AIRO ASEMA SANGO KASERA NI KIONGOZI ANAWAJIBU WA KUSAIDIA MAENDELEO YA WANANCHI
>> Airo akabidhi madawati 40 Kata ya Nyathorogo yaliyotolewa na Sango
Na Dinna Maingo, Rorya
MJUMBE wa Mkutano Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sango Kasera Gungu ametoa msaada wa madawati 40 kwa ajili ya shule za msingi zilizopo Kata ya Nyathorogo wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Pia aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo ameahidi kununua mashine kubwa ya kuchapa mitihani itakayotumiwa na shule zote za msingi katika kata hiyo pamoja na jezi za michezo.
Lameck Airo akizungumza wakati akikabidhi madawati
Akikabidhi madawati hayo katika Kata hiyo kwa niaba ya Sango Kasera, amesema kuwa hawamfanyii Sango kampeni bali ametoa madawati hayo kama kiongozi wa chama anayepaswa kuwasaidia wananchi pindi wanapohitaji msaada.
"Kazi yetu kubwa tumekuja kutoa msaada wa madawati 40 yaliyotolewa na mdau wa maendeleo Sango Kasera, hajafika hapa yupo kwenye majukumu mengine ya kazi akaniomba nije nimwakilishe, siku akipata nafasi atakuja.
"Sango ni mjumbe wa mkutano mkuu Taifa na kulingana na Katiba ya CCM kiongozi yeyote anaweza kushiriki kusukuma maendeleo kwenye eneo lake, na yeye akiwa mjumbe wa mkutano mkuu ametushirikisha kupitia kundi lake la mtandaoni la WhatsApp la marafiki wa Sango, leo nimemwakilisha mimi siku nyingine asipokuja yeye atawakilishwa na marafiki zake wengine" amesema Airo.
Risala ya shule za msingi katika Kata hiyo waliomba kupatiwa mashine ya kuchapa pamoja na jezi za michezo ambapo Airo amesema kuwa amefika katika kata nne kukabidhi madawati na kata hizo changamoto kubwa ni upungufu wa madawati na uhitaji wa mashine ya kuchapa mitihani.
"Kila shule ukienda kilio ni madawati na photokopi mashine, nimeichukua changamoto hiyo nitajitahidi kabla ya wanafunzi kufanya mitihani mashine hizo ziwe zimefika shuleni "amesema Airo.
Diwani wa Kata ya Bukwe Opino Nickson amesema hujio wa Lakairo sio wa kuomba kura bali lengo lake ni kusukuma maendeleo hivyo isichukuliwe tofauti.
Diwani wa Kata ya Nyathorogo Godfrey Nyagwal amewashukuru wadau hao wa maendeleo kwa msaada huo.
"Tumejenga madarasa na zahanti kwa nguvu za wananchi na wadau wa maendeleo, hakuna mchango wa serikali kwenye ujenzi huo, tunakushukuru Airo na Sango kwa kutupatia madawati na ahadi zungine " amesema Diwani.
Irine Elija amemshukuru Sango Kasera pamoja na Lakairo kwa msaada wa madawati kwakuwa yatasaidia kupunguza changamoto kubwa ya uhaba wa madawati.
Mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Manyara katika kijiji cha Kowak, Night Lazaro amesema darasa la kwanza na darasa la pili wanaketi chini hawana madawati
Ameongeza kwamba darasa la saba wanakaa wanne wanne kwenye dawati moja na amewaomba wadau wengine kusaidia kutoa madawati shuleni.
Post a Comment