KIWANDA CHA KUCHAKATA KAHAWA CHA WAMACU LTD KUKUZA UCHUMI WA WAKULIMA TARIME
Na Dinna Maningo, Tarime
WAMACU LTD ni Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima mkoa wa Mara. Dhumuni la uwepo wa chama hiki ni kuratibu na kuunganisha vyama vya msingi ambao ni wanachama kwa ajili ya kukusanya, kuhifadhi, kusindika na kutafuta masoko na kuuza mazao hayo kwenye soko lenye tija.Ni miaka kadhaa wakulima wa zao la Kahawa mkoani Mara wamekuwa wakiteseka kwa kukosa soko la uhakika la kuuza kahawa pamoja na ukosefu wa kiwanda cha kuchakata kahawa kavu na kahawa mbivu baada ya chama cha ushirika cha WAMACU LTD kusuasua na kushindwa kujiendesha.
Miche ya Kahawa
Kusuasua kwa chama hicho ukapelekea kiwanda cha kuchakata kahawa kufa ambacho kilikuwa ni tegemeo la mkulima wa kahawa kuuza kahawa yake kiwandani pamoja na kubangua zao hilo.
Hali hiyo ikasababisha kilimo cha kahawa kusuasua baada ya baadhi ya wakulima kukata tamaa na kuachana na kilimo cha kahawa kwakuwa hakikuwa na tija tena kwao.
Mwaka 2020 Chama cha WAMACU LTD kikafufuka na kuanza kutekeleza upya madhumuni yake na kuanza kuwahamasicha wakulima kulima zao la kahawa ambacho kimekuwa suluhisho kwa mkulima wa kahawa.

Wafurahia kuanzishwa kiwanda
Mnamo, Januari, 31, 2024 Chama cha WAMACU LTD kilifanya mkutano mkuu wa mwaka, uliowashirikisha wajumbe wa mkutano mkuu, viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wa zao la kahawa.
Mkutano huo ulifanyika mjini Tarime, katika kiwanda cha kahawa kilichopo mtaa wa Rebu shuleni, Kata ya Turwa uliokwenda sambamba na uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata kahawa kavu na mbivu.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda akazindua kiwanda hicho chenye mashine za kuchakata kahawa na kuwapongeza WAMACU LTD kwa kujenga kiwanda .
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda (kushoto) akizindua kiwanda cha Kahawa kinachomilikiwa na Chama Kikuu cha Wakulima Mara
Wakulima wazungumza
Wakulima wa kahawa wanaeleza namna zao hilo la kahawa lilivyozolota baada ya chama cha WAMACU LTD kusuasua, na baada ya kurejea na kuanzishwa kiwanda sasa wakulima wanalima kwa wingi zao hilo kwakuwa wana uhakika wa soko na kiwanda.
Mkazi wa Kijiji cha Matongo Kata ya Buhemba aliyeanza kilimo cha kahawa mwaka 1997 , Kikondo Maseke anasema ujio wa kiwanda ni furaha kwake .

Kikondo Maseke
"Nafurahi sana Kiwanda cha kahawa kujengwa maana kitakuza uchumi wa mkulima na upatikanaji wa soko utakuwa mkubwa kwakuwa tutauza kahawa yetu kiwandani na tutapata pesa" anasema.
Mkazi wa kijiji cha Kesangora, Kata ya Nyamwaga wilaya ya Tarime, Chacha Matiko mwanachama wa chama cha wakulima cha Mori AMCOS ( Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko), mkulima tangu mwaka 1969, anasema amesomesha watoto hadi chuo kikuu kwa kilimo cha kahawa, wengine ni watumishi wa serikali.

Mkazi wa kijiji cha Kesangora, Kata ya Nyamwaga wilaya ya Tarime, Chacha Matiko
"Hiki kiwanda kitarahisisha huduma za wakulima, wakati hakipo tulikuwa tunasafirisha kahawa ya maganda kupeleka Moshi, tunapongeza kiwanda kuanzishwa Tarime kwasababu Tarime uzalishaji wa kahawa ni mkubwa kuliko wilaya zingine" anasema Chacha.
Emmanuel Ndege ni Mkazi wa kijiji cha Ingli juu, Kata ya Mirare, wilaya ya Rorya, ni Mwenyekiti wa Mirare AMCOS na mjumbe wa bodi ya WAMACU, anasema baada ya WAMACU kurejea msimu wa kilimo uliopita kikundi chao chenye watu 80 kilivuna kilo 300 kwa mwaka 2022/2023.

Mkulima Kijiji cha Ingli juu Emmanuel Ndege
Anaishauri WAMACU kuongeza kasi ya ugawaji miche kwani itasaidia kuongezeka kwa mashamba lakini pia, wakulima wapatiwe elimu ya upandaji miche.
Mkazi wa kijiji cha Byatika, kata ya Buhemba wilayani Butiama, Wegesa Chacha ni Mwanachama na Katibu wa chama cha msingi cha Shadabi anasema baada ya WAMACU kufufuka walianza kilimo cha kahawa, hadi sasa kikundi kimekusanya tani 3 za kahawa.
Mwenyekiti wa ushirika wa Shadabi Kulwa Nyamhanga, anasema kuanzishwa kwa kiwanda wakulima watajipatia kipato, watalipwa pesa tasilimu, watatumia vipimo halali, fursa za ajira, wakulima wataunganishwa na kupata masoko kwa urahisi.
Anaishauri WAMACU kuongeza kasi ya ugawaji miche kwani itasaidia kuongezeka kwa mashamba lakini pia, wakulima wapatiwe elimu ya upandaji miche.
Mkazi wa kijiji cha Byatika, kata ya Buhemba wilayani Butiama, Wegesa Chacha ni Mwanachama na Katibu wa chama cha msingi cha Shadabi anasema baada ya WAMACU kufufuka walianza kilimo cha kahawa, hadi sasa kikundi kimekusanya tani 3 za kahawa.
Mkulima kijiji cha Byatika Wegesa Chacha
"Mwaka huu nimepanda miche 250 ambayo kikundi tuligawiwa watu wapatao 20. Hiki kiwanda kitatusaidia sana maana kipo karibu wakulima tutajitahidi kuwa na mashamba makubwa ya kahawa" anasema Wegesa.
Mwenyekiti wa ushirika wa Shadabi Kulwa Nyamhanga
"Tulianza kuuza kwa bei ya Tsh. 1200 iliyokuwa inasimamiwa na WAMACU na mwaka 2022 bei ilipanda hadi 2300 na sasa bei imeongezeka hadi sh.2600 kwa kilo " anasema Nyamhanga.
Katibu wa mbunge Jimbo la Tarime mjini, Elias Samo anawaomba wananchi wa jimbo la Tarime mjini hasa vijana kujiunga na kilimo cha kahawa kwani wakivuna watauza kahawa kiwandani.

Meneja WAMACU LTD aeleza
Akosoma Risala mbele ya mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda , Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (WAMACU LTD), Samwel Gisiboye anasema ushirika huo ni miongoni mwa vyama 46, uliosajiliwa Desemba, 24, 2008 kwa namba ya 5573.
Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (WAMACU LTD), Samwel Gisiboye akisoma risala.
Anasema ushirika unaunganisha wakulima wanaojishughulisha na uzalishaji wa mazao ya kahawa na tumbaku katika wilaya ya Tarime, Rorya, Serengeti, Butiama na Buchosa.
" Chama kina miliki rasilimali mbalimbali zikiwemo ardhi, majengo, maghara na mitmbo yenye thamani ya sh. 4, 223, 535, 447.50. Chama kina wajumbe wa bodi 7, na watumishi wapatao 35, wenye mikataba ya ajira na vibarua 60 " anasema Gisiboye.
Anasema katika msimu wa 2020/2021, chama kilikusanya kilo 282,517, kwa msimu wa 2021/2022 kilikusanya kilo 171,481, msimu wa 2022/2023 kilikusanya kilo 337,821 na katika msimu wa 2023/2024 kimekusanya kilo 606,236 ambapo katika msimu huu kahawa imekusanywa kwa bei ya sh. 2,500.
Anasema katika msimu wa 2023/ 2024 ukoboaji wa kahawa ya maganda umefanyika kwa awamu mbili kupitia kiwanda cha WAMACU ambapo wamekoboa kilo 320,364 na kupatikana kilo 151, 501 za kahawa safi sawa na uwiano wa asilimia 50.

Kahawa
Anasema msimu wa 2023/2024 chama kupitia soko la moja kwa moja kimeshauza kahawa kilo 229,560 kwa thamani ya USD Dolla 565,104 na kilo 19,980 zimeuzwa kwa thamani ya sh.117,682, 200.
"Tumeweza kuuza chenga kilo 57,907 kwa wastani wa bei ya sh.3,993.5 kwa kilo, hivyo mauzo yote kufikia sh. 1,417,852,700 kabla ya makato ya bodi ya kahawa (Exportfee-1% na Coffee Development fund -200/kg " anasema Gisiboye.
Mafaniko ya WAMACU LTD
Meneja huyo anataja mafanikio ya Chama hicho kuwa ni pamoja na ushirikiano wa benki ya kilimo (TADB) na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) wameweza kugawa miche bora ya kahawa 100,000 yenye thamani ya Tsh. 120,000,000 kwa lengo la kuongeza uzalishaji.

Kiwanda cha kuchakata kahawa kavu na mbivu
"Chama kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) na Shirika la ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika (COASCO), kimeweza kutoa mafunzo kwa viongozi na watendaji wapatao 207 wa vyama vya msingi na ushirika katika mkoa kwa kiasi cha Tsh.19,000,000" anasema.
Anasema katika msimu wa 2021/2022 chama kiliweza kulipa wakulima malipo ya pili Tsh.34, 296, 200 na msimu wa 2020/2021 kimeweza kulipa sh.113,000,000.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda
(Kulia) Akipanda mti, kushoto ni Meneja WAMACU LTD Samwel Gisiboye
Anazitaja changamoto zinazokikumba chama kuwa ni baadhi ya maeneo ya chama na vyama wanachama kuvamiwa na watu binafsi na taasisi hivyo kupelekea migogoro ya mara kwa mara inayodumaza maendeleo katika sekta ya ushirika katika mkoa huo.
Pia, uwepo wa uzalishaji mdogo wa kahawa usiokidhi mahitaji ya kiwanda na kwamba mkakati ni kuendelea kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwekeza katika uzalishaji na usambazaji wa miche bora ya kahawa.
Mwenyekiti wa WAMACU mkoa wa Mara David Hechei anasema chama kina miaka 3 tangu kianze kufanya kazi japo huko nyuma kilikuwepo lakini kilisuasua, kilinza tena wakati wa uongozi wa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima na aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Tarime Mtemi Msafiri.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa mkoa wa Mara (WAMACU LTD) David Hechei
Viongozi wa Serikali wazungumza
Mkuu wa wilaya ya Tarime aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama hicho, Kanali Michael Mntenjele anawaagiza wataalam wa kilimo kushirikiana na chama hicho.
Anakitaka chama cha WAMACU kusimamia vyema zoezi la usambazaji wa pembejeo ili ziwafikie walengwa kwa makusudi tarajiwa.

Mkuu wa wilaya ya Butiama Mwl. Moses Kaegele, anasema serikali imekuwa ikiwekeza kwa wakulima ikiwemo kuwapatia mikopo na utoaji wa ruzuku, hivyo ni vyema wataalam wawafikie wananchi kuwapa elimu ili waweze kujiunga na kilimo cha kahawa.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda anakipongeza chama cha WAMACU kwa kuunganisha wakulima wa kahawa na kuthubutu kuanzisha kiwanda kitakachoongeza thamani ya kahawa ili kuwa na bei nzuri sokoni na kumuongezea thamani mkulima.
Mkuu wa mkoa wa Mara said Mtanda akizungumza
" Kiwanda tumekikagua ni kizuri sana na bado ipo nafasi ya kutosha ya kufunga mitambo mingine, kwahiyo ni matarajio yangu kuona kiwanda kinasimama vyema, muongeze uzalishaji huu uliopo hautoshi na unachangiwa na wakulima kuendelea kutumia mbegu zisizo bora " anasema Mtanda.
Mtanda anawaagiza viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanathaminisha ardhi na mali zote za vyama.

Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda akisalimiana na Meneja wa WAMACU LTD Samwel Gisiboye pamoja na wanachama wa kahawa na wadau wa kilimo hicho
Anasema wanapaswa kufanya hivyo ili kuondoa changamoto ya maeneo ya vyama yaliyovamiwa na baadhi ya taasisi na watu binafsi wenye nia ya kurudisha nyuma maendeleo ya sekta ya ushirika.
Mwezi Oktoba, 2023 Kahawa ya Tarime iliibuka na kuwa mshindi wa pili kitaifa kwa ubora ikitanguliwa na kahawa ya Arusha shindano lililoendeshwa na bodi ya kahawa Tanzania (TCB).
Post a Comment