RATIBA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI BUTIAMA, SERENGETI, TARIME
Na DIMA Online, Mara
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa yupo mkoani Mara kwa ziara ya kikazi Februari, 25-29, 2024 ambapo atatembelea na kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi pamoja na kuongea na watumishi wa serikali pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Waziri mkuu atafanya ziara wilaya ya Butiama, Serengeti na Tarime Februari, 27, 2024.
Majira ya saa 1:00-1:30 asubuhi msafara utaelekea katika eneo la ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Butiama, 1:30-2:00 Waziri mkuu atakagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi ofisi ya mkuu wa wilaya, 2:00-2:10 msafara utaelekea ukumbi wa mkutano na watumishi.
Waziri mkuu atazungumza na madiwani na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Butiama 2:10-3:10, Saa 3:10- 3:40 atasalimia wananchi na msafara kuelekea Mwitongo kwa baba wa Taifa.
Waziri mkuu atasalimia familia na kuzuru kaburi la baba wa Taifa 3:40-4:10, saa 4:10-5:30 msafara utaelekea Mugumu Serengeti, 5:30-6:30 atakuwa na mkutano na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti.
Saa 6:50-8:00 mchana atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uwanja wa Sokoine-Mugumu, 8:00 -8:45 msafara utaelekea Kijiji cha Getarungu, 8:45-9:20 atakagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Zahanati ya Getarungu.
Msafara utaelekea Nyamwaga wilayani Tarime 9:20-10:00 alasiri, saa 10:00-11:00 jioni ataweka jiwe la msingi jengo la utawala halmashauri ya wilaya ya Tarime na kusalimia wananchi ambapo Februari 28 ataendelea na ziara yake wilayani Rorya na Tarime.
Post a Comment