WANANCHI WATAKIWA KUZIELEWA SHERIA
Na Jovina Massano Musoma
WANANCHI watakiwa kuondokana na mtazamo wa zamani na kuelewa mabadiliko ya kisheria mbalimbali zitumikazo katika vyombo vya usimamizi wa haki.
Hayo yameelezwa Februari 1/2024 kilele cha siku ya sheria hapa nchini Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt.Halfan Haule alipozungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda.
Mawakili kutoka Chama cha mawakili Tanganyika
Amesema kuwa nchi inapitia mabadiliko mbalimbali na Mahakama pia, hivyo ni sahihi wananchi wakipata nafasi ya kupata mabadiliko hayo kwa kupata elimu.
"Wananchi wengi bado kwenye haki jinai wanamtazamo na uelewa wa zamani hasa kwenye makosa ambayo yanadhaminika polisi na Mahakamani
Aidha ametolea mfano wa tukio lililotokea halmashauri ya Musoma vijijini la mwananchi kumshambulia na kumjeruhi Mwalimu kupata dhamana ambapo wananchi waliandamana wakifikiri kuwa ameachiwa huru kwa kutoa hongo.
" Hawakuelewa kuwa kosa lake lilikuwa linadhaminika hivyo walifika kutoa malalamiko katika ofisi yangu kwa kuwa ilikuwa wiki ya sheria na kuna elimu zinatolewa aliwachukua hadi eneo lililotumika kutoa elimu wakaelewa na kuridhika.
Anasema utoaji wa elimu ya muhimili wa Mahakama hasa kwenye eneo la haki jinai itaisaidia jamii kuenenda nayo na kuelewa makosa yanayodhaminika na sheria zingine za nchi.
Nae mgeni rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Musoma Fahamu Mtulya amesema kuwa maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria na siku ya Sheria yalianza Mwaka 1996 nchini.
"Miaka kumi na tano ya mwanzo ilikuwa ni kusoma hotuba zenye maudhui mbalimbali na kusambaa Mahakama ikaona ni vema wiki ya Sheria iweze kuwakutanisha wananchi wahitaji na watu wa Mahakama na wadau wake nia ni kuwafikia wahitaji na kuwasaidia "anasema fahamu.
Ameeleza kuwa kwa kila mwaka kwenye wiki ya Sheria kauli mbiu hubadirika maudhui na mahitaji ya Taifa kwa wakati huo.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa,nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai.
"Ni ukweli usiopingika kauli ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendana na ukweli uliopo kuhusu mfumo wa haki jinai ucheleweshaji wa kusikiliza mashauri kwa wakati katika Mahakama kama taarifa ya tume ya haki jinai ilivyojieleza ukurasa wa 41 na 42", amesema Mtulya.
Ameseme kuwa katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Musoma haina shauri la mrundikano.
Post a Comment