HEADER AD

HEADER AD

AIRO, OCHELE WASEMA HAKUNA WAKUWAZUIA KUTOA MISAADA KWANI RORYA ITAJENGWA NA WANARORYA


>> Wasema watu wasizuie misaada bali wajibu mapigo kwa kutoa misaada zaidi

>> Wawashangaa wanaozuia misaada wakati wao hawatoi misaada

>>Wasema anayezuia misaada ana ushamba wa uongozi

Na Dinna Maningo, Rorya

MBUNGE Mstaafu Jimbo la Rorya Lameck Airo maarufu Lakairo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Rorya Mkoani Mara, Charles Ochele wamesema hakuna mtu wa kuwazuia kutoa misaada kwakuwa Rorya itajengwa na wanarorya.

Viongozi hao wastaafu wameyasema hayo April, 14, 2024 wakati walipofika kuzindua madarasa mawili na choo cha walimu katika shule ya msingi Masara kijiji cha Randa, Kata ya Kigunga.

          Madarasa yaliyojengwa Gilbert Simon Mwenye ulemavu wa viungo

Madarasa hayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi na kukomea usawa wa madirisha na kisha Gilbert Nyamitah mwenye ulemavu wa viungo aliyelelewa na kusomeshwa na Airo kuendeleza ujenzi huo wa madarasa na kuyakamilisha pamoja na kujenga choo cha walimu cha matundu manne huku akitoa madawati 30.

Mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM Charles Ochele amesema kuwa hatoogopa kutoa misaada kwani miradi yake mingi ipo wilayani humo ambapo mapato anayoyapata yanatokana na wananchi hivyo hanabudi kuchangia maendeleo Rorya.

Mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Rorya Charles Ochele akizungumza na wananchi wa kijiji cha Randa

" CCM hoyee, Masara hoyeee, mimi miradi yangu yote ipo hapa Rorya, mapato yangu makubwa yanatokana na wananchi wa Rorya , ukienda kunywa mafuta kwenye sheli yangu ujue na mimi umeniinua.

"Asilimia ya bodaboda wananichangia mafuta kwenye sheli yangu, kwahiyo hata wakinizuia kwa barua mimi nitarudi tena, sitaki mtu wa kunitishia katika kusaidia jamii ya Rorya, wewe nitishie kwenye mambo mengine lakini siyo kutishia kwenye jamii ya Rorya.

"Kwahiyo ule mchango wenu mlioutoa na mimi narudisha kwenu kwa ajili ya kuchangia maendeleo, sasa wewe unaponipiga majungu unataka nipeleke usukumani? kwahiyo lile katazo mi nadhani tuachane nalo" amesema Ochele.

Ochele amesema kuwa ni wachache wenye moyo wa kutoa japo walio na fedha ni wengi huku akichangia sh. 800,000 kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Masara na Tsh. Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Masara.


Mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Rorya Charles Ochele akimkabidhi fedha mkuu wa shule ya msingi Masara kwa ajili ya ukarabatu wa shule ya msingi na ujenzi wa shule ya skondari Masara

" Kuna watu ukienda kumuomba hata elfu 10,000 anajifikilia kutoa lakini Lakairo mimi ukinialika siwezi kujifikilia kutoa. Nataka nikuhakikishie leo nitachangia laki nane hapahapa keshi, kwenye sekondari nachangia milioni moja keshi na niwahakikishie tutashirikiana kwenye maendeleo .

" Juzi nimeona Mwenyekiti wa CCM anahangaika kuzuia watu kuchangia. Rorya tutaijenga sisi wenyewe. Wewe ukijipima uwezo wa kuchangia, ukisikia Ochele ametoa Milioni moja wewe nenda katoe Milioni 10 ndiyo wananchi watafurahi.

"Lakini uking'ang'ana na marufuku, onyo hapana, kwani tulianza kujenga shule Rorya sisi wenyewe wanarorya, tunataka maendeleo hatutaki onyo, wanarorya tumezoea kusaidiana kwa shida na raha.

Mwenyekiti huyo amewaomba wananchi pindi watakapohitaji msaada katika ujenzi wa shule wasisite kumuita na kwamba hatoogopa kusaidia.

       Mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Rorya Charles Ochele (aliyevaa shati nyeupe) pamoja na viongozi wakikagua vyoo

"Mimi nimeona Sango ametoa madawati eti wamemlima barua, eti marufuku Sango kugawa madawati, eti achukue madawati apeleke kwa DC alafu DC ndio aone maeneo ya kupeleka inawezekana kweli ! .

"Sango anaweza kupata ubunge hata bila kugawa madawati, mambo ya ubunge ni riziki ya Mungu inaletwa na Mungu mwenyewe. Niwaombe mkilemewa kwenye sekondari msisite kuniita " amesema Ochele.

Mbunge Mstaafu Lameck Airo maarufu Lakairo ameshangazwa na wanaopinga misaada na kusema kuwa wabunge waliopita hawakuzuia watu kutoa misaada na kwamba wanaokataa misaada wana ushamba wa uongozi.

      Mbunge Mstaafu Lameck Airo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Randa

"Msijemkamshangaa Diwani wenu hayupo hapa wamepigwa stop kwamba sehemu anayokanyaga Airo msiende, anakokanyaga Ochele msiende. Leo madarasa haya yanazinduliwa Mh. Diwani hayupo, mwenyezi Mungu anamuona, tumwachie Mungu, akija hapa mpikieni ugali mkubwa ale, uji anywe.

"Mhe. Oyombe alikuwa mbunge mimi nilikuwa kijana mdogo chini ya miaka 20 nilianzisha ligi ilikuwa inaitwa Okambo Cup  Mh. Oyombe hakuja kuzuia Okambo Cup., Sarungi amekuwa mbunge hakuzuia ligi tena zilikuwa nyingi Lakairo Cup, Wembe Cup, Diwani Cup, Mwenyekiti wa Kijiji Cup n.k. hakuna aliyezuia.

Ameongeza kusema kuwa katika uongozi wake hakuzuia misaada " Mimi nimekuwa mbunge miaka 10 nilikuwa natoa ratiba yangu na nilikuwa nasema anayejisikia tuungane, na wapo waliojitokeza tukazunguka nao nanyi mliwaona.

        Mbunge mstaafu Lameck Airo akizindua moja ya darasa lililojengwa na Gilbert Simon

"Hivi wewe ukizuiliwa na unataka kwenda kuomba ridhaa kwa wananchi wakufahamu utaombaje? hata chama kitapata hasara kumleta mtu asiyejulikana.

"Sisi tumeshaamua kuwa tukitaka kupeleka msaada kwa wananchi kama ni zawadi tutakabidhi wananchi kama ni madawati wakiamu yanyeshewe na mvua basi, shule si ni ya wananchi? hivi nikileta madawati niwakabidhi mtayaacha? " Lakairo ameuliza huku wananchi wakijibu hapana.

Amesema kuwa kiongozi mzuri ni yule anayeona mtu analeta msaada na kumuunga mkono na kwamba kutoa misaada kwa wananachi ni kuijenga serikali ya mapinduzi.

      Choo za walimu zilizojengwa na Gilbert Simon

" Eti wanapiga stop wasipokee madawati kutoka kwa mjumbe wa mkutano mkuu Taifa wa CCM kama sio wivu ni nini?, mi nafikiri kuna ushamba wa aina nyingi, huyo anayezuia ana ushamba wa uongozi.

" Mfano Rais Samia aliwaambia wanachadema mnataka kuandamana muandamane, wameandamana hadi soli imeisha wamepoa. Ukitaka kuwa kiongozi mzuri wewe mbunge huyo anayeleta simenti ,huyu madawati, yule mabati hawa wote wanaleta kwenye utawala wako na unaijenga serikali ya mapinduzi.

" Huyo anayetoa msaada hana serikali anamsaidia Rais Samia kufanya kazi. Leo nilikuwa naona kwenye mitandao kuna bwana mmoja kule Moshi amepeleka madawati 50 wananchi wamepokea kwa shangwe wala hajapita kwa DC ametoka Dar es Salaam ameona kuna upungufu wa madawati kwao amepeleka."amesema Lakairo.

Airo amechangia Milioni moja kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Masara na sh. Milioni moja ujenzi wa shule ya sekondari Masara na kuahidi kuendelea kushiriana na wananchi hao pindi watakapohitaji msaada .

Diwani wa Kata ya Nyathorogo Godfrey Damas amewataka wana Rorya kuweka siasa kando na badala yake wafanye maendeleo kwani suala la maendeleo ni la wanarorya hivyo halina mbadala.

      Diwani wa Kata ya Nyathorogo Godfrey Damas akizungumza na wananchi

Gilbert Nyamitah mwenye ulemavu wa viungo mkazi wa Dar es Salaam mzaliwa wa kitongoji cha Masara, kijiji cha Randa wilayani Rorya amesema kwa sasa siasa imepamba moto na inaleta changamoto ya maendeleo katika wilaya ya Rorya .

" Hilo lipo wazi halipingiki najua wengine wanakatishwa tamaa ya kufanya maendeleo kwasababu za kisiasa, ukionekana upo na mtu fulani ukifanya kitu fulani watakuuliza kwanini, kwanini ifanyike hivi" amesema Gilbert.

Amewasihi viongozi kuwa makini linapokuja suala la siasa lisiathiri maendeleo huku akiwataka kutoogopa kusema ukweli na kutetea jambo ambalo ni sahihi.

        Gilbert Simon akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi, walimu akiwa na cheti cha pongezi alichozawadiwa na uongozi wa shule ya msingi Masara kwa ujenzi wa madarasa na choo

" Viongozi wa kijiji hasa kitongoji cha Masara linapokuja suala la siasa kuweni makini msiangalie nani anawaambia nini, semeni, fuatilieni na mkuze maendeleo yanayofanyika mahali husika. Msisumbuliwe , msitishwe wala msiogope kusema ukweli kutetea kile ambachi ni sahihi.

"Leo nimemkaribisha baba yangu mlezi Lakairo na rafiki yangu Ochele kuzindua madarasa mawili niliyoyajenga kwa Tsh. Milioni 30, wananchi walianza kuyajenga wakaishia usawa wa madirishwa kwa kuchangia kiasi cha Milioni 6 kisha mimi kuyamalizia. Nimejenga choo cha walimu matundu manne kwa Tsh. Milioni 10" amesema Gilbert.

Amewashukuru wananchi kwa kuchangia maendeleo huku akiwaomba wanarorya wanaoishi nje ya Rorya kurudi nyumbani kuchangia maendeleo Rorya.

      Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Randa 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Randa Joseph Isaya Ongang' amemshukuru Gilbart kwa kuwaondolea wanakijiji mzigo wa michango na kujenga madarasa.

A mesema wapo watu wenye uwezo lakini hawasaidii huku akimshukuru Lakairo na Ochele kwa kuchangia fedha ujenzi na ukarabati wa shule.

   Mwenyekiti wa Kijiji cha Randa Joseph Isaya Ongang

      Lameck Airo akimkabidhi Gilbert Sumon cheti cha pongezezi kwa kujenga madarasa kilichotolewa na uongozi wa shule hiyo.
 
       Madawati yaliyonunuliwa na Gilbert Simon

      Madarasa ya shule ya msingi Masara









No comments