HEADER AD

HEADER AD

WAJANE KETARE WAISHUKURU KAMATI YA MAANDALIZI KWA KUWAKUMBUKA MAADHIMISHO YA WANAWAKE


>>Wasema tangu wazaliwe ndio mara ya kwanza wajane kutembelewa na kupewa msaada

>> Waomba wajane wote wafikiwe kwani Kata hiyo ina wajane wengi

>>Diwani Kata ya Ketare asema tukio la wajane kutembelewa katani kweke ni la kwanza kutokea

Na Dinna Maningo, Tarime

WAJANE katika Kata ya Ketare Halmashauri ya Mji wa Tarime, mkoani Mara wameonesha kufurahishwa kwa tukio la Wanawake wa Tarime mjini kufika kuzungumza nao na kuwapa misaada mbalimbali ya vitu.

Halmashauri ya Mji wa Tarime kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii  wakiongozana na Kamati ya Maandalizi ya kufanikisha maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani chini ya Mwenyekiti wa kamati Noellah Gachuma wamefanya maadhimisho ya kuelekea siku ya wanawake Duniani.

Wanawake wa Tarime mji, viongozi wanaume wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajane wa Kata ya Ketare

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi, 5, 2024 katika viwanja vya shule ya msingi Kibumaye katika Kata hiyo ambapo kilele chake ni Machi, 8, 2024 yatakayofanyika kimkoa wilayani Bunda.

Wajane wa Kata ya Ketare wamesema kuwa kitendo cha wanawake wenzao kuwatembelea, kuzungumza nao na kuwapa wajane wapatao 20 msaada wa sukari, mchele, mafuta ya kula, sabuni ya unga, shuka, unga wa ngano kimewapa faraja na kujiona si wapweke huku wakiwaomba kuendelea kuwakumbuka wajane wengine ambao hawajafikiwa.

                   Modesta Paul

Modesta Paul maarufu mjane amesema " Wanawake wenzetu Mungu awabariki sana kufika Ketare kujumuika na sisi, tumefurahi sana na kutuondoa upweke. Mimi nina miaka karibu 60 sijawahi kuona hili tukio kwenye Kata yetu, mimi nina miaka 10 kwenye ujane kiukweli mlichokifanya hilo wazo amewapa Mungu.

"Kutushika mkono wajane ni jambo jema sana Mungu awabariki, tunawashukuru sana kwa hiki mlichotupatia Mungu awaongezee na awabariki kwa kutenda jambo jema, wangepatikana watu 100 kama hawa wajane tungesonga mbele" amesema Modesta.

Baadhi ya wajane na waze wakiwa wameketi

Ameongeza kusema " Kata yetu ina wajane wengi sana ukisema wasimame wote hata wanaume watalia. Ombi letu kwa Serikali tunaomba kuwepo vikundi vya wajane, vikiwepo kiukweli mtakuwa mmetusogeza" amesema.

Elizabeth Mugosi amesema " Tunawashukuru sana wanawake wenzetu, hatuna cha kuwalipa Mungu atawaongezea pele nlipotoa. 

                 Elizabeth Mugosi akiwa amejitwisha vitu alivyopewa (msaada)

Mimi ni mjane mimi ndio mkuu wa familia, kijana wangu aliumia mwaka jana alipata ajali mpaka sasa hivi yupo kitandani, msaada mlionipa utanisaidia sana" amesema Elizabeth.

Lisa Gilbert amesema " Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu wote waliochangia vitu kutupatia sisi Mungu awarudishie mara sabini hata kwenye biblia inasema tusiwatenge wajane.

                  Lisa Gilbert

"Binafsi sikujua kama kutakuwa na mambo mazuri kama haya mimi nilikuja tu kushangilia lakini kumbe wajane tunakuja kupata zawadi, tutakwenda tule tutapata afya na watoto wetu na tutajifunika shuka, Noellah Gachuma nakupongeza sana wewe na timu yako.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya mji wa Tarime Vitus Gwanko ameipongeza kamati ya maandalizi ikiongozwa na Noela  kufanikisha maadhimisho hayo.

Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya mji wa Tarime Vitus Gwanko, Katikati ni Diwani kata ya Ketare Daud Wangwe na Noellah Gachuma

" Idara ya Maendeleo ya Jamii tunafanya kazi na taasisi mbalimbali kiukweli kamati hii imejitahidi sana kwa sehemu kubwa , ushirikiano ni jambo jema. Tuliposema maadhimisho yafanyike wapi kamati yenyewe ikachagua Kata ya Ketare kwasababu kuna maendeleo makubwa yanayofanywa na wananchi " amesema.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni Diwani wa Kata ya Ketare Daud Wangwe amefurahishwa na tukio hilo na kusema halijawahi kufanyika kwenye Kata yake.

Diwani wa Kata ya Ketare Daud Wangwe

"Najisikia majonzi ya furaha mmewatendea hawa wa mama kama kristo anavyotutendea, mmesimama badala ya kristo, kwakweli mmefanya vizuri naomba wajane wengine ambao hawakubahatika kwa leo Mungu ataendelea kuwafungulia njia.

" Mimi nilikuwa sijawahi kuona haya mambo kwenye Kata yangu nayaonaga tu pale mjini, leo yamefanyika hapa ni jambo kubwa, mliyoyafanya hapa ni umoja na upendo yaani nimefurahi sana hata nashindwa cha kusema" amesema Diwani.

Ameongeza " Dada Noellah hongera sana kwa shughuli hii, huwa nakusikia mara unapewa uenyekiti wa maafa na matukio mengine unakuwa mwenyekiti, mi nikadhani labda jina la baba yako ndio linakubeba kumbe una mikakati mikubwa hivi hongera sana" amesema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo Noellah Gachuma amesema hawakupenda kutoa msaada hospitali na Gerezani kwakuwa wengi huenda huko hivyo wakaona wawaguse wajane nalo ni kundi muhimu linastahili kufikiwa huku akiwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kufanikisha jambo hilo.

                     Noellah Gachuma

" Hili jambo hatujalifanikisha wenyewe tumeungwa mkono na baadhi ya wadau wametuwezesha michango ya fedha, na vitu tulivyotoa, pia usafiri kufika hapa kwa ajili ya maadhimisho na shughuli nzima imegharimu kiasi cha Tsh. Milioni 2.5.

"Naishukuru Kamati ya maandalizi kwa mawazo yao na michango ya fedha tumeshauriana vizuri na jambo limeenda salama, nami ni mjane nina watoto wanne najua changamoto za wajane naomba Mungu aendelee kuwalinda ili mlee vizuri familia zenu" amesema Noellah.

Amewataja wadau waliochangia kufanikisha maadhimisho hayo ni Kamati ya Maandalizi, Wilfred Nyehita aliyechangia mafuta ya kula, Chacha Soya, Finius Waheke, Julius Gimunta, 

Wengine ni Mama Mkoi, Mseti Goldland, NMB Benk, FINCA, NSSF, DIMA Online, CWT Tarime, Meneja TARURA Mhandisi Charles Marwa, Jackson Waitara, Zabron Joram, Mama Kasimili na Regina Mbushi.

Picha za baadhi ya Wajane wakikabidhiwa na aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Tarime mji ambaye ni Diwani kata ya Ketare Daud Wangwe.


























            MC Regina Mbushi

          wanafunzi wa shule ya msingi Kibumaye
 Polisi Tarime Rorya

No comments