JUMUIYA YA WAZAZI MARA YAMFAGILIA RAIS SAMIA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA
>>Yasema Rais Samia ametekeleza majukumu ya Jumuiya
Na Dinna Maningo, ButiamaJUMUIYA ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Mara imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutafuta fedha hata nje ya nchi ambazo zimewezesha kujenga vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari nchini.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Mara, Julius Masubo amesema Rais Samia ametekeleza majukumu ya Jumuiya hiyo ambayo yanaitaka jumuiya kusimamia malezi, elimu na mazingira.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo hivi karibuni wakati jumuiya hiyo ikiwa katika maadhimisha ya kuelekea siku ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari, 5, ya kila mwaka ambapo jumuiya imetumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya malezi shule ya sekondari Bumaswa wilayani Butiama .
Mwenyekiti Masubo amesema Rais Samia ametekeleza jukumu la elimu kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu kwa kusoma katika mazingira mazuri pasipo kubanana darasani.
"Tunampongeza rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miradi ikiwemo wilaya ya Butiama na zimefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu.
" Nakupongeza Mwenyekiti wazazi wilaya ya Butiama kwa usimamizi mzuri ,sisi jumuiya ya wazazi ndio tunasimamia malezi, elimu na mazingira " amesema Masubo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara, Nyihita Willfred Nyihita amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikihakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara, Nyihita Willfred Nyihita
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Butiama Baraka Imanyi maarufu ' Obama' amesema rais Samia amefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu kuhakikisha miundombinu inakuwa imara hivyo ni matarajio kuona wanafunzi wakifanya vizuri katika masomo yao.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Butiama Baraka Imanyi
Mkazi wa kijiji cha Masurura Marwa Ngega amewashukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia kijenga mabweni kwa watoto wa kike ambayo yamewasaidia kuepuka mimba zisizotarajiwa huku akiwaomba vijana wa kiume wawaache watoto wa kike wasome ili wamalize masomo yao.
Diwani wa Kata ya Bwiregi Nyageti Joyce Adam amemshukuru rais Samia kwa kufanya mambo makubwa kwenye kata yao na wilaya kwa ujumla.

"Katika shule yetu ya Sekondari ya Bumaswa tulikuwa na shida ya mabweni, sasa tumepata bweni na watoto wa kike wanaishi shuleni, watoto hawatembei umbali mrefu hasa wanaotok kilimota zaidi ya 7 katika kijiji cha Nyamisanga.
"Tumepata fedha sh. Milioni 80 kujenga bweni la wavulana japo fedha zilikuwa ndogo kuweza kukamilisha. Tunaomba serikali iweze kutuongezea fedha bweni likamilike na watoto wetu wa kiume wasitembee umbali mrefu" amesema Nyageti.
Ameongeza kuwa, Kata ilikuwa ina changamoto nyingi hasa ya maji lakini rais ameweza kumtua ndoo kichwani mama wa Bwiregi kwani vijiji vyote vimepata mradi wa maji.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda alisema kuwa Serikali imetoa fedha sh. bilioni 18.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo ambazo zimesaidia kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba madarasa.
Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo Desemba, 30, 2023 katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, kilichofanyika kwa njia ya Zoom.

Post a Comment