HEADER AD

HEADER AD

MIKOA, HALMASHAURI ZISIZO NA MAAFISA HABARI ZATAKIWA KUAJIRI

Na Mwandishi Wetu , Arusha

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Kakele amesema wizara inatekeleza kutangaza sera, kanuni na taratibu ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambapo kazi za serikali kwa umma zinafanyika kupitia mitandao ya kijamii, radio na luninga.

Akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) jijini Arusha, Selestine ametoa rai kwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya ambao mikoa yao , hslmashauri au wilaya haina maofisa habari wafanye hima kuajiri maofisa habari.

     Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Selestine Kakele akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari, 2024.

Amesema kuwa kukosekana kwa maafisa habari kwa baadhi ya mikoa na wilaya kunawakosesha wananchi haki ya kupata habari na kufahamu yanayofanywa na serikali yao huku baadhi ya taasisi za  mawasiliano kwa umma hazitekelezi majukumu yake.

Ameongeza kuwa mikoa 14 imepata fursa ya kutangaza miradi mbalimbali ya serikali huku zoezi hilo likiwa linaendelea ikiwemo uwekaji misingi ya uhuru wa vyombo vya habari sanjari na kushamiri kwa idadi kubwa ya vyombo vya habari ikiweo magazeti , radio na televisheni za mitandao, blogu .

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema baadhi ya halmshauri hazina maafisa mawasiliano wa serikali badala yake maofisa Tehama ndio wanaongoza kitengo hicho jambo linalokwamisha hali ya wananchi kupata habari.

     Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari,2024

"Halmashauri 180 zilizopo nchini lakini inashangaza kuona baadhi yao siwezi kutaja idadi hazina maafisa habari na hawajui maana ya habari na ukiuliza sababu gani hakuna maafisa habari unajibiwa majibu yasiyoridhisha" amesema.

" Lakini pia kwenu maafisa mawasiliano ya serikali wapeni nafasi wananchi nao wazungumze kuhusu mambo mbalimbimbali yanayowasibu ila pia ni lazima sasa halmashauri ziajiri maafisa habari ili waweze kusemea vema serikali na wananchi kupata habari zaidi.

Wakati huohuo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo , Dk.Damas Ndimbaro amewaagiza Maafa Habari Serikalini kutangaza miradi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili wananchi wajue ikiwemo kujibu hoja za uongo zinazotolewa na watu dhidi ya serikali .

   Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Damas Ndumbaro akizungumza na maafisa Mawasiliano Serikalini wakati wa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari,2024

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko, amesema maofisa hao wanawajibu mkubwa wa kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili watu waone ukubwa wa kazi zinazofanywa na serikali nchini.

   Baadhi ya Washiriki wa Mkutano mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia majadiliano

"Baadhi ya watu hawaoni ukubwa wa katarasi nyeupe ulivyo sasa ni wajibu wenu kueleza kazi zinazofanywa na serikali ikiwemo kujibu hoja za uongo dhidi ya serikali lazima mjue kujibu fitna na zengwe"

" Hata serikali inapigwa fitna sasa ni kazi yenu kujibu fitna na zengwe kwani hivi sasa zama za teknolojia ya habari imekua na ni nzuri ila inachangamoto zake kupitia mitandao ya kijamii.


Amesema moja kati ya changamoto kubwa iliyoletwa na mitandao ya kijamii haijui ni nani mtoa habari na nani anayepaswa kujua hii ni habari hivyo amewataka kutumia changomoto hizo kwaajili ya kujibu hoja na lazima mafunzo ya mara kwa mara yatolewe ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

Ametoa rai kwa Waandishi wa habari vyombo vya  serikali na maafisa habari  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uzalendo, weledi na ubunifu pale taarifa zinavyoandikwa.



Ametoa maelekezo kwa waaajiri wote wasioweza kuleta maafisa habari kushiriki mkutano huo watoe maelezo kimaandishi na ifikapo mwakani maafisa wote wa serikali na wasio wa serikali wajiunge na chama hicho.

Amesema treni ya majaribio ya umeme imeanza kazi kwa majaribio ingawa kulikuwa na kebehi nyingi sana lakini treni imeshaanza kazi hivyo serikali inafanya kazi kwa vitendo.

Amewasihi maafisa hao kujiunga kwa pamoja kutetea serikali pale jambo linapotokea badala ya kuachia wizara husika pekee kutoa ufafanuzi ikiwemo kutoa hamasa kwa wananchi kujua umuhimu wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwemo utangazaji wa miradi ya kimkakati ya serikali.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Joshua Nassari amesema ushirikoshwaji wa maofisa mawasiliano ni chachu ya kutoa taarifa kwa umma na kuongeza kuwa wamepokea agizo la kila halmashauri kuwa na maofisa habari na mikoa kwa ujumla.

Awali Kaimu Mwenyekiti wa TAGCO,   Karim Meshack amesema chama hicho kitaendelea kuhakikisha kinawunganisha maafisa habari kujadili mambo mbalimbali sanjari na kujifunza mbinu mbalimbali za teknolojia za upashanaji habari.

     Msimamizi wa Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa TAGCO Bw. Bakari Machumu ambaye ni Mkurugenzi wa Mwananchi Communication akiteta jambo na Anastazia Rugabwa – Mkurugenzi wa Ushawishi na Ushirikishwaji kutoka Twaweza East Afrika wakati wa majadiliano.

No comments