RATIBA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYA YA MUSOMA
Na DIMA Online, Mara
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa yupo mkoani Mara kwa ziara ya kikazi Februari, 25-29, 2024 ambapo atatembelea na kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi pamoja na kuongea na watendaji wa serikali pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Waziri mkuu atafanya ziara wilaya ya Musoma Februari, 29, 2024.
Majira ya saa 2:30-4:00 msafara utaelekea Suguti wilaya ya Musoma, 4:00-4:30 Waziri mkuu atakagua na kuweka jiwe la msingi jengo la utawala halmashauri ya wilaya ya Musoma, 4:30-5:30 kikao cha ndani na Madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Musoma.
Saa 5:30-6:00 msafara utaelekea Kijiji cha Bwai, 6:00-7:00 Waziri mkuu atakuwa na mkutano wa hadhara Kijiji cha Bwai, 7:00-7:40 msafara utaelekea Manispaa ya Musoma kwenye eneo la mkutano wa hadhara, 8:00-10:00 atazungumza na wananchi na hivyo kuhitimisha ziara yake mkoani Mara.
Post a Comment