MURIBA SEC. HAINA MWALIMU WA SOMO LA KINGEREZA, WANAFUNZI WAKAA CHINI
Na Dinna Maningo, Tarime
SHULE ya Sekondari Muriba Kata ya Muriba, katika halmashauri ya wilaya ya Tarime, mkoani Mara haina mwalimu wa somo la kingereza huku wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili wakisoma wakiwa wamekaa chini.
Hayo yamebainika Januari, 4, 2024 baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara, Julius Kambarage Masubo akiwa ameongozana na viongozi wa chama hicho wilaya ya Tarime, kufika katika kijiji cha Muriba kuadhimisha miaka 47 ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara, Julius Kambarage Masubo
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi amesema ameshangaa kubaini kutokuwepo mwalimu wa somo la kingereza shule ya sekondari Muriba huku shule hiyo ikiwa haina viti na meza katika madarasa ya kidato cha kwanza na cha pili.
" Nimeshangaa eti shule haina mwalimu wa somo la kingereza. Hii shule imefanya vizuri matokeo ya kidato cha nne ina Division two zipatazo 11, hongera mwalimu mkuu wa shule mwanamke unachapa kazi.
"Pia wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili wanakaa chini, ngoja nimtafute kwa simu afisa elimu Babukege kwanini shule haina mwalimu wa somo la kingereza na kwanini watoto wanakaa chini?" amehoji.
Mwenyekiti huyo alimpigia simu afisa elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Tarime, Venance Babukege lakini simu hiyo iliita bila kupokelewa.

Viongozi wa CCM
Mwenyekiti huyo akiwa anaendelea kuzungumza na wananchi na wanaccm baada ya dakika kadhaa kupita, afisa elimu alimpigia simu na kisha mwenyekiti amehoji;
" .....Afisa Elimu niko hapa shuleni Muriba kwanini shule haina mwalimu wa somo la kingereza? na kwanini wanafunzi wanakaa chini?" amehoji.
Afisa Elimu alijibu "....Ni kweli shule haina mwalimu wa somo la kingereza, tuna upungufu wa walimu 239 na si shule hiyo tu shule sita hazina mwalimu wa somo la kingereza na pia walimu wa kiswahili"amesema Babukege.

Baadhi ya Wanachama wa CCM wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM
Amesema kuwa, mwaka jana waliajiriwa walimu wa sanaa wawili pekee " wameajiriwa wawili mmoja wa somo la kingereza na mwingine wa Literature. Ajira ya Serikali tunaajiri walimu wa baiolojia, fizikia,Hisabati, na Kemia, kuna upungufu mkubwa wa walimu wa sanaa"amesema.
Afisa Elimu ameongeza kusema " Kuna walimu wa masomo ya sanaa walipelekwa kufundisha shule za msingi kama yupo tukimpata kwenye hiyo kata tutamwajiri, nimepata mmoja kata ya Nyarero atarudishwa kufundisha shule ya sekondari hapo hapo Nyarero" amesema Babukege.
Akijibu kwanini wanafunzi wanakaa chini amesema halmashauri inakabiliwa na upungufu wa madawati 9,100 ambao umesababisha uhaba kwa shule zote kidato cha kwanza hadi cha sita.
Afisa huyo wa elimu amesema kwamba tayari wameshaweka kwenye mpango wa fedha za uwajibikaji wa kampuni kwa Jamii (CSR) fedha kutoka Mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara ambapo shule hiyo ni miongoni mwa shule zitakazotapata madawati.
Mwenyekiti Masubo ameitaka Serikali ya wilaya ya Tarime na halmashauri hiyo kutatua changamoto za shule kwa kile alichosema kuwa mapungufu yanachangia wanafunzi kufeli mitihani.
Post a Comment