WAJUE WALIOTUNUKIWA VYETI VYA PONGEZI KWA USHIRIKIANO NA DIMA ONLINE
>>> Wamo Waandishi wa Habari, Wananchi, Viongozi, Taasisi, Wizara
Na DIMA Online, Tarime
KATIKA kutambua mchango wa Waandishi wa habari wanaoripoti habari Katika chombo cha Habari cha DIMA ONLINE Blog, Uongozi wa DIMA ONLINE hivi Karibuni uliwatunuku vyeti vya pongezi badhi ya Waandishi wa habari kwa uwajibikaji wao tangu kuanzishwa kwa Blog Septemba, 21,2022 hadi Septemba, 20, 2023.
Waandishi wa habari 10 wanaripoti habari kutoka baadhi ya mikoa nchini. Hata hivyo Uongozi wa DIMA ONLINE umewatunuku baadhi yao ambao wameonekana kuripoti habari nyingi zaidi na wawajibikaji kazini tangu walipoanza kuripotia chombo hiki cha habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa DIMA Online, Rose Joseph Kimaro amesema kuwa uongozi wa DIMA Online unatambua mchango wa kihabari wa Waandishi wa habari wote wa DIMA Online kwani kupitia wao wananchi wameweza kupata habari mbalimbali.
" Waandishi wote wanafanya kazi vizuri, tunatambua na kuthamini jitihada zao katika kuhabarisha umma kupitia DIMA. Tumewatunuku vyeti Waandishi wa habari wanne kati ya 10 ambao wameonekana kufanya vizuri zaidi na uwajibikaji mzuri.
"Tunawashukuru wote pia tunawaomba waendelee kuisaidia DIMA katika kuripoti habari na kila mwaka tutakuwa tunatoa vyeti vya pongezi kwa Waandishi waliofanya vizuri pamoja na Taasisi, Viongozi,Wafanyabiashara, Wizara na Wananchi n.k wanaotoa ushirikiano wa kihabari, tunafanya hivyo kama shukrani na pongezi kwao" amesema Rose.
Pia Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Siasa, Wizara, Wafanyabiashara, Taasisi na wananchi, wametunukiwa vyeti vya pongezi kwa ushirikiano wao wa kihabari pamoja na ushiriki wao Katika huduma za kijamii kwa wananchi.
Waandishi wa habari waliotunukiwa vyeti vya pongezi waliowajibika vyema Kwa kipindi cha mwezi Septemba, 21 hadi Septemba, 20,2023 ni ANDREW RAMADHANI CHARLE - Mwandishi WA habari kutoka Mkoa wa Dar es Salaam aliyetunukiwa cheti kuwa Mwandishi bora wa habari za Burudani na Utamaduni.
Charle ameongoza kwa kuripoti habari za Michezo na burudani zipatazo 30, huku waandishi wengine wa habari wakiripoti habari za burudani zisizozidi 5.
Uongozi wa DIMA ONLINE umemtunuku cheti cha pongezi JOVINA JOHN MASSANO kuwa Mwandishi bora msikivu na anayezingatia maelekezo katika kazi zake za uandishi wa Habari.
Jovina Mwandishi wa habari kutoka Musoma amekuwa ni msikivu pindi anapopewa maelekezo katika stori zake kama vile kusahihisha makosa, ufafanuzi unaojitokeza pindi mhariri anapohariri habari zake.
Uongozi wa DIMA ONLINE umemtunuku cheti cha pongezi SAMWEL LOTH MWANGA kuwa Mwandishi bora anayejituma kazini.
Samwel Mwandishi wa Habari kutoka mkoa wa Simiyu amekuwa akijitahidi kutuma habari kwa wakati stori zake siyo viporo anapokwenda eneo la tukio hutuma habari bila kulaza kazi. Na ukimpa maelekezo ya kazi utekeleza kwa wakati.
Uongozi wa DIMA ONLINE umemtunuku cheti cha pongezi DINNA STEPHANO MANINGO kuwa Mwandishi bora wa habari za Kijamii, Makala, Habari za Uchunguzi pamoja na kuongoza kwa kuandika habari nyingi zaidi.
Kwa Kipindi cha mwaka mmoja Dinna anaongoza kwa kuandika habari nyingi zilizopostiwa DIMA ONLINE zipatazo 131, akifuatiwa na Andrew Charle aliyeripoti habari 58 huku Jovina akirupoti habari 51 na waandishi wengine wakiripoti idadi isiyozidi habari 35.
Uongozi wa DIMA Online umewatunuku vyeti vya pongezi Kwa ushirikiano na uwajibikaji Kwa jamii Viongozi, Wafanyabiashara, Taasisi, Wizara na Wananchi ambao ni
Uongozi wa DIMA Online umeitunuku cheti cha pongezi OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) kwa uwajibikaji ulioleta mafanikio kwa jamii baada ya habari kuripotiwa DIMA Online.
Mafanikio hayo yanatokana na TAMISEMI kufuatilia kwa ukaribu habari zinazopostiwa na hivyo kufanya uwajibikaji ambao umeleta mabadiliko kwa jamii yatokanayo na habari zilizoandikwa kwenye chombo hiki cha habari.
Mf. Shule ya msingi Magufuli yenye wanafunzi wa mahitaji Maalum ilisajili wanafunzi wasioona tangu mwaka 2019 lakini haikuwa na vitabu vya nukta nundu kwa ajili ya wanafunzi wasioona lakini baada ya habari kuripotiwa DIMA Online mwanzoni mwa mwaka 2023 Serikali ya awamu ya sita imepeleka vitabu vya kutosha vya nukuta nundu.
Serikali ilipeleka Milioni 75 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu na matundu ya choo katika shule ya msingi Kamimange iliyopo Kata ya Mirwa wilaya ya Butiama, madarasa yakajengwa ambapo shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 2000 ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa baada ya habari kuripotiwa fedha zikapelekwa shuleni kujenga madarasa.
DIMA Online illiripoti malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Magunga wakilalamika Kamati ya shule na Uongozi wa Kijiji na Kata kuwataka kuchanga fedha kujenga madarasa ambayo Serikali ilikwishatoa fedha za ujenzi.
Baada ya habari kuripotiwa Serikali ilizuia wananchi kuchangishwa fedha za ujenzi wa madarasa ambavyo Serikali ilikuwa tayari imetoa fedha za uje
Serikali kupiga marufuku Ng'ombe wenye mimba kuchinjwa machinjioni Kijiji cha Magunga. Ni baada ya DIMA ONLINE kushuhudia machinjioni ndama wakiwa wamekufa na kutupwa baada ya ng'ombe wenye mimba kuchijwa.
Zahanati ya Bukenye Kata ya Manga- Tarime iliyosota kwa miaka kadhaa bila kukamilika, baada ya habari kuripotiwa ujenzi ulikamilika sasa wananchi wanapata huduma ya afya.
Shule ya Bukenye Sekondari kuweka bendera ya Taifa na kibao cha shule, Ni baada DIMA kuripoti shule hiyo kutokuwa na Bendera na Kibao cha shule kinyume na waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka 2000 utundikaji na upeperushaji wa bendera ya Taifa. Walaka unataka Bendera ya Taifa itundikwe kwenye Majengo yote ya Serikali na Taasisi zake ikiwa ni pamoja na Serikali za Mitaa.
Uongozi wa DIMA Online umeitunuku cheti cha pongezi WIZARA YA AFYA kupitia maafisa habari wa Wizara kwa ushirikiano wa habari ambapo habari zipatazo 50 zimepostiwa DIMA ONLINE na maafisa habari wa Wizara ya Afya.
Uongozi wa DIMA Online umeitunuku cheti cha pongezi MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA kwa uwajibikaji katika utoaji elimu ya sheria kwa wananchi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (wa kulia) akipokea cheti cha pongezi kutoka Mwandishi wa Habari kutoka blogu ya DIMA Online Joviana Masano (wa pili kushoto) kwa niamba ya Uongozi wa DIMA Online, wengine ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya (wa kwanza kulia) pamoja na Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma Mhe. Erick Marley.
Wananchi Kata ya Mwisenge- Musoma kupitia DIMA Online waliiomba Mahakama Kuu ya Kanda ya Musoma kuwapatia elimu ya sheria.
Mahakama kuu kupitia Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ilitoa elimu ya sheria kwa wananchi wa Mwisenge.
Pia Wajasiliamali wapatao zaidi ya 200 na Waandishi wa habari wanawake wakiwa kwenye kongamano la kikundi cha Waandishi wa habari wanawake wenye maoni mkoani Mara, lililofanyika viwanja vya Mukendo -Musoma walipata elimu ya sheria kuhusu maswala ya Ndoa, Talaka na Mirathi iliyotolewa na Mahakimu, Naibu msajili wa Mahakama hiyo.
Uongozi wa DIMA Online umeitunuku cheti cha pongezi KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA TARIME ikiongizwa na Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Michael Mntenjele kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa Waandishi wa Habari.
Waandishi wa Habari wanapokumbwa na changamoto za kiusalama wanapokuwa walitekeleza majukumu yao Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tarime imekuwa mstali wa mbele kuhakikisha Waandishi wa Habari wanalindwa na kuwa salama.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi PROF. MARTINI MHANDO kwa ushirikiano wake na DIMA Online ,akiwa kama Mtendaji mkuu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) amekuwa na ushirikiano na chombo hiki cha habari kuhakikisha jamii inapata burudani kupitia Matamasha ya Filamu.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi ENG. CHARLES NESTORY kwa ushirikiano wake na DIMA Online ,akiwa kama Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) kwa ushirikiano wa habari za Miundombinu ya barabara, amekuwa akitoa ushirikiano wa karibu pindi DIMA ONLINE inapowasiliana nae kupata taarifa kuhusu ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi ESTER CHARLES MWERA ambaye ni Mwenyekiti wa NGOME ya Wanawake wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Mara kwa ushirikiano wa habari na DIMA Online. Amekuwa akitoa ushirikiano wa taarifa juu ya changamoto mbalimbali za kijamii.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi JULIUS JOHANNES MWITA ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Turwa, wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ushirikiano wa habari na waandishi wa habari.
Amekuwa mfuatiliaji wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kushirikisha waandishi wa habari ambapo baadhi ya habari zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari ikiwemo DIMA zimezaa matunda na hatua zimechukuliwa.
Mfano ujenzi wa shule ya msingi Rebu, miradi ya ujenzi inayobainika kuleta utata katika ujenzi kikiwemo kisima cha asili mtaa wa Rebu Senta Serikali ilichukua hatua na changamoto za ujenzi zikatatuliwa.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi MWL. MEKAUS MAINGU akiwa kama Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa ushirikiano wa habari ulioleta matunda ikiwemo shule ya msingi Magufuli iliyokuwa na changamoto ya ukosefu wa vitabu vya nukta nundu na baada ya ushirikiano wake wa kihabari serikali ilitoa vitabu vya nukta nundu katika shule hiyo.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi SAMWEL ITINDE MSETI ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Manga, wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ushirikiano wa habari na DIMA Online .
Amekuwa mfuatiliaji wa changamoto za wananchi na hivyo ufatiliaji wake kuleta mafanikio kupitia habari zinazoripotiwa. Mfano ni ni ziara yake ya kushtukiza katika shule ya sekondari Bukenye na Zahanati iliyochelewa kuanza kutoa huduma ambapo kwa sasa inatoa huduma.
Upungufu wa Samini za shule, baadhi zilinunuliwa. Bendera ya Taifa na kibao cha shule ambavyo awali havikuwepo sasa vipo vimewekwa n.k
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi JOSEPHAT ELIAS HARUN ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha mjini Kati - Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ushirikiano wa habari na DIMA Online .
Amekuwa akionyesha ushirikiano wa dhati katika kushea link za habari za DIMA Online kwenye makundi ya Whatsapp kwa gharama zake za vifurushi vya MB pamoja na ushirikiano wa habari mbalimbali.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi JOHNAS CHACHA MAGWE ambaye ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tawi la Nyabichune- Nyamongo kwa ushirikiano wa taarifa zinazogusa jamii zikiwemo changamoto mbalimbali.
Amekuwa na ushirikiano na kujituma katika ufatiliaji wa taarifa kwa kushirikiana na Waandishi wa DIMA.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi CHACHA HECHE kwa ushirikiano wa habari na DIMA Online. Amekuwa na ushirikiano kwa waandishi wa Habari katika taarifa mbalimbali zinazotokea ndani ya jamii.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi mfanyabiashara ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ujenzi ya RIN CO. LTD, ISACK CHARLE RANGE mkazi wa Kijiji cha Nyangoto- Nyamongo Wilaya ya Tarime mkoa wa Mara kwa ushirikiano wake katika kuchangia maendeleo sekta ya elimu katika shule za Serikali.
Ni mwananchi mzawa amekuwa alijitahidi kuchangia fedha kutekeleza miradi ya ujenzi Sekta ya elimu kwa shule za Serikali pamoja na michango mbalimbali kwa jamii.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi KIBIBA MACHAGE ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PKM, mkazi wa Kijiji cha Mjini Kati-Nyamongo Wilaya ya Tarime kwa ushirikiano wake katika kuchangia huduma za Kijamii.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi LAMECK AIRO mkazi wa Kijiji cha Utegi Kata ya Koryo Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ushirikiano wake katika kuchangia huduma za kijamii.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi JOYCE SOKOMBI Mkazi wa Mtaa wa Kwanga B wilaya ya Musoma mkoani Mara kwa ukubali wake kuwa mlezi wa Kikundi cha Waandishi wa habari Wanawake wenye maono Mkoa wa Mara na mchango wake wa kifedha kuendesha ofisi ya kikundi.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi TEREZIA CHACHA MARWA ambaye ni Mkulima mkazi wa Kitingoji cha Kegonga B Kijiji cha Matongo- Nyamongo kwa kujituma Katika Kilimo.
Terezia ni mjane aliyefiwa mmewe na kumwacha na watoto wadogo ambao amewakuza na kuwalea kwa kutegemea kilimo ambacho anakitegemea katika Maisha yake yote.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi Mjasiriamali BHOKE BWISO kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa DIMA ONLINE uliofanyika Oktoba, 8, 2023.
Uongozi wa DIMA Online umemtunuku cheti cha pongezi Mjasiriamali BHOKE BWISO kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa DIMA ONLINE uliofanyika Oktoba, 8, 2023.
Baadhi ya Vyeti vimeshawafikia wahusika na vingine juhudi za kuhakikisha vinawafikia zinaendelea. Uongozi wa DIMA Online Unawashuru na kuwapongeza Viongozi, Wafanyabiashara, Wakulima, wafugaji, Taasisi, Wizara, wananchi kwa ujumla na wasomaji wote wa DIMA Online kwa ushirikiano wao.
Mwandishi wa Habari Samwel Mwanga ameupongeza uongozi wa DIMA Online kwa kutambua mchango wake.
"Awali ya yote niupongeze uongozi wa DIMA ONLINE kwa kutambua mchango wangu nikiwa Mwandishi wa habari ambaye natuma habari zangu mbalimbali kwenye chombo hicho cha habari.
"Kupewa cheti cha pongezi ni ishara tosha uongozi wa DIMA Online unawathamini wadau wake mbalimbali ambao wanatumia chombo hicho na hii ni motisha chanya kwangu ya uandishi wa habari na kunifanya binafsi kufanya kazi kwa bidii na maarifa na ubunifu mkubwa ili kuendana na hali ya teknolojia ya habari ambayo kila siku inakuja" amesema Samwel.
DIMA Online inawaomba kuendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha jamii inatoa na kupata habari kwa wakati ili kuendelea kutekeleza haki ya uhuru wa mawazo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18 inayosisitiza haki na uhuru wa mtu kutoa maoni yake, kutafuta na kupata taarifa.
Imetolewa na Uongozi wa DIMA ONLINE.
Post a Comment