamii wanashiriki katika ustawi wa chama na taifa kwa kusimamia elimu, malezi na maadili kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuhakikisha chama cha mapinduzi kinakua imara na madhubuti siku zote.
Mwezi Januari, 31, 2024 Vongozi wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara, walifika wilayani Butiama na kuungana pamoja na wazazi wa jumuia katika wilaya hiyo kuadhimisha kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi kilichozaliwa Februari, 05, 1977.

Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Butiama wakiwapokea viongozi wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara baada ya kuwasili wilayani humo
Viongozi hao wa jumuiya wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Mara, Julius Kambarage Masubo wakatumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya maadili kwa wanajumuiya wa Butiama.
Pia Viongozi hao wakafika shule ya sekondari Bumaswa iliyopo kijiji cha Kamgendi, Kata ya Bwiregi na kutoa elimu ya maadili kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kupanda miti.
Viongozi wanafanya hivyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa jumuiya ya wazazi kuhakikisha inasimamia malezi na kutoa elimu ya maadili kwa jamii ili kujenga taifa lenye maadili.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Mara Julius Masubo anaeleza kuwa wao kama jumuiya wanashughulika na malezi, Elimu na mazingira na kwamba malezi huanzia nyumbani.

" Kuna makundi matatu katika malezi, malezi ya kwanza yanaanzia nyumbani mtoto anapozaliwa anatunzwa na kulelewa na wazazi, akifikia umri wa kwenda shule, walimu nao wataendelea kukuza malezi yao, baada ya kuhitimu shule wanakabidhi kwa jamii.
Anasema kuwa mtoto akilelewa katika msingi mbaya wa maisha ya nyumbani kwao anapokwenda shuleni inakuwa ni shida na mzigo kwa mwalimu.
" Kuna baadhi ya watoto wenye tabia mbaya ambazo waliziiga kutoka kwa wazazi wao, watoto wanakopi kwa wazazi wanaangalia tabia za wazazi wanakopi anapokuwa mkubwa inakuwa ni changamoto kumrekebisha.
Samaki mkunje angali mbichi, mtoto akiwa nyumbani na shuleni unaweza kumkunja kwakuwa bado ni mdogo lakini anapokwenda kwenye jamii nje ya shule ni mgumu kumbadilisha tabia kwakuwa anakuwa ni mtu mzima anayefanya maamuzi yake " anasema Masubo.
Masubo anasema kwamba, migogoro ya ndoa inachangia watoto kujifunza tabia mbaya za nje ya ndoa hivyo anawaomba wanandoa kuepuka migogoro ya ndoa kwakuwa upelekea wanandoa kuachana na hivyo watoto kukosa malezi mazuri ya wazazi.
Anawaomba wazazi wawe marafiki na walimu shuleni na wawafuatilie watoto kadri wakuavyo ili wanapokwenda kwenye jamii wawe ni watu wema na wenye heshima.
Nyihita Willfred Nyihita ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM mkoa wa Mara, anasema wazazi wana jukumu la malezi, elimu na mazingira na kwamba kumekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa vijana.

Nyihita Willfred Nyihita ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM mkoa wa Mara
"Tuna wajibu wa kuhakikisha tunaongoza watoto wetu tunawalea katika misingi inayotakiwa. Miaka ya nyuma mtoto alikuwa akianza shule mpaka awe na uwezo wa kushika sikio maana yake tayari amefikia umri wa kuanza shule, amekua katika malezi ya wazazi wake , ameshajifunza kuongea sasa anapaswa kusoma" anasema.
Anaongeza kuwa pamoja na mtoto kwenda kusoma shuleni bado mzazi hapaswi kumwachia mzigo mwalimu bado anatakiwa kumpa malezi mema na kuwa na mahusiano na walimu ili kumjengea mtoto uelewa mpana wa maisha yake.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Butiama Baraka Imanyi maarufu (Obama) anasema maadili ni swala mtambuka na jumuishu si kwa wazazi tu au walimu bali ni jukumu la kila mtu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Butiama Baraka Imanyi maarufu (Obama)
"Maadili siyo tu shuleni na nyumbani pia kwa wazazi, tunawaasa wazazi wawe mlango wa kwanza kuwalea kwasababu maadili yanaanzia nyumbani, pale ambapo kuna changamoto tishirikiane na polisi kitengo cha dawati la polisi.
Anawaasa walimu kujitahidi kuwalea wanafunzi katika maadili mema pindi wawapo shuleni na kwamba walimu watakaokwenda kinyume na maadili na wakabainika vyombo vya dora viwachukulie hatua kali za kisheria.
Mjumbe wa mkutano mkuu CCM mkoa wa Mara na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Mwibara, Kangi Lugola aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya kuzaliwa CCM, anasema simu na runinga zimechangia kuporomosha maadili ya watoto.
Mjumbe wa mkutano mkuu CCM mkoa wa Mara na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Mwibara, Kangi Lugola
"Nitoe wito kwa wazazi wenzangu sisi ndio tuna dhamana kwenye jumuiya hii tujitahidi kudhibiti watoto kwenye matumizi ya simu na vipindi visivyo faa kwa watoto vinavyorushwa kupitia runinga.
"Tuwaepushe na michezo ya kubeti, kuchezea kompyuta kwani vitu hivi vinachangia sana kubadili tabia za watoto, mtoto anakaa hadi saa saba usiku kuangalia mpira muda ambao angelala, na wengine wanabeti badala ya kujisomea " anasema Lugola.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Bumaswa Christina Matiku anawaomba wanafunzi wenzake kutojihusish na vitendo viovu na badala yake wajikite katika masomo kwakuwa elimu ndio ufunguo wa maisha.

Rais Samia apongezwa
Jumuiya hiyo ya CCM inampongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kutekeleza majukumu ya Jumuiya kwani serikali yake imekuwa ikijitahidi kutengeneza mazingira mazuri ya elimu ikiwemo miradi ya ujenzi wa shule.
Mwenyekiti Masubo anasema kuwa Rais Samia anatekeleza malengo ya jumuiya ya wazazi inayosimamia malezi, elimu na mazingira kwani ana hakikisha wanafunzi wanapata elimu kwa kusoma katika mazingira mazuri pasipo kubanana darasani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara Julius Kambarage Masubo akizungumza na wanajumuiya wilayani Butiama
"Tunampongeza rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miradi ikiwemo wilaya ya Butiama na zimefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu, wazazi wamepumzishwa michango ya ujenzi wa shule." anasema.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara, Nyihita Willfred Nyihita anasema kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa kikihakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Baraka Imanyi anasema rais Samia amefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu kuhakikisha miundombinu inakuwa imara hivyo ni matarajio kuona wanafunzi wakifanya vizuri katika masomo yao.
Mkazi wa kijiji cha Masurura Marwa Ngega anaishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia kijenga mabweni kwa watoto wa kike ambayo yamewasaidia kuepuka mimba zisizotarajiwa huku akiwaomba vijana wa kiume wawaache watoto wa kike wasome ili wamalize masomo yao.

Mkazi wa kijiji cha Masurura Marwa Genga
Diwani wa Kata ya Bwiregi Nyageti Joyce Adam anampongeza rais Samia kwa kufanya mambo makubwa kwenye kata yao na wilaya kwa ujumla.
"Katika shule yetu ya Sekondari ya Bumaswa tulikuwa na shida ya mabweni, sasa tumepata bweni na watoto wa kike wanaishi shuleni, watoto hawatembei umbali mrefu hasa wanaotok kilimota zaidi ya 7 katika kijiji cha Nyamisanga " anasema Nyageti.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda alisema kuwa Serikali imetoa fedha sh. bilioni 18.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo ambazo zimesaidia kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba madarasa.
Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo Desemba, 30, 2023 katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, kilichofanyika kwa njia ya Zoom.
Post a Comment