RATIBA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI BUNDA
Na DIMA Online, Mara
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa atakuwa mkoani Mara kwa ziara ya kikazi Februari, 25-29, 2024 ambapo atatembelea na kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi pamoja na kuongea na watendaji wa serikali pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Waziri mkuu atafanya ziara wilaya ya Bunda Februari, 26, 2024 ambapo saa 2:00-3 :00 asubuhi msafara utaelekea Kijiji cha Mariwanda Bunda, saa 3:00-3:40 Waziri mkuu atasalimia wananchi kijiji ch Mariwanda.
Msafara utaelekea shule ya msingi Sabasita (Bunda) 3:40-4:00, saa 4:00-4:30 Waziri Mkuu atatembelea na kukagua shule ya msingi Sabita. Saa 4:30-5:10 msafara utaelekea shule ya sekondari ya wasichana Mara, 5:10-6:10 mchana atakagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Mara.
Msafara utaelekea eneo la mradi wa maji Sazira Bunda mjini 6:10-6:40, saa 6:40-7:10 waziri mkuu atazindua mradi wa maji Kata ya Sazira Bunda mjini, 7:10-7:30 msafara utaelekea ukumbi wa mkutano Bunda mjini.
Waziri mkuu atakuwa na mkutano na Madiwani na watumishi wa wilaya ya Bunda 7:30-9:00, 9:00-9:20 alasiri msafara utaelekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara.
Saa 9:20-11:20 Waziri mkuu atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara shule ya msingi Miembeni na hivyo kuhitimisha ziara yake wilayani Bunda na kuendelea na ziara katika wilaya zingine mkoani Mara.
Post a Comment